Madawa ya Kulevya: Waziri wa Katiba na Sheria aomba Shikuba akashtakiwe Marekani!

Wayapeleke kule GWANTANAMO wakayasagesage kabisa maana wamefanya wabongo wengi kuwa machizi
 
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amewasilisha maombi mahakamani akitaka watanzania watatu akiwemo Ally Hajji maarufu Shikuba wapelekwe nchini Marekani kujibu mashtaka ya kufanya biashara ya dawa za kulevya.

Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki aliwasilisha maombi hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Kakolaki aliwataja washtakiwa katika maombi hayo kuwa ni Ally Haji maarufu Chikuba, Iddy Mfuru na Tiko Adam.

Wakili huyo aliomba kuwasilisha ushahidi na vielelezo kisha mahakama itoe uamuzi na amri kwa washtakiwa kusafirishwa.

Hata hivyo ushahidi huo haukuweza kusikilizwa kwa sababu Wakili Majura Magafu, Hudson Ndusyepo na Adinan Chitale kuomba muda wa kuupitia kabla haujasomwa mahakamani.

Hakimu Mkeha alikubali kuwapa muda mpaka kesho asubuhi kwa ajili ya mahakama kusikiliza ushahidi huo, alimuru washtakiwa kurudi rumande.


Chanzo: Mtanzania

HIVI NANI ANAOMBA ? SISI AU MAREKANI ?
KAMA US HAWAJA WASILISHA HATI YA EXTRDITION...HAWATAKI MIZIGO..HASA HUYU TRUMP
 
Mkuu kuna tangazo la kutafutwa Shikuba na serikali ya marekani. Kuna bandiko limo humu na pia taarifa zipo ktk tovuti za serikali ya Marekani(USA). Nadhani mwanasheria wa serikali anapitia taratibu zinazotakiwa ili raia wa Tanzania akabidhiwe na nchi nyingine kwenda kujibu mashitaka yake.

Mkuu hilo tangazo halina tafauti na "Fake news " za Trump kumsifia Magufuli, ni habari za kutengenezwa,Hakuna asiejua shinikizo la Marekani kama inataka lake,Kama kweli serikali ya Marekani inamtaka huyo jamaa basi amini huyo jamaa angelikuwa ameshapelekwa Marekani..

Kuna habari zimeenea katika mitandao kuwa Tanzania itaingia bila ya viza Marekani,habari ambazo zimeandikwa na foxsnews,fake news ambazo zinatengenezwa na moja katika kikundi cha usalama wa taifa

Marekani haimtaki Shkuba,isipokuwa serikali haina kesi sasa inatapatapa,,,tusibiri tuone hii movie staring atakufa vipi
 
Wee pongo kibuduu utakua muuza unga lazma ndio maana unaongea pumba hapa au umetumwa kuleta kuwatetea mabwana zako, huna haya kutetea wezi kweli au laana inakuhangaisha...kweli Nyumbu nyumbu tu
Ni tabia ya watanzania kama hawana hoja wanakuwa wanatukana,watanzania kama nyinyi ndio mnaiaibisha hii nchi,unajibu bila kufikiri,unafuata upepo,huna mawazo yako,sasa ndio umeongea nini hapa,,toa na wewe msimamo wako,toa sababu zako kwanini huyu jamaa apelekwe Marekani,kwanini wamarekani wanamtaka nk,sio matusi,,,,
 
Majipu mapya haya, wazee wa kukurupuka. Madaraka ya kulevya teyari watu wameshakua mateja wa madaraka ya kulevya
 
bora hata umeeaeleza wehu wanaopinga kila jambo kwa sababu tu wana njaa
Kama nchi imefikia hapo ambapo mtu mmoja anaweza kuhonga mahakimu wote basi hatuna taasisi ya mahakama. Na unamaanisha wote waofingwa ni kwasababu hawana hela... hii ni sawa na kuikashifu idara yetu ya mahakama. Kama hamjajua sababu ni bora mkaitafuta mkajua nikwanini wameomba apelekwe marekani na sio kuongea propaganda za kuidhalilisha mahakama ya Tanzania.
Mahakimu na majaji wetu njaa sana anaweza kuachiwa tu, hii biashara imetamalaki na imemeza vyombo vingi
 
Anaenda kuchomokea unyamwezini. ......deal done.
Tanzania ndiyo anachomoka .....ila marekani hatoki.....ulizia smbdy beka ranger ndg yake madega bongo walimlinda wazungu wakamvuA huku mpaka leo kimyaaaa......
Shkuba amefanyiwa mpango sana achomoke hapa tz maana ana uhusiano na kigogo mmja mstaafu na bado anafanya njia atoke..
Kwa nje shkuba kesi yake ndiyo iko vibaya sana na anajuaa akienda huko harudi tenaaa

Ova
 
Waziri anaomba raia akasgitakiwe nchi nyingine... Haitakaa itokee duniani waziri wa marekani aombe raia wake ashtakiwe nchi nyingine
 
Yani kumshtaki Raia wenu mmeshindwa mpaka mumpeleke marekani? Chapo alipelekwa america sababu alingiza dawa za kulevya Tani nyingi mno...sasa huyo shkuba hajafkia hata Tani 2 jamni kwel mnashindwa kuendesha nchi na sheria? kama mna ushahidi why mshindwe kumhukumu hapa??? So ina maansha Mahakama za Tanzania hazina meno
Mkuu kukaa kimya pia ni busara, umeonyesha jinsi ulivyo mweupe kichwani
 
Tanzania na michezo ya kuigiza,Nimeisoma hii habari kwa muono wangu,Wakili wa serikali anacheza mchezo wa kuigiza kama waliovyowachezewa akina Lema na watu wengine, Mawakili wa serikali waanainajissi sheria za Tanzania.

Huyu jamaa sio mkubwa hivyo katika madawa ya kulevya kama anavyotanganziwa na Media za Tanzania,Huyu jamaa kweli alikuwa anauza madawa ya kulevya lakini hana sifa kama anazopewa

Hii kesi ya huyu jamaa kwa ufupi wakili wa serikali imemshinda!!!,kama kawaida yao polisi walikurupuka kumkamata huyu jamaa,polisi hawana ushahidi wa kutosha kwa huyu jamaa na ndio maana hii kesi ina miaka mingi bila ya kutolewa hukumu

Anachofanya wakili wa serikali ni kupoteza muda tu,ili huyu jamaa azidi kusota mahabusu,swali muhimu la kujiuliza kwani marekani wameomba huyu jamaa apelekwe huko? inavyojulikana kama nchi ya Marekani inamuhitajia mtu, wao ndio wanaomba kuwa huyo mtu wanamtaka apelekwe akashitakiwe Marekani,lakini kwa kesi hii naona imekwenda kinyume yaani ni Wakili wa serikali anaomba wamerekani wamchukue huyu jamaa,sasa wamarekani watamshitaki huyu jamaa kwa kesi gani

Kwa ufupi nchi ya Marekani hakuna muuza unga wa Heroine aliepelekwa huko,wauza dawa za kulevya wanaoshitakiwa marekani wote ni wale wanaouza Cocaine.

Watanzania ni wazuri wa kutoa maamuzi bila ya kufikiri au kutafuta ukweli uko wapi,mpaka sasa tunachosikia ni habari ya upande mmoja tu,upande wa wakili wa serikali na propaganda zake,bado hatujasikia upande wa mshtakiwa,Wakili wa Shkuba nae angelitumia mbinu wanazotumia wakili wa serikali atumie Media kumtangaza mteja wake ili watanzania nao wasikia upande mwengine wa hii stori

Kwa ufupi msilete movie isiokuwa na maudhui kama mmeshindwa kumshtaki ama mahakama imeshindwa kutoa hukumu mwacheni kama ana kosa mshitakini,sheria lazima zifuatwe sio visasi na mihemko
Wamshtaki kwa ushahidi gani,mi nmeshangaa sana eti wanataka wampeleke marekani kwan wamerekani wameleta extradition request kwetu.pia ni kweli ulivyosema shkuba sio big fish kiivyo kama wanavyotuaminisha
 
Tanzania ndiyo anachomoka .....ila marekani hatoki.....ulizia smbdy beka ranger ndg yake madega bongo walimlinda wazungu wakamvuA huku mpaka leo kimyaaaa......
Shkuba amefanyiwa mpango sana achomoke hapa tz maana ana uhusiano na kigogo mmja mstaafu na bado anafanya njia atoke..
Kwa nje shkuba kesi yake ndiyo iko vibaya sana na anajuaa akienda huko harudi tenaaa

Ova
Mkwere au ???

Noma
 
Hapo huyo WAZIRI KISHAPEWA CHAKE...maana hapa kwetu KIFUNGO CHA MADAWA NI MAISHA,,,kule MAREKANI kifungo ni MIAKA 2.....PUMBAVU ZAKE....wenye AKILI NYINGI tumewashtukia,,,,kwnz hapa SHERIA YA MADAWA NI NGUMU MNO KUCHOMOKA,,wanaona WAKAMCHOMOE MAREKANI....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom