Stories of Change - 2021 Competition

Ntaganda boy

Member
Jan 16, 2016
90
59
MAHUSIANO YANAVYOATHIRIWA NA MAGONJWA YA HAIBA (PERSONALITY DISORDERS AND RELATIONSHIP)

Habari zenu JamiiForums, hususani jukwaa hili la stories of change. Ni tumaini langu nyote ni wazima
Haiba
: Ni urithi au vitu unavyozaliwa navyo na baadhi kutoka kwenye mazingira na kukufanya au kumfanya binadamu kuonyesha matendo/tabia, hisia/mihemko na ufikrio/fikra kwa watu au kwa mazingira aliyopo huyo mtu. Mfano haiba ya ucheshi, hasira, majivuno, kusaidia watu na ugomvi.

Magonjwa ya haiba: Ni hari inayoadhiri au kumwadhiri binadam na kusababisha kuonyesha tabia zisizokua za kawaida (kuzoeleka kwa jamii) anapokua kwenye mazingira Fulani au anapokua na watu, mfano; kazini, familia, marafiki, shule na sehemu za ibada. Baadhi ya tafiti zinasema magonjwa ya haiba mtu hazaliwi nayo ila ni namna huyo mtu alivyokuzwa (environment/parenting style) na kusababisha kuzuka kwa tabia za kujirudiarudia na kupelekea kuwepo na ugumu hasa kwenye kuingiliana/kujamiiana na watu (socialization), hapo ndipo shida ya mahusiano inapoaanzia. Mifano ya magonjwa ya haiba na sifa zake kwa uchache;

1. Haiba ya ubishi (paranoid personality disorder) – sifa, kutoamini mtu mwingine pale anapoambiwa jambo ingawaje anaweza kuwa halijui hilo jambo.

2. Haiba ya ubinafsi (schizoid/schizotypal personality disorder) – sifa, kupendelea kuwa wapekee na kuwq wagumu kuonyesha hisia zao kwa watu au vitu, kufikria na kuongea na kuonyesha tabia zisizofaa na wakati mwingine kuwa kuona na kusikia vitu wengine wasivyokua na uelewa navyo. Hizi zimewekwa kwenye makundi kwa ufanani wingi wa sifa zao.

3. Haiba ya jamii-chukizi (antisocial, borderline, histrionic, narcissistic personality disorder) – sifa, kuwa na wasiwasi juu ya watu wengine, kupatwa na unyongofu/sonona mara nyingi, kuwa na tabia za kuwaumiza wenzao na kutokua na hisia juu yao, kuchagua marafiki wakua nao, kuwa na hasira za mara kwa mara, mihemko/hisia kubadilika, mawazo ya kujidhuru au kuwadhuru wengine, kujisifia sana au kupenda wengine wamsifie sana na kujihisi yeye ni mtu maalumu kuzidi wengine na kuwa mada ya mazungumzo hasa kwa kumtaja yeye tu. Hizi zimewekwa kwenye makundi kwa ufanani wingi wa sifa zao.

4. Haiba ya sizihitaji (avoidant personality disorder) – sifa, kuwa na fikra juu ya kitu inayokatishwa na uoga anaokuanao ndani, kuwa na hisia kali juu ya kukataliwa na kupelekea kujitenga na kitu, kuwa na ukomo kwenye mahusiano, kuepuka kazi zenye mahusiano na maisha yake na huogopa kuanzisha kitu kipya hasa zaidi chenye uhatari ndani yake.

5. Haiba ya utegemezi (dependent personality disorder) – sifa, hupendelea kukaa chini y uangalizi wa watu wengine, tabia za utiifu, hawezi kutengeneza hoja au kuingia kwenye mdahalo wa hoja kinzani, kushindwa kuwa na maamuzi na kushindwa kusimamia maamuzi na kuwa na fikra za kutoweza kujisimamia kwenye maisha yao ya kila siku.

6. Haiba ya ulazimishi pindukizi (obsessive compulsive disorder) – sifa, mawazo mengi juu ya kuyaendesha mazingira yaliyomzunguka, ugumu wa kukubaliana na mabadiliko kwenye vitu, hutawaliwa na kanuni na sharia zinazompelekea fikra za kuwa mkamilifu wa kila jambo, kufanya vitu kwa ratiba, kujilimbikizia pesa na vitu visivyo na dhamani kwa wengine ila muhimu kwake tu na watu wanaotumia muda mwingi kwenye utendaji wa kazi kutengeneza dhana ya ukamilifu wao.

Mahusiano: Jinsi/namna watu au vitu vinakua na ukaribu na mwingiliano na kuonyesha tabia, hisia na fikra hasa kwa binadamu. Baadhi ya wataalam wanataja aina nne za mahusiano ambayo na mimi nitajikita hapo, kwanza ni mahusiano ya kifamilia, mahusiano ya kirafiki, mahusiano ya kitaaluma na mahusiano ya kimapenzi. Uzii huu utajikita zaidi kwenye mahusiano ya kimapenzi na jinsi gani yanaadhiriwa na magonjwa ya haiba kama niivyoandika mwanzoni na kuelezea magonjwa ya haiba na kuelezea kwa ufupi sifa zake kwa kuzitaja tu.

Mahusiano ya kimapenzi (romantic relationship): Ni moja ya mahusiano yenayohusisha mwingiliano wa mihemko/hisia na migusano ya miili zaidi na kujumuisha tendo la ndoa. Mahusiano ya kimapenzi huanza na hatua tofauti tofauti kwa kutegemea wahusika wamekutana wapi, saa ngapi na mengineyo mengi. Kwenye mahusiano ya kimapenzi jinsi mbili tofauti (moja kwa utamaduni wan je hasa nchi za ughaibuni) huvutiwa na vitu mbalimbali vinavyowashawishi wao kuwa pamoja, mfano wa vitu hivyo ni mwaonekano wa mwili, kazi anayofanya mtu, mpangilio wa uvaaji na mikogo ya namna ya kutembea, ukaribu wa mazingira wanayoishi, uwezo wa uchumi uliopo, kufahamiana kwa muda mrefu na mfanano wa hisia kwenye kupokezana.

Nitatumia kitabu cha Gary Chapman: The Five Love Languages, kuhusianisha na magonjwa ya haiba kwa sababu kitabu hiki kimetumiwa na watu wengi duniani kama kielelzo cha namna watu wanaelezea na wengine wanapenda waelezewe kwa vitenda na kuonyeshwa wanajaliwa na wenza wao.

Uthibitisho wa maneno (Words of affirmation) – maneno yanayovutia na kuonyesha umiliki hudhibitisha upendo kwao, mfano we ni mzuri, umependeza, nakupenda, wewe ni wa kipekee, umeumbika, n.k. Upekee huweza kutengenezwa kwenye akili yake na kusababisha kuwa na hisia zaidi kwako.

Kutoa huduma (Acts of service) - kuwahudumia na kuhudumia vitu wavipendavyo, mfano kumuangalia chai/chakula na kumtengea, kumwagilia maua pamoja, kuosha vyombo pamoja, kumfungulia mlango wa gari, kumwandalia kiti akiwa anakaa n.k

Utoaji wa zawadi (Receiving gifts) - mapendeleo zaidi ni zawadi zinazobebeka au zinazogusika, mfano maua, nguo, pipi, chocolate, gari n.k. Hii hupendeza zaidi kwa kuangalia vitu avipendavyo vilivyo ndan ya mhusika.

Kutumia muda pamoja (Quality time) – mizizi ya uthamini wa penzi lako upo kwa kipimo cha muda unaotumia kuwa nae, kufanya nae vitu pamoja, kucheza nae n.k.

Mgusano wa viungo vya mwili (Physical touch) – unapokua nae ni kwa kiasi gani humgusa na kumshikashika, mfano mkiwa mnatembea kumshika mkono, wakati unamtamblisha kwa marafiki kumshika kama kiashiria cha umiliki na kujali n.k. Hii husaidia pia kuongeza msukumo wa ufanyaji wa tendo la ndoa.

Ufafanuzi kidogo, kuna watu wanahitaji zaidi ya lugha moja lakini kuna moja wapo inayofanya kazi zaidi na ukiitumia utamuona zaidi anafurahia na kuongeza ukaribu tofauti na zingine japo zitahitajika pia.

Swali
: kwa kutumia sifa chache tulizoona juu ya magonjwa ya haiba, ni kwa namna gani unaweza kuwa kwenye mapenzi/mahusiano/ndoa?

Wanataaluma wa haiba na magonjwa yake na tafiti mbalimbali wanapendekeza kwa watu wenye magonjwa ya haiba kuonana na kuongea na wanasaikolojia watakaosaidia juu ya mbinu mbalimbali za kuishi na kukabiliana na haiba hizo kwa sabbu kwa watu wazima kuanzia miaka 21 na kuendelea kutibu ugonjwa wa haiba ni changamoto na hutumia miaka na miaka na magonjwa mengine ya haiba hayatibiki ila kuna mbinu za kuishi nayo.
Nichukue nafasi kuwashukuru wasomaji wote mliotumia muda wenu kusoma na niwaombe mnipigie kura kwenye hili shindano la hapa #JAMIIFORUMCHALKEMGE

By Ntaganda Boy
 
Dawa kuachana tu
 
Uchambuzi mzuri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom