Machali: Watu kama Tundu Lissu, Magufuli angeamuru wachapwe bakora

Huyu si ni kati ya wale waliokatwa mikia baada ya kurudi chama kubwa?
 
Atulie Asubiri mabwana zake wampe viti maalum. Maana has watu kigoma sasa tumewajua usaliti wenu
 
Tundu Lisu ameendelea na msimamo wake kwamba mikataba ya madini ni ya kinyonyaji, anachompinga Magufuli kwasasa ni namna anavyoshughulikia unyonyaji huu, kwa ufupi anataka unyonyaji huu ushughulikiwe kwa uangalifu bila kulisababishia Taifa Hasara zaidi, ndiyo maana kakumbushia Hasara tuliyo wahi kupata katika kuwashughulikia wezi wa Samaki katika bahari yetu, lakini wenye akili timamu wamemuelewa. by the way nahisi utakua umemnukuu vibaya Machali kwasababu kumbukumbu za hivi karibuni zinaonyesha alikua na akili timamu
Shikamoo mzee!
 
Kwani Mh Rais amefanya nini mpaka hatua hii dhidi ya hao wawekezaji zaidi ya kuzuia export ya huo mchanga ili kujiridhisha dhidi ya madai ya hujuma kupitia machanga huo? mpaka sasa hatua za kinidhamu zimechukuliwa dhidi ya watendaji wa serikali TMAA na wizara ya madini sio wawekezaji. Tusubiri matokeo na mapendekezo ya kamati ya pili ya kisheria tutakapoona mapendekezo yake yana athari hasi, hapo ndipo hofu na tahadhari za Lisu zitabeba maantiki. Na ni utovu wa busara wa hali ya juu kufikia mahali pa ku comment utafikiri kana kwamba Mh Lisu ndio spika ya mkondo wa wanasheria hapa nchini bado wapo wanasheria wabobezi lukuki
ambao hawana political Interests, na bila shaka yoyote naamini sasa hivi wako kazini ili kulisaidia Taifa ktk sakata hili. Turejee hotuba ya Mh Majaliwa bungeni session ya tar 1june wakati wa maswali ya papo kwa papo.
 
Akiongea kwenye kipindi cha jambo leo TBC1 leo kwenye mahojiano maalum yaliyo kuwa yakiendeshwa na mtangazaji Shaban Kisu, aliyekuwa mbunge kupitia NCCR Mageuzi Mhe Machali Sanjari na Dr Yaredi Yakusa wamesema:
  • Wameshangazwa na watu ambao kwa muda mrefu wamepambana kuhakikisha wizi uliokuwa unaendelea unakomeshwa, lakini sasa wamegeuka na wanataka ACACIA waachwe kwa madai ya kuogopa kushitakiwa.
  • Wamshaangaa Mh Tundu Lisu kwa U turn ya aina yake aliyoionyesha baada ya hatua kuanza kuchukuliwa.Amtilia mashaka huenda amehongwa ili anyamaze kwani makampuni haya ni mabingwa kwa rushwa.
  • Adai kuipiti mikataba ya MIGA na kugundua kuwa hakuna mahari ambapo mikakataba hiyo inampa mwanya na kumlinda muwekezaji anapokuwa mwizi ama mdanganyifu.
  • Adai kuwa kwa sasa wanasheria na watetezi wa udanganyifu huu wako kwenye hatua ya ujinga na wanaelekea kwenye hatua ya upumbavu.
  • Awaasa watanzania kusimama pamoja kutetea Mali zao na kuachana na hofu wanayo pandikiziwa.
  • Asema ni heri kupambana Leo na kuihami Mali yetu inayopotea kwa gharama yoyoye na sio kuiacha iendelee kuondoka kwa kisingizio cha kuogopa kushitakiwa.

Mara ingine huwa nagutuka kuwa watu wa hii kanda hawana tofauti na wacongo, warwanda na warundi ambao kila kukicha ni kupigana pigana tu. Yaani kwao ni mbabe ndiyo anayelalia godoro. Sasa ndiyo nini kuchapana tena?
 
NI kweli pale unapomuamini once a State Attorney aliyenunuliwa kwa cheo na shares za Kampuni ya madini leo aje atuambie ati washindani wetu wanaliibia TAIFA ,hivi nani aliyeliibia TAIFA uliyenunuliwa kwa cheo na shares au Lissu anayetaka kila kitu kifuate sheria ili tusilipe zaidi??

Hebu jiulize kwanini hao Douglas Lake Mineral hawakumpa huyo waziri wenu nafasi za Uanasheria wa kampuni au Usecretary wa kampuni husika??

Nitakupa jibu,wazungu wanatendency moja wakishajua weakness yako wanakumaliza,walijua weakness ya Kalemani na kwa sababu walijua wakafikiria hivi Mwanasheria aliyeuza Raslimali za TAIFA lake kwa kiwango hicho na akakubali kupewa cheo na hsares chache ukimpa uanasheria au Usecratary wa Kampuni atauza kampuni kwa mikataba mibovu,leo ndiyo mmempa nafasi ya Unaibu Waziri wa Nishati na Madini kisa wa kwetu.

Kwa mwenye akili Lissu anajua anachokizungumza msilete mzaha kwenye kuvunja mikataba mliyoiweka wenyewe baada ya kuuza nchi kwa punje za mtama.
Nani kavunja mkataba mpaka sasa au serikali haina haki ya kuhakiki allegations za udanganyifu kupitia export ya mchanga?
 
Tundu Lisu ameendelea na msimamo wake kwamba mikataba ya madini ni ya kinyonyaji, anachompinga Magufuli kwasasa ni namna anavyoshughulikia unyonyaji huu, kwa ufupi anataka unyonyaji huu ushughulikiwe kwa uangalifu bila kulisababishia Taifa Hasara zaidi, ndiyo maana kakumbushia Hasara tuliyo wahi kupata katika kuwashughulikia wezi wa Samaki katika bahari yetu, lakini wenye akili timamu wamemuelewa. by the way nahisi utakua umemnukuu vibaya Machali kwasababu kumbukumbu za hivi karibuni zinaonyesha alikua na akili timamu
Mkataba hauhusiki. Huyu ni mwizi, period. Unamtetea wa nini? Kwani MIGA inaruhusu wizi? Kwani Canada inaruhusu wizi? Tundulissu aende aombe kazi awe wakili wa wezi amtetee mwizi. Ondoka hapa usituchanganye.
 
Jimbo aliuza kwa Zitto fedha katumia zimeisha sasa anataka kacheo kutoka kwa Msukuma hajui kuwa jamaa hataki kupangiwa, maneno haya naomba tuyatunze mpaka 2020
 
Tundu Lisu ameendelea na msimamo wake kwamba mikataba ya madini ni ya kinyonyaji, anachompinga Magufuli kwasasa ni namna anavyoshughulikia unyonyaji huu, kwa ufupi anataka unyonyaji huu ushughulikiwe kwa uangalifu bila kulisababishia Taifa Hasara zaidi, ndiyo maana kakumbushia Hasara tuliyo wahi kupata katika kuwashughulikia wezi wa Samaki katika bahari yetu, lakini wenye akili timamu wamemuelewa. by the way nahisi utakua umemnukuu vibaya Machali kwasababu kumbukumbu za hivi karibuni zinaonyesha alikua na akili timamu
Hili ndo wanalipindisha, nadhani nia yao ni kufanya watu wasielewe ili waendelee kuwaamini.
 
Back
Top Bottom