Magomeni Kilosa ni mafuriko ama gharika?

Wasioijua kilosa watachanganya habari kuwa ni bondeni but ukweli location ya mto imehama kutokana na serikali kujenga tuta upande wa mjini na kuacha upande wa magomeni. Mkuu na mimi nimesoma lamulilo hapo
Hahaha pamoja mkuu, hii sio mara ya kwanza kwa serikali kujenga tuta upande wa mjini, lilijengwa tuta miaka ya zamani likaondolewa na mafuriko ya 1998/99
 
Zamani kulikuwa na tuta
Hahaha pamoja mkuu, hii sio mara ya kwanza kwa serikali kujenga tuta upande wa mjini, lilijengwa tuta miaka ya zamani likaondolewa na mafuriko ya 1998/99
kubwa upande wa Magomeni maeneo ya pump station kote huku. Lakini sehemu kubwa halikuwa kubwa kama la mbumi ba behewa kwasababu ya ground level, huku kumeinuka na mbumi na behewa ni bondeni
 
Zamani kulikuwa na tuta

kubwa upande wa Magomeni maeneo ya pump station kote huku. Lakini sehemu kubwa halikuwa kubwa kama la mbumi ba behewa kwasababu ya ground level, huku kumeinuka na mbumi na behewa ni bondeni
Du kama ni ivo ipo shida kubwa aidha watu wanatakiwa wahamie kule miliman au ukivuka pale daraja la mwidu kama sikosei kupo juu kidogo
 
Shida moja kubwa ya nchi hii nikuwa na watendaji wasio na weredi wa kutosha kwenye maeneo yao ya kazi.

Kawaida maeneo yasiyofaa kwa kitu chochote ndiyo yanapaswa kuwa makazi. Lakini kwetu eneo lenye unyevunyevu wa kutosha na rutuba nzuri watu wanajenga.

Mipango miji ovya halmashauri zipo tu zinashangaa. Hatawao wanagawa viwanja maeneo ya kilimo baadala ya kugawa maeneo ya miinuko Ambayo hayafai kwa shughuri za uzalishaji
 
Chacha limekutoka au ulimaanisha unataka kufurahi kuona watu wanataabika??
 
Mtu umesombwa mara ya kwanza ukapona,tena ukarudi hapo hapo uliposombewa mara ya kwanza as if hakuna masika nyingine hivi mtu wa aina hii anakuwa vizuri upstairs kweli?

Hivi hili nalo mpaka serikali kweli? Kwani iliyowajengea hapo ni serikali?

Ingekuwa hayo maafa ndo yanatokea kwa mara ya kwanza inge-make sense lakini haya ya kila mwaka ni uzembe na ni upuuzi kuendelea kuilalamikia serikali.

Mbona sehemu salama kwa makazi ipo yakutosha tu tena at affordable prices.
 
Mafuriko makubwa zaidi yaliyotokea leo katika eneo lote la Magomeni Kilosa ni ya kushtusha. Nadhani ni busara serikali ikachukua hatua madhubuti na za kudumu kuliondoa tatizo hili.

Ingawa kwenye mafuriko yaliyopita kulitokea ahadi mbalimbali ikiwepo ya kuwajengea makazi mapya wakazi hawa lakini baada ya kukaa makambini kule eneo la Kiwanda cha mazuria walirudishwa tena makwao.

Sijui safari hii mafuriko haya yatasababisha maafa kiasi gani lakini tayari yamesambaa mji mzima na nyumba kadhaa zimekwishaanguka.Ingalie pia busara za kujenga tuta upande mmoja ambao sehemu kubwa ndio njia rasmi ya maji na kuacha upande wa pili bila tuta na kuwa dhaifu kiasi kwamba maji yetu yakasambaa upande huo na kusababisha madhara makubwa kiasi hiki.

Pia namuomba mheshimiwa raisi aombe orodha ya walioathirika kwenye mafuriko ya mwanzo yote na kuhakiki mmoja mmoja kama walipewa viwanja kama walivyoahidiwa au viwanja viliishia kwa wajanja wachache.

Pia reli ambayo ilijengwa hapo zama za kale kwa teknolojia ya kale ingetafutiwa njia mbadala badala ya kuishia kuikarabati wakati tunajua ni zoezi lenye kushindwa.

Mungu watie wepesi wakaazi wa Kilosa.

Mafuriko yanazidi kufanya uharibu eneo la Magomeni Kilosa muda huu. Mji wa Magomeni umegeuka bahari na unaendelea kuangamia.
picha pliz, yamefika kwa zaid zaid, genery au lamulilo?
 
Nimekulia kilosa nimesoma shule ya msingi lamlilo magomeni kilosa, naufahamu sana huo mto unaitwa Mkondoa,nimevua samaki nimeogelea sana kwenye huo mto na tunamashamba kando kando ya mto huo, ila sijui huu mto unamatatizo gani kila mwaka unatengeneza mkondo mpya wa maji, japo hapo zamani serikal iliweka matuta lakini wapi yaliondoka yote, vilevile kilosa centre mvua hainyeshi isipokuwa utaona tu mafuriko makubwa inasemekana maji yanatoka bwawa la mtera na maeneo ya dodoma na morogoro aidha mara nyingine tulikuwa tunambiwa maji yanafunguliwa kutoka bwawa la Mtera hivyo msiende mtoni .Kinachoniuma zaidi ni kwamba mafuriko yameingia nyumbani kwa bibi na kwa mjomba pia kwenye kaburi la mama yangu mzazi,babu na ndugu wengine kama familia tunafikiria kuamisha famila ije kilosa uhindini au mlimani maanke hii mara ya pili sasa mafuriko yanafika pale home
Poleni. nendeni manzese au MYombo. kule maji hayafiki
 
Yamesambaa Masanze, Maeneo ya msikiti wa kiyangayanga kwa Salum Zaidi, Kwa Mzee Shomari kote ni maji.
 
Back
Top Bottom