Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Manchester City imeweka rekodi ya kuwa timu kubwa kutoka England ambayo imeshinda mechi nyingi mfululizo. Ikiwa imeshinda mechi 15 , huku ikifunga magoli 40, na kuruhusu magoli 5, ikiwa na clean sheets 10 chini ya Pep Guardiola.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich amefikia katikati mwa msimu wake wa tano akiwajibika kama kocha wa Manchester city.
Pep Guardiola alipata ushindi wake wa 200 kama kocha wa Manchester City siku ya Jumatano tarehe 10 wakati kikosi chake kilipoifunga Swansea City katika mechi yao ya Kombe la FA.
Mabao kutoka kwa Kyle Walker, Raheem Sterling na Gabriel Jesus yalisababisha City kuwa salama na kujihakikishia kuingia robo fainali na ushindi huko Wales kusini.
Pia imeleta historia muhimu kwa Guardiola, ambaye amekuwa mwalimu wa mfano kwa klabu katika misimu yake minne na nusu aliyoongoza.
Mkatalunya huyo alichukua kazi ya kuinoa City mnamo mwaka 2016 kufuatia kazi nzuri aliyoifanya Barcelona na Bayern Munich.
Miaka minne ya Guardiola akiwa madarakani huko Camp Nou aliipatia Barcelona si chini ya mataji 14, pamoja na ushindi mara mbili wa Ligi ya Mabingwa.
Kuwasili kwake kwenye Uwanja wa Etihad kulileta matarajio makubwa kutoka kwa The Citizen, na akaanza vyema kwa kushinda mchezo wake wa kwanza, 2-1 nyumbani dhidi ya Sunderland.
Katika hili, msimu wake wa tano kwenye usukani, Guardiola na City wana uwezekano mkubwa wa kupata tena taji la Ligi Kuu ambalo ilipoteza kwa Liverpool msimu wa 2019-20.