Maelfu wawasili jijini Mwanza kushuhudia uteuzi Katibu Mkuu CHADEMA

NA mmiliki wa chadema Lowassa anawasili lini
Acha kujivua ufahamu.... Lowassa ni mwanachama wa chadema na ataendelea kuwasumbua vichwa nyie kunguni wa Lumumba....

Lowassa amesababisha Magufuli leo anafanya kazi kwa Ilani na Sera za Ukawa!

Lowassa ni habari nyingine wewe!
 
Sisi na Magufuri wetu anaendelea kutumbua majipu , Kyadema na na nyumbu zake wnaendelea na mafuriko eeeeh ?
 
Duh....yaani maelfu ya watu kutoka mikoani waje kufuatilia tu uteuzi wa katibu mkuu mpya?Haya bhana!!!??
Hakika ni historia.Hilo ndilo tunaloweza kusema kwa sasa kutokana na hekaheka zinazoendelea hapa jijini Mwanza.

Umati wa wafuasi,wapenzi na wanachama wa Chadema umekuwa ukifurika hapa jijini tangu jana wakitokea mikoa mbalimbali kwa lengo la kushuhudia utangazwaji wa Katibu Mkuu mpya anayetarajiwa kukiongoza chama hicho chenye ufuasi mkubwa nchini.

Baadhi ya wafuasi waliotokea Ruvuma walisema wamekuja hapa kuonyesha mapenzi waliyo nayo kwa chama chao.

Mitaa mbalimbali ya hapa Mwanza kwa sasa imepambwa kwa bendera za Chadema huku magari mengi ya watu binafsi na ya kubebea abiria na bodaboda zikiwa zinapeperusha bendera za Chadema.

Kwa hakika Katibu Mkuu atakayechaguliwa kesho ataingia kwenye vitabu vya historia kwa jinsi kulivyo na mhemko wa umma juu ya upatikanaji wake.

Ratiba inaonyesha mara baada ya kuchaguliwa kesho usiku atatambulishwa Jumapili kwenye viwanja vya Furahisha,mkutano unaotarajiwa kuvunja rekodi ya mahudhurio.

Vikosi vya ulinzi vya Chadema vya Red brigade pamoja na polisi wametanda maeneo vinapofanyika vikao vya Kamati Kuu na baadaye Baraza Kuu kwa lengo la kuimarisha ulinzi.

Hakika hii ni zaidi ya kumpata Katibu Mkuu.Katibu Mkuu atakayeweka historia mpya.
 
Back
Top Bottom