Mafanikio na kuanguka kwa shule mbalimbali za sekondari halmashashauri ya Bunda MjinI

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
400
987
Wasalaam wanajamvi, Mimi ni mdau wa elimu nchini nikiwa ni mzaliwa wa mkoa wa Pwani ila nimekulia Mkoa wa Mara. Kwa kipindi chote nilichokaa Mkoa wa Mara na hasa halmashauri ya Bunda mji nimebaini mambo mbalimbali katika mashule ndani ya halmashauria mbayo yanachangia ufaulu au anguko la mashule husika kama ifuatavyo:

1. ACT BUNDA GIRLS
Ni shule ya private inayomilikiwa na kanisa Anglican Tanzania.Ina wanafunzi wachache sana Kwa idadi ambapo unakuta darasa la mtihani (candidate class)Lina watahiniwa chini ya 50. Maajabu sasa pamoja na kuwa na idadi ndogo zaidi ya watahiniwa utakuta division one za kutafuta na ni nadra kupata one za single digit. Haina tofauti na shule za kata. Division four ni nyingi tu. Changamoto kubwa ya shule ni ukabila ambapo top layer ni wajaluo. Kwa kifupi ni shule ambayo matokeo yake hayana hadhi ya u-private.Wazazi wanapigwa tu pesa zao

2. ELLY'S SECONDARY SCHOOL
Ilikuwa tishio mwanzoni mwa miaka ya 2000,ilikuwa ni shule ambapo karibu Kila mzazi ndani ya mkoa wa Mara alitamani ampeleke mtoto wake shule husika.Na haishangazi kipindi hicho ndicho ilikuwa inaongoza Kwa idadi kubwa ya wanafunzi kuliko shule nyingine ndani ya mkoa zaidi ya wanafunzi 3000. Tuhuma za wizi wa mitihani na mmoja wa wamiliki kujihusisha kimapenzi na mmoja wa walimu kulileta mgogoro wa ndoa ambapo ulichangia anguko la shule mpaka Leo.Tunavyoongea hivi inajitafuta na haifikishi hata idadi ya wanafunzi 200 huku ikiwa chini ya msimamizi mwingine.

3.DR. NCHIMBI SECONDARY SCHOOL
Ilizinduliwa kipindi cha Dr.Emmanuel Nchimbi akiwa (enzi hizo akiwa mkuu wa wilaya BUNDA)Ni shule ya mashindano haswa kwa walimu. Ndio shule yenye walimu wengi wenye magari mengi kuliko shule zote za wilaya husika. Ipo katika kata tata sana ya nyasura. Uimara wa misimamo wa Mkuu wa shule ndugu Mutta umeimarisha taaluma Kwa kuwamudu wazazi vichwa ngumu kwenye vikao.

4. GUTA SECONDARY SCHOOL
NI Shule ya wastani katika matokeo,shida kubwa ni kuwa kando kando ya ziwa ambapo wanafunzi wengi wanaathiriwa na uwepo wa wavuvi ambao huwarubuni Kwa kuwapa pesa na kufanya nao mapenzi.

5. BUNDA HIGH SCHOOL
Ndio shule kubwa katika wilaya iliyoanzishwa mwaka 1990. Ukilinganisha na mashule mengine, shule Ina miundombinu mbinu ya kutosha. Ina bahati pia ya kuwa na wakuu wa shule wazuri wanaounganisha jamii,wazazi na wanafunzi.Ila msingi wa umoja na ushirikiano wa shule husika uliasisiwa na Mr.Machota ambaye baadae alihamishiwa Tarime High school.Mkuu wa shule aliyepo sasa hana makundi hali iliyochochea kufanya vizuri kwenye mitihani ya Taifa.Kidato cha nne wamefanikiwa kupunguza division zero huku pia wakipata division one,two,three nyingi.Division four ni chache.

6. KABASA SECONDARY SCHOOL
Ilianza kama shule mbovu zaidi lakini baadae ikasimama vizuri.Wakati inaendelea vizuri Mkuu wa shule akahamishwa akaletwa mwingine ambaye pia hana ushirikiano mzuri na waalimuwengine.Haina maajabu kwenye matokeo.

7. NUI SECONDARY
Ni shule ya private ambayo ambayo awali ilikuwa tishio sana lakini hii Leo mmiliki wa shule analala ofisini hapo hapo ofisini huku akila wali na maharage na wanafunzi.Mwaka juzi ilikuwa na wanafunzi wawili kidato cha pili.Shule hii awali iliendeshwa kiujanja ujanja tu ambapo mkuu wa shule alikuwa anapita kwenye mashule ya serikali na kurubuni watoto maskini wenye uwezo kitaaluma na kuwapeleka shule yake,hii ilichangia kuinua jina la shule.Ila ujanja wake uliposhtukiwa shule ikafa chaliiii!

8. NYIENDO SECONDARY SCHOOL
Ndio shule maarufu zaidi kuliko zote katika halmashauri ya mji na hata wilaya husika.Ilianzishwa mwaka 2005.Awali ilijulikana kama Chuo cha Mapenzi lakini ujio wa Mkuu mpya wa shule Ndugu Erasto Arende ulibadilisha nidhamu ya wanafunzi na shule ilirudi kwenye mstari ulionyooka.Ndugu Arende ndio founder wa Nyiendo yenye nidhamu. Huyu bwana hakuwa na makundi ya walimu mpaka alipohamishwa 2015. Ujio wa Mkuu mpya ambaye ni mwanamke uliibua makundi ya walimu ambapo kundi la kwanza ni lile la watu wake na kundi jingine ni lile lisilokubaliana nae. Changamoto ya shule ni haya makundi ambapo vikao vinapokaa agenda kupitishwa ni mpaka kundi la mkuu wa shule liaafiki ndipo Inapita.Mbaya zaidi katika vikao husika Mkuu wa shule amekuwa akisifia hadharani walimu kutoka kundi lake kwamba ndio waonafanya vizuri zaidi lake ili kuwadhoofisha wengine.Hali ni mbaya! Mfano mwingine shule ilikubaliana walimu wanaofaulisha mitihani ya Taifa kidato cha pili na cha nne watapewa zawadi binafsi kwa kila mwalimu.Mwalimu mmoja wa somo la kiswahili aitwaye Madam Pendo Edward alifaulisha somo lake kwa karibu asilimia 99 katika mtihani wa CSEE na kwa kuwa siyo kipenzi cha mkuu wa shule,yeye na baadhi ya walimu ambapo pia siyo vipenzi wa Mkuu wa shule waliofaulisha vizuri walitengenezewa mazingira ya kunyimwa zawadi zao.Ghafla utaratibu ukabadilishwa na ikawa walimu waende trip (huku wakijua madam PENDO HATAWEZA KWENDA MAANA ALIKUWA NA MTOTO MCHANGA)Mawazo ya kwenda trip yaliratibiwa vizuri na kundi la mkuu wa shule ili kuwamaliza hao wengine.Na hili lilifanikiwa maana walengwa karibu wote hawakuwepo kwenye trip!Hili limechangia kuvunja morari ya walimu na haitashangaza matokeo ya mwaka huu yakawa mabaya katika historia ya shule tangu kuzaliwa kwake.Kitu kingine walimu wa kike wamekubaliana wasimbugudhi chochote mkuu wa shule ili asije kuwabana kwenye maternity leave zisizo rasmi.Kwa hili pia wamefanikiwa.Hali ni mbaya.Changamoto nyingine ni undumulakuwili wa wazazi.Mara nyingi kwenye vikao wanapitisha maazimio Kwa zaidi ya 90% ila kwenye utekelezaji ni 0000.5%Mfano shule iliazimia wanafunzi wasome masomo ya jioni (Remedial)ambapo iliazimiwa kwenye vikao wazazi wachange chakula Kwa ajili ya Hilo zoezi. Wazazi walikubaliana na azimio hilo ila mpaka sasa wanafunzi waliochanga inasemekana ni chini ya 50 kati ya wanafunzi 1270.Jambo la kuchekesha sasa pamoja na wazazi kugomea kuchanga chakula wanafunzi wanasoma mpaka saa 11:00 jioni hivyo hivyo na njaa.Mwanafunzi asome kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa 11:00 jioni bila kuweka chakula tumboni utegemee ataelewa anachojifunza kweli?Sasa hapo jamani tutegemee maajabu kwenye ufaulu wao?Hapa sasa wazazi wanavizia matokeo yatoke vibaya walaumu uongozi wa shule na walimu wake.

9. OLYMPUS SEC SCHOOL
Ilikuwa moto sana miaka ya 2008-2010 .Haikushangaza mitihani ya kidato cha pili kuwemo ndani ya tatu Bora miaka mitatu mfululizo.Tuhuma za wizi wa mtihani,Dhuluma Kwa walimu na matumizi mabaya ya pesa Kwa watoto wa mwenye shule kuliingiza shule kwenye madeni na Kisha shule ikafa Rasmi.Liwe fundisho Kwa wamiliki wa shule nyingine za mkoa huu.

10. MAHENDE SEC SCHOOL
Licha ya utata kuhusu mmiliki halali ikihusisha pia shule ya Day Star English medium inaendelea kufanya vizuri zaidi.Haina makando kando mengi.

11. RUBANA SEC SCHOOL
Ndio shule yenye mashindano ya kuvaa Kwa walimu wa kike.Shule hii pia inaathiriwa zaidi na siasa za wazazi ambao uwa hawataki watoto wao waadhibiwe.Tukio kubwa la adhabu Kwa watoto lililoleta kasheshe ni lile la 2017 ambapo walimu walipoadhibu watoto waliofeli mtihani wa Mock waliandamana mpaka ofisi ya D.E.O kulaani watoto wao kuchapwa.D.E.O aliyekuwepo enzi hizo aliwasili shuleni na kuwakaripia walimu.Walimu walisusa kuadhibu watoto hali iliyopelekea watoto wawe na utawala binafsi.Hali hii ilipelekea Tena wazazi kurudi kuwalilia walimu kuwa wanaadhibu watoto wanapifanya makosa.Walimu wengi walishikilia msimamo mpaka leo.Ni wachache tu waliorudi kwenye msimamo wa kuadhibu.Hili lilikuwa anguko la shule mpaka Leo.

13. PAUL JONES SEC SCHOOL
Shule ipo karibu kabisa na mbuga ya Serengeti.Inaongozwa na mkuu wa shule mdogo tu kiumri Jonathan Abayo.Kijana Huyu ni bonge la kiongozi Kwani asilimia 98 ya walimu wake ni vijana.Anaishi nao vizuri sana na hakuna migogoro wala makundi.Ni shule changa ila itafika mbali sana kitaaluma!

14. WARIKU SEC SCHOOL
IPO nje kidogo ya mji wa bunda.Muda mwingi wazazi hushiriki migogoro ya kugombea ardhi na migogoro ya wakulima na wafugaji.Ushirikiano wa wazazi na shule ni mdogo sana.Haina matokeo mazuri ipo ipotu!

15. SIZAKI SEC SCHOOL
Umaarufu wa shule hii tofauti na shule nyingine ni umahiri wa matukio ya kishirikina yaliyowahi kuitikisa shule na japo yamepungua Kwa kiasi.Miaka ya nyuma wanafunzi wa kike waliokuwa hostel walikuwa wakiingiliwa kimwili kishirikina hali iliyopelekea kudumaa Kwa maendeleo ya kitaaluma shuleni hapo.Mwaka 2016 yalitokea mapigano makali kwenye kikao cha kutambua washirikina waliokuwa wanasumbua shuleni hapo ambapo watu walicharangana mapanga.Ukifika sizaki kata ya mcharo utapewa mkanda mzima kuhusu ushirikina uliotikisa shuleni hapo hali iliyopelekea watoto wengi kuhamishwa shule.

Hitimisho:1 Wakuu wa shule acheni makundi mnapowagawa walimu mnaua taaluma.Umoja ni nguvu,utengano ni udhaifu!

2: Walimu timizeni wajibu ndipo mdai haki zenu!

3: Wazazi mna nafasi ya kukuza taaluma ila kinyume chake mnaua taaluma zaidi mashuleni hebu badilikeni!

Mwisho kabisa Afisa elimu Sekondari Bunda mji karudisha Imani Kwa wadau wa elimu hapo halmashauri. Anaongea na walimu Kwa staha,hajikwezi na ni mtu wa watu.Ni kiongozi na siyo mtawala walimu mtumieni mtatue changamoto zenu!

Mjumbe hauwawi!
 
Point yako ilikua ni kutoa umbea wa NYIENDO, Pia mbona hujaitaja Sazira, Kunzugu?.
Et walimu kushindana kuvaa, magari. Yani watu wakipendeza mnaona wanashindana.
 
Back
Top Bottom