Mafanikio ya Sugu na Profesa Jay yalivyowaponza Wasanii na Siasa chakavu za CCM

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,894
44,091
Hali imekuwa ndivyo sivyo. Ni vilio na simanzi . Kila kona ni aibu tupu. Wahenga walisema Tamaa mbele mauti nyuma. Au majuto ni mjukuu.

Inasemekana kuna tofauti kubwa kati ya wasanii wa tanzania, uganda a Kenya, wachambuzi wa maswala ya siasa na uchumi, utamaduni na maendeleo wanasema kundi la wasanii tanzania limejaza watu wasio na mwono wala maono. Wanajiendea endea tu kama kondoo ni watu wa kusukumwa na kwamba hawana uwezo binafsi wa kujikwamua au kujiendeleza ktk sana yao. Kundi hili linahusisha wasanii wa Bongo Fleva na Bongo movies.

Kumekuwa na mlinganisho kati ya Josee Chamilioni na Boby Wine wa Uganda na wachovu wetu mfano akina Diamond, Alikiba, Nick wa Pili, Uwoya, Wema, Harmonizer, Rayvany na wengineo kuwa hawana mwono na wanapenda mteremko.

Kwa upande mwingine Josef Mbilinyi Mr. Sugu na Josef Haul prof Jay wakilinganishwa na wasanii wenye Future wanaojitambua hapa kama Jose chamileon na Boby Wine na wengineo.

Baada ya Muda mrefu ambapo Chama Makini CHADEMA kilizingatia sifa, uwezo na weledi wa kupambania haki za raia, uhuru, uomoja, amani, Maendeleo na haki za binadamu kulikofanywa na Vijana wa Mfano kama Mr Sugu na Prof Jay kwa miaka mingi licha ya kazi zao zilizotukuka kwa kuburudisha na kuleta hamasa kwa vijana kufanya kazi pia walifanikiwa kujenga heshima zao. Chama kiliwaona wanafaa.

Na wao pia walijua ni upande gani wa kuungana nao wenye mwelekeo wa ukombozi wa kifkra. Nakumbuka Mr Sugu na song lake la "Niko mikononi mwa Polisi mwaka 2001"

Sugu akaukwaa Ubunge, prof Jay akaukwa ubunge na wananchi wakamuunga mkono. Vijana hawa walisimama kidete hata wakati wa dhuruba la kuunga mkono kwa hongo z pesa na vyeo.

Wakajijengea majina ndani ya nchi na nje ya nchi na hadi barani ulaya. Record zinaonesha kuwa Mr Sugu ndiye msanii wa kwanza wa music kuwa Mbunge akifatiwa na Prof Jay na Mwingine wa Ufaransa dunia nzima. Hii record ni muhimu mno.

Vichwa maji wengine wakaibuka kama uyoga. Hawana sifa yoyote ya kulinda jamii. Kwanza hawana maadili ktk jamii na hawana weledi wala exposure. Hawna rekodi yoyote ya kutetea maslahi ya taifa zaidi ya matumbo yao. Wakajitokeza mbaya zaidi ktk chama kilichochokwa na wananchi na hadi na wanachama wake. Wooote kama walivyomwagika wakapigwa chini. Hii ni aibu kubwa.

Walipooma wako maarufu instagram na tweeter wakadhani wako na umaaruf huo mitaani. Kibao kikabadilika wasijue cha kufanya. Wamejidhalilisha kwa kukurupuka.

Hata hivyo imekuwa ikisemekana kuwa tangua awamu ya tano iingie madarakani hali ya fedha na mapato kwa wasanii ni mbaya mno. Amekuwa akisikika msanii Diamondi akisema "halii ya uchumi wa Magu sio"

Msanii mwingine Maarufu kama V-money au Vanesa Mdee mwezi uliopita alisikika akidai kuwa hajawahi kuwa na maisha magumu na ya kuigiza kama kipindi hiki. Na hivyo ikapelekea kubwaga manyanga kazi zake zoote za kisanii. Kweli awamu hii imewashusha wengi. Hoja za V-money ziligongelewa msumari na msanii mkongwe wa Hip hop Dudubaya.

Lakini pia mwaka 2018 wasanii waliansdaa tamasha kubwa Leaders club jijin Dar es salaam kwa pesa nyingi ma muda mwingi lakini lilikuja kuzima kwa sababu tu za kisiasa kwa barua iliyotolewa na Mkurugenzi wa Kinondoni Bwana Aron kajirumjuli nov 2018 kwa madai kuwa wagonjwa wa maeneo hayo wametoa malalamiko yao kuhusu kelele za music na shughuli hizo za sanaa. Hoja hizi zilikuwa dhaifu kwani eneo hilo halijaanza kufanyiwa tamasha 2018 tu. Ni muda mrefu sana.

Wivu na tamaa za kutaka kuwa kama Mr sugu na Prof Jay zimewaponza wamebaki wanalialia huku washabiki wao tusijue cha kuwasaidia.

Watu kama akina Amberuty, Diamond, Alikiba, Mwijaku, Wema, harmonzizer, Stev nyerere, Uwoya, hawana sifa yoyote ya kuwa viongozi . Kwa kuwa walijua CCM huko ni shamba la bibi na ni kichaka cha wachafu wote hata huko nako wameonekana hawafai ni aibu kubwa.

Nawaasa wajitafakari kama wamayo sifa ya kuendeleea kuitwa kiyoo cha jamii.

Mwisho kabisa. Wasiache kuunga mkono His Excellence Mh Tundu Lissu ktk safari yenye baraka ya kuchukua nchi.ni mwanasheria mpenda haki atawawezesha wasanii kunufaika na kazi zao kwa kusimamia sheria za hatimiliki na kuinua vipato vyao waepukane na aibu hizi.

Asalam aleykum.
 
Mkuu,

Unapozungumzia wasanii Tanzania ni Pro J na Sugu,wengine wote uliiwataja ni waigizaji na siyo wasanii,kunatofauti kubwa sana Kati ya wasanii na waigizazi,alikuwepo John Komba.hao waigizaji wengine wasubili kampeni zianze wapewe posho wakanengue majukwani kuunga juhudi.
 
Mkuu,

Unapozungumzia wasanii Tanzania ni Pro J na Sugu,wengine wote uliiwataja ni waigizaji na siyo wasanii,kunatofauti kubwa sana Kati ya wasanii na waigizazi,alikuwepo John Komba.hao waigizaji wengine wasubili kampeni zianze wapewe posho wakanengue majukwani kuunga juhudi.
Hahaa asante kwa masahihisho.
 
Siku Upinzani ukichukua nchi hakutakalika kwa aibu za wasaniii wanaojipendekeza sijui wataweka wapi sura zao.
 
Back
Top Bottom