Mafunzo kwa viongozi wa UWT na madiwani wanawake Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
810
513
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na wanachama wake kuyatumia vyema mafunzo wanayopatiwa ambayo yatawajengea uwezo wa utekelezaji wa majukumu yao ili kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika Chama cha Mapinduzi sambamba na kutatua changamoto za wanachama zinapojitokeza.

Ameyasema hayo Mei 11, 2024 katika ufunguzi wa Semina ya siku moja ya kuwaongezea ujuzi na maarifa Madiwani, Makatibu wa Wadi na Majimbo pamoja wajumbe wa kamati tendaji iliyofanyika katika ukumbi wa Viwanja vya Maonesho Nyamanzi Zanzibar Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.

Mhe. Hemed amesema moja ya jukumu la UWT ni kutoa elimu kwa wanachama, kuwahamasisha wanawake katika kugombea nafasi za Uongozi, kuishauri Serikali na kutatua changamoto katika jamii kwa lengo la kuweka mustakabali mwema wa Taifa na chama cha Mapinduzi ili kiendelee kushika Dola awamu kwa awamu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Uongozi ni kuonesha njia kwa wanao waongoza ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na kusema kuwa kufuata maadili ya Uongozi na Utendaji ni jambo la msingi ambalo litasaidia kunyanyua ari kwa wafuasi wa Chama na kuleta maendeleo kwa Jumuiya.

Aidha Mhe. Hemed ametoa wito kwa Viongozi kuzitumia vyema nafasi zao kwa kufuata misingi ya uongozi kwa wanao waongoza ikiwemo nidhamu, uaminifu, uadilifu, unyenyekevu, kujenga umoja, matumizi mazuri ya lugha, kutatua kero na kuandaa viongozi wapya watakaoweza kushika nafasi mbali mbali katika Jumuiya.

Sambamba na hayo, Mhe Hemed amesema anatambua kuwa wapo baadhi ya viongozi na watendaji hawana lugha nzuri kwa wanaowaongoza hivyo amewataka kujirekebisha na kuachana na tabia hiyo kwani Chama cha Mapinduzi hakitamvumilia mtu yoyote atakae kwenda kinyume na maadili ya Chama, hivyo amewahamasisha wanawake ndani ya Chama Cha Mapinduzi wenye uwezo wa kuongoza kujiandaa na kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi katika Uchagzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda amezipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kukamilisha vyema na kwa mafanikio makubwa zoezi la sensa la kidigital ambalo halijawahi kutokea nchini ambalo takwimu zake zitalisaidia Taifa katika kupanga mikakati mbali mbali ya kimaendeleo nchini.

Chatanda amewaagiza viongozi ambao wamepatiwa mafunzo hayo kushuka kwa wananchi kusikiliza kero zao zinazowakabili ili kuweza kufanya maamuzi sahihi katika vikao vya chama na Serikali.

Aidha amewataka viongozi wa UWT kuendelea kufanya zoezi la usajili wa wanachama wapya kwa njia ya kielektroniki ambao watasaidia katika kupanga mikakati ya Jumuiya sambamba na kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi mkuu wa nchi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025.

Mapema Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Zainab Khamis Shomari amesema kuwa Mafunzo hayo waliopatiwa viongozi wa UWT yataleta mabadiliko chanya katika Utendaji kazi wa Jumuiya na Chama kwa Ujumla.

Amesema kuwa UWT wamejipanga kukipigania na kukilinda chama cha Mapinduzi kwa kuhakikisha kinafanya vizuri katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwisho wa mwaka huu na ule uchaguzi Mkuu wa nchi mwaka 2025 CCM inashinda na kuendelea kuiongoza nchi.

IMG-20240511-WA0027.jpg
IMG-20240511-WA0023.jpg
IMG-20240511-WA0024.jpg
 
Back
Top Bottom