Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,434
- 1,985
Wapendwa waTz wenzangu! Hawa watu hawajuwi wajibu wao. Na zungumzia FIRE, NEMC, TBS, WASANIFU WA MAJENGO, na wahusika wengine.
Majengo mengi yameungua katika kipindi cha miaka 10 hadi 20 iliyopita ikiwa ni pamoja na mabweni ya shule kama Shauritanga nk., magorofa kama waterfront tower, kitegauchumi, hoteli ya kitalii na ikulu yenyewe hapa DSM, enzi za Mkapa. Tena ilikuwa baada ya ukarabati mkubwa wa ikulu uliofanywa mwaka huo. Kibaya zaidi kabla ya tukio la moto mtaalamu ambaye kwa usalama wake sitamtaja hapa aliwashauri kuhusu viwango vya materials kama rangi, makapeti, mapazia, makochi, nk. kama vilikuwa salama kwa masuala ya moto. Washauri wa serikali wakampuuza. Si muda mrefu baadae sehemu fulani ya ikulu ikaungua!
Sasa nataka kusema hivi:
1. TZ haina kitu kinachoitwa FIRE CODE kama kipo yawezekana hakikidhi mazingira yaliyopo au hakiheshimiwi miongoni mwa wadau na walengwa wake.
2. Baadhi ya wadau ni ZIMAMOTO, POLISI, TBS, NEMK, BODI YA WASANIFU UJENZI, IDARA YA UHANDISI YA JIJI, WIZARA YA UJENZI (construction materials testing lab) na wengine.
3. Baadhi ya mambo ya kuzingatiwa kwenye FIRE CODE; pamoja na vifaa na vigezo vya tahadhari ya moto ni kuwa na sheria (by-laws) za kuwalazimisha wenye miradi ya majengo marefu na viwanda vikubwa na vidogo kuchangia gharama za magari na vifaa kwa kikosi cha zimamoto na uokoaji katika mji husika ili kiweze kuhudumia majengo kama hayo katika ajali za moto na mambo engine. Jambo hili hutekelezwa wakati wa kuomba kibali cha ujenzi na Environmental Impact Analysis.
4. Kabla ya kupigwa marufuku (katika dunia ya wenzetu), asbestos ilitumika kwenye ujenzi kujihami na moto. Hapa kwetu pamoja na NEMC, TBS, BODI YA WASANIFU UJENZI tulionao, asbestos inayosababisha saratani ya mapafu IPO na tunalishwa hewa ya vumbi lake mitaani kwenye magereji. NEMC na wenzi wao wapowapo tu!
5. Ufisadi sio lazima rule rushwa tu, hata kitendo cha kupuuza ushauri halali ili kulinda usalama wa afya na mali za jamii nao ni ufisadi.