Madai ya Wanafunzi kusomea chini ya mti Shule ya Msingi Kwembe (Dar), Serikali yasema walikuwa katika programu maalumu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,583
13,270
GSLrDiIXkAE4YfS.jpeg

KUKANUSHA TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MWANDISHI DICKSON NG'HILY NA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO

Kumekuwa na taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kumkamata mwandishi wa habari ambaye pia ni Mhariri wa biashara na Mkuu wa Kitengo cha Mtandaoni (digital) Ndugu Dickson Ng'hily kutoka Gazeti la The Guardian.

Taarifa hiyo imeeleza pia mwandishi huyo alipigwa sana na kuumizwa kwenye mkono na simu yake kuvunjiwa kioo huku sababu ikielezwa kuwa ni kupiga picha wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwembe waliokuwa wanasoma chini ya mti. Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa mwandishi huyo alipelekwa ofisi ya Serikali ya Mtaa na baadaye kushikiliwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo anapenda kukanusha taarifa hiyo iliyoleta tahahuruki kwa wananchi na waandishi wa habari. Ukweli ni kwamba mwandishi huyo hakupigwa na mtu yeyote isipokuwa aliulizwa na Mwalimu Mkuu kwa nini anapiga picha bila ridhaa yao wala kujitambulisha.

Baada ya mwandishi huyo kukataa kutoa ushirikiano alipelekwa Ofisi ya Serikali ya Mtaa na baadaye akapelekwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kujiridhisha kama kweli ni mwandishi na ana kibali cha kufanya kazi hiyo.

Hata hivyo leo Julai 10, 2024, Mhe. Mkuu wa Wilaya alikuwa kwenye ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mburahati na hivyo hakuhusika wala kutoa amri yoyote kuhusu kukamatwa kwa mwandishi huyo.

Aidha, ni kweli kuwa wanafunzi walikuwa nje ya madarasa yao kwa ajili ya programu maalumu ya kufanya masahihisho ya mtihani wa Utamilifu (mock) Mkoa, hivyo kimsingi shule haina wanafunzi wanaosomea nje kwa kukosa madarasa.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inathamini na kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari katika kufanikisha kazi yao muhimu ya kuhabarisha Umma juu ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Hata hivyo, ni muhimu Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo katika kutimiza haki yao ya kutafuta, kuchakata na kusambaza habari.

Joina Nzali
KAIMU MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

Taarifa za nyuma kuhusu tukio hili soma bofya hapa:
~ THRDC yakemea Mwandishi wa Habari kukamatwa kwa kupiga picha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwembe wakisoma chini ya mti

~ Mwandishi wa Habari wa The Guardian anadai amepigwa na Walimu baada ya kupiga picha Wanafunzi wakisoma chini ya miti
 
Kwani yeye mwandishi anasemaje, leta na picha na maongezi ya mwandishi Ili tupate taarifa kutoka pande zote Ili tujue kama kapigwa au ajapigwa, hatuwezi kusikilizia upande mmoja na tukaona sawa tu
 
Kasome hapa ndugu

Aidha, ni kweli kuwa wanafunzi walikuwa nje ya madarasa yao kwa ajili ya programu maalumu ya kufanya masahihisho ya mtihani wa Utamilifu (mock) Mkoa, hivyo kimsingi shule haina wanafunzi wanaosomea nje kwa kukosa madarasa.
Idadi ya waliofanya mtihani ni ileile idadi ya wanaofanya masahihisho, kwa nn wasifanyie kwenye darasa walilofanyia mtihani?
 
Darasa la kwanza wanafanya mtihani wa Utamilifu (mock) Mkoa, hivyo kimsingi shule haina wanafunzi wanaosomea nje kwa kukosa madarasa.

Kwembe hapo mjini kabisa aise,

Ila pia ule ni ubunifu, kutoka nyumbani na majivu kuyafanya ubao ni ubunifu.

Mengine rekebisheni tu kimya kimya, barua za nini?
 
KUKANUSHA TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MWANDISHI DICKSON NG'HILY NA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO

Kumekuwa na taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kumkamata mwandishi wa habari ambaye pia ni Mhariri wa biashara na Mkuu wa Kitengo cha Mtandaoni (digital) Ndugu Dickson Ng'hily kutoka Gazeti la The Guardian.

Taarifa hiyo imeeleza pia mwandishi huyo alipigwa sana na kuumizwa kwenye mkono na simu yake kuvunjiwa kioo huku sababu ikielezwa kuwa ni kupiga picha wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwembe waliokuwa wanasoma chini ya mti. Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa mwandishi huyo alipelekwa ofisi ya Serikali ya Mtaa na baadaye kushikiliwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo anapenda kukanusha taarifa hiyo iliyoleta tahahuruki kwa wananchi na waandishi wa habari. Ukweli ni kwamba mwandishi huyo hakupigwa na mtu yeyote isipokuwa aliulizwa na Mwalimu Mkuu kwa nini anapiga picha bila ridhaa yao wala kujitambulisha.

Baada ya mwandishi huyo kukataa kutoa ushirikiano alipelekwa Ofisi ya Serikali ya Mtaa na baadaye akapelekwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kujiridhisha kama kweli ni mwandishi na ana kibali cha kufanya kazi hiyo.

Hata hivyo leo Julai 10, 2024, Mhe. Mkuu wa Wilaya alikuwa kwenye ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mburahati na hivyo hakuhusika wala kutoa amri yoyote kuhusu kukamatwa kwa mwandishi huyo.

Aidha, ni kweli kuwa wanafunzi walikuwa nje ya madarasa yao kwa ajili ya programu maalumu ya kufanya masahihisho ya mtihani wa Utamilifu (mock) Mkoa, hivyo kimsingi shule haina wanafunzi wanaosomea nje kwa kukosa madarasa.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inathamini na kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari katika kufanikisha kazi yao muhimu ya kuhabarisha Umma juu ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Hata hivyo, ni muhimu Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo katika kutimiza haki yao ya kutafuta, kuchakata na kusambaza habari.

Joina Nzali
KAIMU MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

Taarifa za nyuma kuhusu tukio hili soma bofya hapa:
~ THRDC yakemea Mwandishi wa Habari kukamatwa kwa kupiga picha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwembe wakisoma chini ya mti

~ Mwandishi wa Habari wa The Guardian anadai amepigwa na Walimu baada ya kupiga picha Wanafunzi wakisoma chini ya miti
Mhu! Habari za Mkuu wa Wilaya akanushe mkurugezi wa Halmashauri ya Manispaa!
 
Una akili kidogo sana ,madarasa A,B,C,D wakae chumba kimoja

USSR

Wewe utakuwa punguani kabisa.

Ufahamu kuwa, hata leo hii ukianzisha shule, kigezo kimojawapo muhimu ili upate kibali, pamoja na kuwa na madarasa, ni lazima shule iwe na ukumbi. Lengo mojawapo la ukumbi ni kutumika kwenye matukio yanayohusisha wanafunzi wengi. Yaani ukumbi unaweza kuwahifadhi hata wanafunzi wote kwa mara moja.

Hiyo shule inayoshindwa kuwa chumba hata cha kuwahifadhi japo wanafunzi wa darasa moja tu, itakuwa ni shule zile duni kabisa.

Tunafanya matumizi ya hovyo ya kutapanya pesa za nchi kama kuzurula nje na wasanii, kunua magoli, misafara mirefu ya watawala, wakati hata vitu basic kabisa, hatuna!!
 
Back
Top Bottom