Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,038
- 4,752
Tathmini yangu binafsi inaoonyesha mafunzo ya JKT yanawafanya vijana kuona kama wao ni wanajeshi na kwamba ujeshi ni ukatili kitu ambacho siyo kweli.
Katika ulimwengu ulioendelea mwanajeshi ni binadamu mwenye mafunzo na nyenzo za kuisaidia jamii kukabiliana na maadui na siyo kuwafanya jamii kuwa maadui. Mwanajeshi siku zote ni mtu wa mwisho kuchukua hatua dhidi ya RAIA pale anapokwazwa au kushuhudia uhalifu. Mwanajeshi badala ya kupambana na RAIA anapaswa kuwa na skills zakumwezesha kumdhibiti RAIA na kumkabidhi kwenye mamlaka za kisheria ikiwemo jeshi la polisi.
Kinyume chake watoto wetu wanapokuwa JKT wanafundishwa namna ya kuwapiga RAIA. Wanajielekeza zaidi kuwafanya RAIA adui kuliko rafiki. Kwa mfumo huu wakufanya RAIA kuwa adui wanakosa misaada wa intelijensia ya jamii kuhusu maadui wetu.
Vijana wa JKT wanapohitimu wanakwenda vyuoni na baadaye kwenye ajira. Tathmini inaonyesha vijana hawa wamekuwa wakatili kazini na kuwaona watumishi wengine kama vile wao ni RAIA wa kawaida wasiotakiwa kuheshimiwa.
Tumeshuhudia watoto hawa wenye mafunzo ya JKT wanaoajiriwa kama walimu wakipiga wanafunzi hadi kuua na wakati mwingine kusababisha ulemavu. Ukihoji hii nguvu wanatoa wapi unasikia hawa ni wanajeshi. Nani kawaambia wao ni wanajeshi?
Tumeona watoto hawa ndani ya jeshi la Polisi wanavyotumia nguvu kupora, kuadhibu na kulazimisha mambo bila kujali umri. Wengi wamesoma kupata degree lakini hakuna degree kichwani. Ukienda sekta binafsi mfano miradi ya Suma JKT angalia namna wanavyofanya kwa RAIA. Badala ya kutoa huduma wao wanaamini kila kitu ni nguvu.
Haya yote ni matokeo ya kuwa na mfumo wa mafunzo ya JKT yenye ukatili badala ya mafunzo yenye kuondoa utegemezi na kuingiza kichwani mwa watanzania hawa maarifa ya kujitegemea. Wengi wa hawa vijana wakikosa ajira wanatumia nguvu na ukatili wao kujiingiza kwenye uhalifu.....wanatumia confidence yaliyojengewa kupambana na RAIA badala ya kufanya jukumu la kijeshi lakutoa msaada kwa jamii.
Wazazi msipokaa chini na watoto wenu na kuwaonya kwamba wao siyo wanajeshi na hata kama ni wanajeshi kazi ya wanajeshi siyo kupambana na RAIA mtaishia kuwapelekea wanenu chakula maabusu baada ya kufanya uhalifu ikiwemo kuua.
Mwanajeshi gani anaweza kumchapa mtoto wa darasa la kwanza kwa kuchelewa shule? Tuwaambie wazi hawa watoto wanaokwenda JKT miezi mitatu sijui sita wao siyo wanajeshi ni RAIA wakakamavu tu na kwamba wanajeshi kazi yao kubwa kusaidia jamii siyo kupambana na jamii.
Niwaombeni siku zote tuwakumbushe hawa watoto wao siyo askari wala wanajeshi kwani wanajeshi wetu JWTZ wana maadili yao ya kazi na siku zote wameyatekeleza vyema. Wao wakitambua ni RAIA watawahudumua wananchi badala yakupambana na wananchi