Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,392
- 121,026
Video ya Mafanikio ya TIC chini ya Julliet Kairuki
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Akimsifu Julliet Kairuki na Makubwa Aliyoyafanya.
Shuhudia Jinsi Julliet Kairuki alivyokuwa anahamasisha uwekezaji.
Wanabodi,
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!, japo huyu mama ametumbuliwa, sababu za utumbuzi huo, ni kitu kinaitwa "personal matter", and has nothing to do na utendaji wake TIC, ifike mahali Watanzania tuwe na shukrani kwa mazuri mtu aliyoyatenda na aliyolitendea taifa, licha ya mapungufu yoyote ya kibinaadam!.
Mimi kama mwanahabari huru ninayejitegemea, nimeifanyia TIC kazi za kihabari, tangu enzi za TIC ya Samuel Sitta, TIC ya Ole Naiko na hii TIC ya sasa ya Julliet Kairuki, mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 3 tuu ya Juliet Kairuki, ni mara mia ya mafanikio yote yaliyopatikana katika kipindi cha Samweli Sitta na Ole Naiko put together!, hivyo huyu mama pamoja na hilo tatizo lake "personal" la mshahara, amekifanyia makubwa Kituo cha Uwekezaji, na kulifanyia makubwa taifa hili Tanzania, kiasi cha kuifanya Tanzania kuwa ndio nchi inayoongoza kwa kuvutia wawekezaji kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kitendo ambacho ni cha kustahili pongezi na kuenziwa na sio kubezwa kama hivi anavyobezwa sasa as if she did nothing!, ila pamoja na makubwa yote na mazuri yote, akifanya makosa yanayostahili adhabu, aadhibiwe tuu kama wengine, ila angalau kwa staha!.
Huu ni uzi kuhusu mafanikio ya TIC iliyoanzishwa mwaka 1997 ni mengi, naomba kutumia item 2 tuu kama performance indicators nazo ni Strategic Investors na FDI.
Strategic Investors.(Wawekezaji Mahiri)
Miradi ya Strategic Investors inapitishwa na kamati ya National Investment Steering Committee,(NISC), inayoongozwa na Waziri Mkuu, wajumbe wa kamati hii ni Waziri wa Fedha, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Ardhi, Mwanasheria Mkuu, Gavana wa Benki Kuu na Mkurugenzi wa TIC ambaye ndiye katibu wa kamati hiyo!. Wakati wote wa kipindi cha Samwel Sita na Ole Naiko kama hii ilikuwa inafanya kikao chake mara moja tuu kwa mwaka. Katika kipindi chote Sitta na Ole Naiko, walipitisha miradi 21 ya wawekezaji mahiri.
Julliet Kairuki baada ya kuichukua TIC, kamati hiyo ya NISC, badala ya vikao kukaa mara moja tuu kwa mwaka, kama hiyo sasa inakaa mara 4 kwa mwaka, na miadi ya uwekezaji mahiri katika miaka 3 tuu ya Juliet, imeshoot toka miradi 21 hadi miradi 43, hili ni ongezeko la zaidi ya asilimia 100%!. Piga hesabu ya miradi 21 katika kipindi cha miaka 1997-2013 (miaka 16) halafu piga hesabu za miradi 22 ndani ya miaka 3!, wajuzi wa hesabu za tija tusaidieni!.
FDI.
Julliet Kairuki alipojiunga TIC, aliikuta inaingiza FDI za dola milioni 500 tuu kwa mwaka, sasa hivi tunapozungumza, TIC inaingiza FDI za dola Bilioni 2 kwa mwaka, ikiwa ni ongezeko la asilimia 400%, ambapo ni Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuvutia uwekezaji kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuliko nchi nyingine zote!.
NB. Simaanishi kuwa Sitta na Ole Naiko hawakufanya kitu pale TIC, bali ninamaanisha Julliet ameichukua TIC iliyokuwa inakwenda kwa mwendo wa kuchechemea, akaimbiza mchaka mchaka, kisha kuiendesha mbio, akaiongezea kasi, hadi sasa hapo ilipo TIC ilikuwa inapaa angani!. Pia simaanishi mafanikio yote ya TIC ni Julliet peke yake, this is a team work na bodi yake, menejment yake, wafanyakazi wake na wadau wake tukiwemo sisi wanahabari wenye jukumu la kuitangaza vyema Tanzania kwenye media, kunakopelekea wawekezaji kuvutiwa kuja kuwekeza Tanzania.
Wiki hii nilialikwa katika kipindi cha 360 cha Clouds TV, kuzungumzia uhuru wa habari Tanzania. Swali la mwisho nililoulizwa niliulizwa nitoe maoni yangu kuhusu utendaji wa Rais Dr. John Pombe Magufuli, nilimpongeza Magufuli, na kuzipongeza hatua za utumbuaji majipu kuwa anafanya kitu sasa katika muda sahihi ila njia anayoitumia kutumbulia haya majipu, sio njia sahihi. (Magufuli is doing the right thing, at the right time but in a wrong way), nadhani kwa vile Magufuli ni rais, no ones tells him, kuwa that is not the right way!. Nikasema kwa vile Magufuli ni rais wetu, Watanzania na dunia wana very high regards on him na very high expectations on him, that he has to be perfect, not only on doing the right thing at the right time, but he got to do it right!. Tanzania inachohitaji sasa sio a populist leader wa kutifanyia one man show, tunahitaji kujenga mifumo imara, ambapo kukijitokeza jipu, halitahitaji bingwa wa one man show kuja kulitumbua, bali the systeam yenyewe inalitumbua pale pale, au linatumbuka lenyewe hata kabla halijaiva kusubii kutumbuliwa!.
Kwa vile maamuzi ya utumbuaji ni maamuzi ya mkuu wa nchi, ambaye ndio the highest authority, no one can challenge the authority, the king is always right hivyo haya kutumbuliwa na tuyaache lets concentrate on her positive side, ndio mada iliyopo mezani.
Kwa vile sisi Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma makala ndefu, hivyo mafanikio ya TIC nayaweka kwenye attachment form, ili yasomwe na wale tuu wenye muda na wenye inteest bila kuwachosha wengine!.
Pamoja na yote haya huyu mama aliyoyafanya, yamemkuta ya kumkuta, wakati sisi tunanyanyapaa kwa mshahara wa milioni 5, sasa subirini wenzetu watakavyo mgombania!, japo hakutendewa vema, lakini you never know, everything happens for a reason, na kuna majanga mengine huwa ni blesing in disguise!.
Nampongeza Julliet Kairuki kwa kazi nzuri TIC, nampa pole kwa yaliyomkuta, hiyo ni ajali kazini, na kosa lake kubwa ni kuwa mkweli na mwaminifu toka ndani ya nafsi yake!, kiukweli mishahara Tanzania ni midogo, Mfano mshahara wa rais tulioelezwa ni TZS 9.5 tax free, laiti Watanzania wangeonyesha expenses zote za kumhudumia rais na familia yake, kila kitu ikiwemo chakula, mavazi na malazi, labda watu wangeweza kumwelewa Julliet kwa nini aligomea mshahara wa TZS 5.M kwa mwezi. Kama tuna viongozi wa taasisi za umma wanaolipwa vizuri na serikali hii hii, why Boss wa TIC anayeliingizia taifa hili FDI ya dola bilioni 2 kwa mwaka?!.
Mungu ambariki.
Paskali.
NB. Nimeweka attachment 3.
1. Document ya mafanikio
2. Video Documentary ya Mafanikio
3. Testimonial ya Jinsi Juliet alivyopatikana na kazi nzuri ambayo Julliet ameifanyia TIC na Tanzania kwa ujumla, kutoka kwa bosi wake wa zamani, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda.