Madaraja Makubwa ambayo Tanzania Inajigamba nayo Yalishajengwa na Nchi mbalimbali mfano ni Uganda

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
58,784
69,441
Tanzania tumekuwa tunajiainisha sana kwenye mitandao Kwa kuweka picha mbalimbali za miundombinu mfano madaraja Makubwa na flaiova huku tukibeza Nchi zingine bila kujua kinachoendelea huko.

Ukiangalia makelele yanayopigwa baada ya kukamilika Kwa daraja la JPM Kigongo Busisi,Tanzania,Wami nk unaweza dhani Tanzania ndio Nchi ya kwanza hapa Afrika kufanya hivyo.

Hivyo hivyo kwenye flaiova.Kwa Taarifa yenu tuu Uganda hapo ilishajenga daraja kama la Kigongo -Busisi miaka 5 iliyopita na madaraka mengine makubwa mengi tuu.

Hivyo hivyo kwenye flaiova,huko ndio tuko nyuma mboo kiasi kwamba tukioata hata kamoja tusiwe na makelele sana maana tunajiabisha na kuonesha jinsi gani tuna akili finyu.

Tulitakiwa kujigamba kama tumejenga daraja kutoka Bagamoyo-Zanzibar au Pangani-Pemba nk

Jinja bridge 👇👇

View: https://youtu.be/-aHr89ANq_E?si=bbfEFbAp3hREwCW5

My Take
Ni vyema tusafiri Nje ya Nchi kupata exposures na nini kimefanyika au nini kinafanyika .

Sio vibaya kufurahia na kushangilia ila sio sawa kujigamba na kukejeli wengine wakati uhalisia tunaoneoana hamnazo.

View: https://youtu.be/wFqb-VY0H10?si=rktF8SDrFDfYpnJc
 
Wanajua wabongo hatusafiri ndio maana wanatuaminisha kua wao ndio wa kwanza Afrika mashariki na kati kufanya hivyo.
Hata You tube tuu inashindikana kuangalia?

Juzi mwingine kamsena eti PET Scan Kwa EAC ipo Tzn pekee wengine hawana na kama ipo Iko private sector wakati ni uongo.

Siasa za kijinga na upotoshaji tuache.
 
tunajiabisha na kuonesha jinsi gani tuna akili finyu.

Tuwasamehe maana lugha ya kigeni inawapiga chenga sana sisi waTanzania kiasi pamoja ya kuwa kuna chaneli nyingi za habari kwa lugha ya English, magazeti, majarida, online TV, Online Radio, YouTube n.k lakini ndiyo hivyo tunapitwa sana na habari kemkem za yanayoendelea duniani hata hapa jirani Zambia, Malawi, Zimbabwe, Uganda, Kenya n.k kutokana na lugha.
 
Back
Top Bottom