Mabishano kati ya Wakili Kibatala na shahidi, kesi ya Boniface Jacob na Malisa

CHRC

Member
Aug 2, 2011
40
39
Kesi ya jinai nambari 11805 Jamhuri dhidi ya Boniface Jacob na Godlisten Malisa ilisikilizwa juzi, Jumanne, Aprili 12, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Ifuatayo ni sehemu ya cross examination kati ya Wakili Msomi Peter Kibatala na Shahidi wa Jamhuri.

KIBATALA: Shahidi, ikumbushe Mahakamaa unaitwa nani?

SHAHIDI: Staff Sergeant Lugano (anataja Force number yake).

KIBATALA: Kazi yako?

SHAHIDI: Askari polisi.

KIBATALA: Kituo chako cha kazi?

SHAHIDI: ofisi ya ZCO kanda maalumu Dar.

KIBATALA: Majukumu yako?

SHAHIDI: Mimi ni Mpelelzi lakini pia nafanya kazi kama dereva.

KIBATALA: Shahidi, hivi kuna tija yoyote kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Sijatoa ushahidi wa kutunga.

KIBATALA: Sijasema umetunga, nimekuuliza: hivi kuna tija yoyote mtu kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Nimekula kiapo, na kwenye kiapo hakuna kutunga.

KIBATALA: Sijakuuliza kama kwenye kiapo kuna kutunga au hakuna. Nimekuuliza: kuna tija yoyote mtu kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani? Jibu ndiyo au hapana.

SHAHIDI: Mimi sijatunga ushahidi.

HAKIMU: Shahidi, nakuonya. Jibu maswali kama unavyoulizwa.

KIBATALA: Shahidi, nakuuliza mara ya mwisho. Kuna tija yoyote kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?

SHAHIDI: Hakuna tija.

KIBATALA: Unajua ushahidi utakaoutoa utatumika kupima uwezo wako wa akili, hekima na uadilifu wako?

SHAHIDI: Nina akili timamu.

KIBATALA: Sijasema huna akili timamu. Nimesema: unajua kwamba ushahidi utakaoutoa utatumika kupima akili yako, hekima yako na uadilifu wako?

SHAHIDI: Nimekuja kutoa ushahidi nikiwa na akili timamu.

KIBATALA: Shahidi, acha kujitungia maswali. Jibu kama ninavyokuuliza.

SHAHIDI: Unanipimaje akili wakati nina akili timamu?

KIBATALA: Usiniulize maswali. Mimi ndiye natakiwa nikuulize wewe. Kazi yako ni kujibu.

HAKIMU: Shahidi, upo chini ya kiapo. Tafadhali Jibu kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Mheshimiwa, ananiuliza maswali kwa malengo yake.
KIBATALA: Ndiyo, ni kwa malengo yangu kama wakili. Kwa hiyo tuliza kichwa ujibu.

KIBATALA: Unajua kwamba ushahidi utakaoutoa utatumika kupima uwezo wako wa akili, hekima na uadilifu wako? Ndiyo ama hapana?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Umesema wewe ni dereva wa polisi?

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Umeonesha leseni ili kuthibitisha kama kweli wewe ni dereva?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Jibu swali, leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Shahidi, usijitungie maswali ambayo hujaulizwa, unaipotezea mahakama muda. Leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaulizwa.

KIBATALA: Unajifanya mjanja eeh? Tutakaa hadi saa 9 hapa.

SHAHIDI: Hata tukikaa hadi saa 10 hakuna shida. Ninao muda.

HAKIMU: Shahidi, nakuonya, jibu maswali kama unavyoulizwa.

KIBATALA: Leseni umeonesha au hujaonesha?

SHAHIDI: Sijaonesha.

KIBATALA: Umemwambia Mheshimiwa Hakimu kama ulishuhudia Boniface Jacob akipewa haki zake wakati anahojiwa?

SHAHIDI: Sio kazi yangu. Ni kazi ya mpelelezi.

KIBATALA: Hapa nakuhoji wewe sio mpelelezi.

SHAHIDI: Jukumu la kuhakikisha mtuhumiwa anapewa haki zake ni la mpelelezi.

KIBATALA: Shahidi, elewa swali. Umemwambia Hakimu kama ulishuhudia Boniface akipewa haki zake wakati anahojiwa?

SHAHIDI: Mimi nilikuta tayari ameshahojiwa.

HAKIMU: Shahidi, jibu swali kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, Wakili hanipi nafasi ya kutoa ufafanuzi.

HAKIMU: Wewe jibu kama anavyokuuliza, akitaka ufafanuzi atakuambia.

KIBATALA: Shahidi, ulimwambia Hakimu kama ulishuhudia mshtakiwa Boniface Jacob akipewa haki zake kwa mujibu wa sheria? Umemwambia au hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Sasa mbona ulikuwa unapoteza muda wa mahakama bure?

KIBATALA: Shahidi, una elimu gani?

SHAHIDI: Elimu yangu haikuhusu.

KIBATALA: Inanihusu.

SHAHIDI: Haikuhusu.

KIBATALA: Unataka nikuoneshe kama inanihusu? (Anafungua nyaraka na kusoma vifungu, kabla hajamaliza Hakimu anaingilia kati).

HAKIMU: Shahidi, una wajibu kisheria wa kutaja elimu yako ikiwa Wakili atahitaji kufahamu.

SHAHIDI: Elimu yangu ni Form Four.

KIBATALA: Kumbe ndiyo maana ulikuwa unakataa kutaja? Sikuulizi ulipata division ngapi usije ukashindwa kuendelea na ushahidi.

MAHAKAMA: (Kicheko)

KIBATALA: Sheria inataka mtuhumiwa kabla hajapekuliwa, yeye awapekue kwanza askari. Je, ulimwambia Hakimu kama Boniface alipata nafasi ya kuwapekua askari?

KIBATALA: Shahidi, hapa umeletwa wewe au mpelelezi?

SHAHIDI: Mpelelezi atakuja utamuuliza.

KIBATALA: Kwa sasa mahakamani mpelelezi yupo?

SHAHIDI: Atakuja.

KIBATALA: Nakuuliza wewe, umemwambia Hakimu kama ulishuhudia Boniface akiwapekua askari kabla? Umemwambia, hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Sasa kwa nini unapoteza muda wa mahakama?

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, samahani, naomba kumuelimisha kidogo Wakili.

KIBATALA: Huwezi kunielimisha chochote. Hapa umekuja kujibu maswali, sio kuelimisha. Kama unataka kunielimisha subiri nikija kituo cha polisi, lakini hapa upo kwenye himaya yangu, na utajibu maswali kama navyokuuliza.

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, naomba kumuelimisha Wakili kuhusu taratibu za utendaji kazi za polisi.

HAKIMU: Jibu maswali kama anavyokuuliza. Akitaka kujua taratibu za kazi atakuuliza.

SHAHIDI: Sawa Mheshimiwa.

KIBATALA: Pole sana Shahidi, unajisikia vibaya?

SHAHIDI: Hapana.

MAHAKAMA: (Kicheko).

KIBATALA: Umesema wakati wa upekuzi nyumbani kwa Boniface kuna jirani aliitwa kushuhudia.

SHAHIDI: Ndiyo.

KIBATALA: Anaitwa nani?

SHAHIDI: George Steven.

KIBATALA: Unajua kwamba hakuna jirani yeyote wa Boniface mwenye jina hilo?

SHAHIDI: Anaitwa George Steven.

KIBATALA: Unajua kwamba kati ya majirani wanaomzunguka Boniface ni mmoja tu mwenye jina Frank Steven. Na hata huyo si yeye aliyekuja kushuhudia upekuzi.

SHAHIDI: Mi sikumbuki.

KIBATALA: Jina la jirani aliyeshuhudia upekuzi lipo kwenye nyaraka zenu au halipo?

SHAHIDI: Lipo.

KIBATALA: Na nyaraka hizo umezipitia lini mara ya mwisho?

SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, Wakili ananiuliza maswali bila kunipa nafasi ya ufafanuzi.

HAKIMU: Amekuambia anataka ufafanuzi?

SHAHIDI: (Kimya).

HAKIMU: We jibu kama anavyokuuliza, akitaka ufafanuzi atakuambia. Pia baadae una nafasi ya kutoa ufafanuzi kadri utakavyoongozwa na Wakili wa Jamhuri.

SHAHIDI: Sawa, Mheshimiwa.

KIBATALA: Unafahamu kuwa Bonny ni kiongozi wa kisiasa mwenye wafuasi wengi na anayefahamika ndani na nje ya nchi?

SHAHIDI: Labda anafahamika na familia yake.

KIBATALA: Familia yake haihusiki hapa. Nimekuuliza wewe.

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajua Bonny amewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajua Bonny ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani na alishinda akiwa gerezani?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Unajifanya mjanja eeh? Sasa hao waliokutuma leo utaenda kuwaambia ulichokutana nacho mahakamani.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mlipoenda kumpekua Bonny mlichukua simu aina gani yenye IMEI number gani?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu kama Bonny alisaini hati ya upekuzi?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ukiwa dereva wa gari la polisi lililoenda nyumbani kwa Bonny, ulimwambia Hakimu nani alifungua geti?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ulipokuja hapa umeoneshwa hati ya upekuzi ili uitambue?

SHAHIDI: Hiyo ataoneshwa mpelelezi.

KIBATALA: Jibu swali, usijitungie maswali yako.

SHAHIDI: Utaratibu wa kazi haupo hivyo.

KIBATALA: Sijakuuliza utaratibu wa kazi zenu. Nimekuuliza umeoneshwa hati ya upekuzi au hujaoneshwa?

SHAHIDI: Sio kazi yangu.

HAKIMU: Shahidi nakuonya upo chini ya kiapo, jibu maswali kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Sijaoneshwa Mheshimiwa.

KIBATALA: Sasa kwa nini unatupotezea muda?

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mlipotoka kwa Bonny mlielekea wapi?

SHAHIDI: Tulirudi ofisi ya ZCO.

KIBATALA: Elewa swali. Umemwambia Hakimu au hujamwambia?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Umemwambia Hakimu mliporudi kituoni mliripoti kwa nani?

SHAHIDI: Sijamwambia.

KIBATALA: Ni hayo tu Mheshimiwa.

HAKIMU: Jamhuri kuna re-examination?

JAMHURI: Hapana Mheshimiwa.

HAKIMU: Shahidi, tumemaliza unaweza kuondoka.

HAKIMU: Upande wa Jamhuri mmebakiza mashahidi wangapi?

JAMHURI: 10 Mheshimiwa.

HAKIMU: Kama mashahidi wenyewe ni kama huyu, nashauri mulete watatu watatu.

MAHAKAMA: (Kicheko).

HAKIMU: Namaanisha kama watatoa ushahidi mfupi kama huyu basi waje watatu watatu ili tumalize haraka.

JAMHURI: Sawa Mheshimiwa.

Credit:page ya malisa fb
HAKIMU: Kesi imeahirishwa itasikilizwa mfululizo tarehe 05, 06 na 07 Mei 2025.
 
Hivi haya mazungumzo nani huwa ni shahidi wa kuthibitisha ya kuwa ni kweli yalikuwa hivyo ?

Ni kama tungo fulani hivi, fulani ambayo inaonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye pande zote mbili.

Katika mazungumzo hayo inaonyesha ni kuwa mara nyingi mawalkili hukutana na watu ambao hawajui lugha, na hao mawalkili wanauliza maswali pasi na kuzingatia ufasaha wa lugha. Natamani siku wakutane na mjuzi wa lugha, kwa maana kila nukta anarekebishwa yeye kwanza Kabla ya kuendelea na swali lingine.

Kwa ufupi hufanya uhuni katika kuuliza maswali.
 
Ukishakula kiapo mahakamani Unachoulizwa na wakili ndiyo unachotakiwa kujibu tu! Hakuna explanations wala kukosoa swali.
Kama ni ndiyo jibu ndiyo
Kama ni hapana jibu hapana
 
Ningekuwa Mimi hapo, ningemjibu tu "Sijui". Sababu inaonekana hata yeye hajui ana muhoji mtu mwenye sifa gani.

Kwanini alazimishe ndiyo au hapana tu. Lazima ajielezee na yeye.
Hakunaga kesi kama hiyo jombaa na ndiyo maana hakimu alikuwa anasimamia ya wakili ili mtuhumiwa ajibu kile alichoulizwa tu kama ni ndiyo ni ndiyo...no more explanations
Kama hapana ni hapana....
Anaingia next question
 
Ndio maana nasema Kuna madhaifu makubwa sana katika uendeshaji wa kesi zenu. Ni uhuni na uchache wa maarifa. Ndio maana hata muhalifu huwa anatetewa na akashinda.
 
Naendesha kwa uadilifu na maarifa, zenu zimekosa uadilifu lakini wakili akiuliza anataka mtu awe Muadilifu wakati yeye sio Muadilifu.
Unajua kuwa yale maswali yametokana na ushahidi ambao ameshaieleza mahakama? Kwahiyo anakuwa amemaliza ni mwendo wa ndiyo au hapana yaan ni kujibu alichoulizwa no more explanation wala arguments lete case study moja iliyoendelea tujifunze
 
Ndio maana nikasema Sheria zenu Zina shida. Unapopewa ushahidi tayari unatakiwa wewe kama wakili uhakiki usahihi wa ushahidi huo, sio tena kurudi mule mule, ni kupotezeana muda.
 
Hivi haya mazungumzo nani huwa ni shahidi wa kuthibitisha ya kuwa ni kweli yalikuwa hivyo ?

Ni kama tungo fulani hivi, fulani ambayo inaonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye pande zote mbili.

Katika mazungumzo hayo inaonyesha ni kuwa mara nyingi mawalkili hukutana na watu ambao hawajui lugha, na hao mawalkili wanauliza maswali pasi na kuzingatia ufasaha wa lugha. Natamani siku wakutane na mjuzi wa lugha, kwa maana kila nukta anarekebishwa yeye kwanza Kabla ya kuendelea na swali lingine.

Kwa ufupi hufanya uhuni katika kuuliza maswali.

Ndio maana nikasema Sheria zenu Zina shida. Unapopewa ushahidi tayari unatakiwa wewe kama wakili uhakiki usahihi wa ushahidi huo, sio tena kurudi mule mule, ni kupotezeana muda.
Unajua kama maswali anayouliza ni yale ameona mapungufu kwenye ushahidi aliowakilisha mahakamani? Maana mengi si umeona anajibu hapana, sijui, sasa kulikuwa na haja gani ya kutoa ushahidi na mengi ni hapana na hajui ndiyo maana hakimu akasema kama mashahidi ndiyo kama hao waletwe watatu🤣
 
Hivi haya mazungumzo nani huwa ni shahidi wa kuthibitisha ya kuwa ni kweli yalikuwa hivyo ?

Ni kama tungo fulani hivi, fulani ambayo inaonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye pande zote mbili.

Katika mazungumzo hayo inaonyesha ni kuwa mara nyingi mawalkili hukutana na watu ambao hawajui lugha, na hao mawalkili wanauliza maswali pasi na kuzingatia ufasaha wa lugha. Natamani siku wakutane na mjuzi wa lugha, kwa maana kila nukta anarekebishwa yeye kwanza Kabla ya kuendelea na swali lingine.

Kwa ufupi hufanya uhuni katika kuuliza maswali.
Hakuna uhuni, labda hujui cross examination, au maswali ya uhakiki ya uliyoyaeleza mahakamani yana mashiko au hakuna. Wakili upande wa mashitaka alitakiwa amuulize tena maswali ya ufafanuzi kama angeona kuna haja ya ufafanuz toka kwa shahidi.
Mahakamani haupeleki stori, unaenda na maelezo yenye ushahidi. Kama pale aliposema jirani aneitwa George Steven, wakati hakuna mtu kama huyo.
 
Back
Top Bottom