Madhara ya kumsaidia mwanamke kazi za ndani

Coke Zero

JF-Expert Member
Mar 30, 2015
1,024
542
Wadau,

Kuna jamaa yangu analalamika kwamba analazishwa kazi za ndani na mke wake.
Ishu iko hivi, Jamaa anapenda sana kumsaidia sana mkewe kazi za ndani kama kufua kupika, kuogesha watoto, kufanya usafi nk kwa siku ambazo anakuwa yuko free.

Sasa tatizo ni kwamba mwanamke amefanya hayo ni majukumu ya jamaa kiasi kwamba kwa mfano mwanamke akichelewa kurudi kazini siku ambazo mshkaji anakuwa yeye amewahi na kukuta jamaa hajafanya kazi yeyote mwanamke anamgombeza jamaa au ananuna kabisa na hazifanyi hizo kazi mpaka jamaa yeye afanye.

Je wadau hii ni sawa.?
 
Ndio tatizo lao unafanya kwa nia njema kabisa lakini anageuza ni jukumu lako ndio maana wanaume wengi hawafanyi hizo kazi totally hata kama anaziweza,ila huu unaoitwa upendo wa kusaidiana unauta mume na mke wanashikana shikana jikoni wote mnaonekana sawa.
Lingekuwa jambo jema kwa ke wangeelewa kwamba anasaidiwa na si kuleta mazoea.
 
aaaaaaisee hii imeanza kunikuta na mimi ss hiv akiwa bize na mm niko free nisipo pika au chota maji au kufua anagomba nabak namshangaa tyu nmemzoesha vibaya na sasa ni mjamzito imekua km ni lazma nifanye najua bcz ni prgnant kumbe hata kawaida wapo hata kumuoa bd shaur yake
 
Shost yangu mmoja mume wake alikuwa anafua nguo zote za nyumba J'mosi lakini kuanika tu nje alikuwa anamwambia kuepuka longo longo za shilawadu aanike mke.
 
Kuwa makini itakula kwako.
 
Ni Vizuri Mwanaume Usitoe Nafasi Kwa Mkeo/Mpenzi Kuzoea Tabia Flani, Always Be Undifined Maana Akili Yao Ikizoea Kufanyiwa Kitu Flani Basi Huweka Matarajio Ya Kufanyiwa Siku Zote. Ni Kama Mtoto Ukimzoesha Kumletea Pipi Kila Utokapo Kazini, Siku Usipokuja Nayo Hatoelewa Wala Kufikiria Kwanini Hujamletea Bali Atahisi Humpendi Na Hujamtendea Haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…