Magari na Abiria Waliokwama Lindi Waanza Kuruhusiwa Kuendelea na Safari

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,994
961

MAGARI NA ABIRIA WALIOKWAMA LINDI WAANZA KURUHUSIWA KUENDELEA NA SAFARI

Magari ya Mizigo, Mabasi na magari mengine madogo yaliyokwama kwa siku sita katika barabara ya Lindi-Dar es Salaam eneo la njia nne (Mikereng’ende) hadi Somanga yakitokea Lindi kuelekea Dar es Salaam yaanza kuruhusiwa kuendelea na safari.

Hatua hiyo imechukuliwa leo asubuhi, tarehe 09 Mei, 2024 Mkoani Lindi mara baada ya kukamilisha urejeshaji wa mawasiliano katika maeneo ya Mikereng’ende, Songas na Somanga ambayo yalikatika kutokana na mvua zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya.

Akisimamia zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack amewataka wasafiri, wasafirishaji na watumiaji wengine wa barabara kusafiri kwa tahadhari ambapo maeneo mengine yanaendelea na matengenezo.

“Naipongeza Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zilizofanyika ndani ya muda mchache na leo tunashuhudia magari yaliyokwama yameruhusiwa kuendelea na safari”, Amesema Mkuu wa Mkoa.

Aidha, Kazi ya urejeshaji wa miundombini ya barabara ya Lindi - Dar es Salaam eneo la Nangurukuru ipo katika hatua ya ukamilishaji chini ya usimamizi wa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Timu ya Wataalam kutoka
Wizara ya Ujenzi na Wakala ya Barabara (TANROADS)

Kwa upande wa wananchi, Wameishukuru Serikali kwa namna ambavyo wamerejesha mawasiliano ya barabara kwa vipande hivyo na kuweza kuruhusiwa leo baada ya siku sita kukwama katika barabara hiyo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.17.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.17.jpeg
    232.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.18.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.18.jpeg
    402 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.19.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.19.jpeg
    694.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.20.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.20.jpeg
    647.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.46.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.46.jpeg
    668.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.47.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.47.jpeg
    632.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.48.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.48.jpeg
    604.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.48(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-09 at 12.42.48(1).jpeg
    715.5 KB · Views: 1
  • MAGARI NA ABIRIA WALIKWAMA LINDI WAANZA KURUHIWA KUENDELEA NA SAFARI.mov
    89.3 MB
Back
Top Bottom