Madawa ya kulevya; Serikali kama ina nia ya dhati kutokomeza ianzie hapa kwa sasa!!

kuacha ngada uamue mwenyewe na sio mtu akuamlie, kwan uyo chid hajapelekwa kwenye ivyo vituo? sasa mnataka asaidiweje? kapelekwa bagamoyo katoroka, apa dar anatoroka sasa mnataka asaidiwe vp? na kwa nn iwe chid tu kwan chid yeye ndio nan? sisi sote ni wa tz na hii inch sio ya flan sasa ifikie hatua tuache ubinafs, wapo waathirika wengi tu, tunao uku mtaan ivyo mpaze sauti kwa wote na sio chid pekee ila mm saut yangu sipaz kwa wavuta unga ambao mm naamin kuwa ile ni starehe yao, bali mm napaza sauti kwenye vipaumbele vingine ila hao wajinga mm sina shirika nao
 
hahhah hii serikali ni kali usitegemee tejA asaidiwe labda kwa kuwasaidia tu wasiteseke tumwazime duterte kwa mwezi 1 tuone!
 
hao watumiaji kwa kweli serikali ilitakiwa iwakamate na iwaweke kabisa ndan, kwa mtu yeyote anayewajua hawa watumiaji wa unga nadhan angeunga mkono hoja yangu kwa 100%, sababu asilimia kubwa japo sio wote ila zaidi ya 70% ya wavuta unga ( mateja ) ni wezi wa mifukoni, wakabaji, wapigaji watu mapanga hasa kwa kipindi kile wanapokuwa alosto (alosto kwa mtu asiyejua ni ile hali anayokuwa nayo mteja pindi anapokosa unga) yaan ukimkuta mteja yuko kwenye alost!! anaweza akafanya tukio ambalo sio la kawaida bila kujal mazingira yakoje nikimaanisha anaweza akakukaba mbele za watu mchana kweupeeee, au anaweza akakupiga mapanga, sasa jaman mtu wa namna iyo kuna haja gan ya kumjadili kwa mazur????
 
nimeona Instagram,waziri Mwigulu kaenda nyumbani kwa mzazi wa chid benz,nimeona tuzo za chid Enzi zake kwenye mziki,imeniuma sana.......

I hope Mwigulu atamsaidia kama hakwenda kumuona just for show off.....
 
Kwa kuwa serikali imekuwa ikitangazia umma kuwa inapambana na madawa ya kulevya kwa juhudi zote, sasa ionyeshe umma kuwa haijashindwa chochote kwenye hili suala!
Kwanza kuna huyu anayeitwa Chid Benz sijui ni kwa nini hadi hivi sasa serikali imekaa kimya kuhusu hili suala lake, imeshathibitika kwamba huyu mtu ni drug abuser, ameshaathirika sana na madawa ya kulevya, hivi ni kwa nini serikali haitaki kumsaidia kama ina nia ya dhati kabisa ya kupambana na madawa ya kulevya..
Anaachwa tu aendelee kutumia aangamie..?
Ni vijana wangapi kama huyu Chid wapo katika hali aliyonayo huyu Chid benz..?
Binafsi huwa nakutana na vijana wengi mno ambao wapo kwenye hali mbaya sana ambao wameshakuwa addicted!
Sasa kama haijulikani hao wauzaji wanapatikana wapi mbona njia ya kuwapata ni rahisi sana..
Hawa vijana ambao ni addicted wakamatwe au wapelekewe wapelelezi wanaweza kujifanya wao ni watumiaji wakadeal na hawa addicted mwisho wa siku ikajulikana wanakoyapata na hatimaye huo mtandao kunaswa!
Au ni kwamba wapo vigogo wa serikali waliopo kwenye huu mtandao wa kuuza madawa ya kulevya??
Huyu chid ataangamia tukiwa tunamuona na wala haitasaidia chochote kama hatu stahiki zisipochukuliwa mapema, achukuliwe asaidie huko anakoyapata ili tuokoe vijana wengine!!
Wakichukuliwa vijana kadhaa ambao ni addicted wakataja huo mtandandao itasaidia sana kuokoa kizazi hiki, kuwapeleka sorber haitasaidia sana, kikubwa tudeal na ile source wapi wanayapata!
Nawasilisha...
Tunashukuru kwa ushauri wako na Huruma yako kwa vijana wanaotumia madawa ya kulevya.

Hii vita si rahisi sana kama unavyofikiri kuwa unamkamata mtumiaji anakupeleka kwa muuzaji halafu unavunja mtandao wa wauzaji si rahisi kama haya maneno ulivyoandika.Na kama ungekuwa hivyo basi nchi kama Marekani yenye majeshi imara biashara hii ingekuwa historia.

Mabadiliko ya kwanza kabisa kwa mtu ambaye ni addicted yanaanza na yeye mwenyewe.Ndipo wengine wataweza kumsaidia kutumia mabadiliko hayo bila hivyo ni sawa sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Serikali nyingi dunia zimeweka sheria Kali na adhabu Kali hadi kunyongwa lakini bado binadamu kila kukicha ndo kwanza anafikiria hii biashara.

Na kumbuka Tanzania hakuna soko la madawa ya kulevya ila ni njia ya kupita kwenda mataifa mengine kwa kujibu ya taarifa za UN.kitengo cha kudhibiti biashara ya madawa.
 
sio kweli mtu akiwa ameathirika na madawa ya kulevya,then kuacha ni maamuzi yake mwenyewe,ukiingia huko huelewi kinachoendelea unless watu wako wa karibu wahangaike na wewe mpaka upone.
 
kwan chid ndio mteja wa kwanza nchi hii ....?
Rudia kusoma uelewe, Chid ni kama sample!
Wapo vijana wengi walio kama Chid, hawa ndio ninaowazungumzia, wataweza kutoa dira kwenye hili!
Tusiishie kuwalaumu hawa vijana kwamba wanatumia basi shauri zao unless basi kama tuambiwe yamehalalishwa..
 
freyzem! hoja yako haina mashiko ndugu yangu, hv kwa mtazamo wako vijana walioathirika na madawa nchi hii wako wangapi? napinga kauli yako kwa 100%, we unaacha kuishaur serikal itatue kero na changamoto mbali mbali muhim zinazowakabili wananchi wake, eti unashaur iwaangalie wa akina chid, kwan chid yeye nan? umejishusha sana ndugu yangu, hv ww mvuta unga unamjua vzr? mvuta unga si bwege tu, kwan kuna mtu alimtuma akavute? ww mbona huvut si kwa sababu unayajua madhara yake? kwa iyo mi naishaur serikali isihangaike kabisa na hao wajinga sababu ni maisha waliojichagulia ayo, kama ni nguvu kazi wapo vijana kibao tu mtaan ambao hawajaathirika na ayo madawa
Huo ni mtazamo wako kuona kuwa hoja yangu haina mashiko, lakini ukweli utabaki kuwa kwamba hawa vijana wanaangamia si kwa uzembe wao tu bali taifa limeshindwa kupambana na hii kitu.
Waathirika ni wengi na kama ni wengi hatuwezi kuendelea kupoteza nguvu kazi hii wakati ni jambo tunaweza liwekea mikakati na kulitungia sheria kali tukalitatua!
Kuhusu kuwakamata hawa vijana hii itatoa njia zaidi wapi wanapoyapata iwe vichochoroni au wapi!
Vibaka na wahalifu wengine wengi wao ni addicted wa haya makitu,
Unless basi iwe serikali ina maslahi na hawa wauzaji ndio maana imeshindwa kupambana na haya madawa..
 
kama hujui vzr, mvuta unga hata umsaidie vp , hawez akaacha kuvuta ndugu yangu, na kama unakumbuka vzr rais wa awamu iliyopita alifanya juhud za makusud kumsaidia yule dada mwanamuziz ray . lakin umeona kilichotokea?
Unayoyasema ni kweli, lakini mbadala wake upo!
Hivi mfano wangedeal na yule dada wakambana awaambie anakoyapata, si ingesaidia kumegua huo mtandao kwa kiasi flani kama walikuwa na nia ya dhati ya kumsaidia?
Muhimbili mateja wapo kibao wanaotibiwa pale na wanapona hawarudii tena hayo madawa, lakini tatizo mzizi ndio inakuwa shida kuung'oa...
 
Kwa jinsi nilivyomuelewa mtoa mada hajamaanisha hela ya serikali itumike kwa wala Unga, bali hao vijana walioathirika watumike kuwabaini wauzaji vivyovivyo back wise hadi kuwapata importers. Na kwa kuongezea wakishabainika na kuthibitishwa wafanyiwe kile anachofanya Rais wa Philippines ndugu Rodrigo Dutetre. Kusema serikali isihangaike nao kuwa ni maisha waliojichagulia sio sahihi, leo ni kwa Chidi Benz kesho akinasa ndugu yako wakaribu utaona umuhimu wa serikali kulivalia njuga suala la drugs.
 
freyzem! hoja yako haina mashiko ndugu yangu, hv kwa mtazamo wako vijana walioathirika na madawa nchi hii wako wangapi? napinga kauli yako kwa 100%, we unaacha kuishaur serikal itatue kero na changamoto mbali mbali muhim zinazowakabili wananchi wake, eti unashaur iwaangalie wa akina chid, kwan chid yeye nan? umejishusha sana ndugu yangu, hv ww mvuta unga unamjua vzr? mvuta unga si bwege tu, kwan kuna mtu alimtuma akavute? ww mbona huvut si kwa sababu unayajua madhara yake? kwa iyo mi naishaur serikali isihangaike kabisa na hao wajinga sababu ni maisha waliojichagulia ayo, kama ni nguvu kazi wapo vijana kibao tu mtaan ambao hawajaathirika na ayo madawa
Madawa ya kulevya nayo ni changamoto Mzee ,usijifanye umeshikiwa maiki
 
Mkuu moja kati ya biashara mbaya na yenye mizizi mikubwa na ushawishi mkubwa hapa duniani.....ni hii ya madawa yanayoitwa ya kulevya........

Ni biashara ambayo inafanyika hata katika nchi ambazo wewe unaweza kuona ulinzi uko juu.....

Ni biashara inayohusisha watu walioshika mihimiri yote ya kiuchumi ya ulimwengu huu......fedha chafu zinazotokana na biashara hii....ndizo zinazotakatishwa na kuendesha shughuli mbali mbali za kiuchumi.......

Ni kama sigara ambayo ni hatari kwa maisha ya mwanadamu....lakini pato lake haramu....ni muhimu kiuchumi......

Jukumu lako ni wewe kuwa balozi kwa wale wapendwa wako....wasijihusishe na ushetani huu.....
Umenena vyema
 
Back
Top Bottom