Madhara ya kufanya tendo la ndoa hovyo hovyo!

mchungaji7

Senior Member
Feb 2, 2017
187
396
Wana MMU habari za majukumu?

Leo naomba tuangalie madhara ya kufanya tendo la ndoa hovyo hovyo, nikisema hovyo hovyo nina maana ile tabia ya kutaka kuzini na kila mwanamke au mwanaume unayemtamani.

Kufanya tendo la ndoa na kila mwanamke au mwanaume kuna madhara mengi sana,Leo ntataja machache.

1. Hushusha heshima ya mtu husika.
Kufanya tendo la ndoa hovyo hovyo huitwa zinaa, zinaa husababisha mfanyaji aonekane ni mtu asiheshimika wala kuaminiwa na jamii.

2.Huharibu mahusiano kati ya mtu husika na Mungu.

3. Humuweka muhusika mbali na Mungu

4. Hujenga mazoea ya kutotulia na mwanamke au mwanaume mmoja hata baada ya kuoa au kuolewa.

5. Hupelekea kupata magonjwa ya zinaa kama vile ukimwi,gono , kaswende na kadharika.

6. Hupelekea mwili kuchoka na kuzeeka haraka.

Hayo ni baadhi tu ya madhara ya zinaa.

Geuka acha zinaa , mrudie Mungu wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…