Kesi ya jinai nambari 11805 Jamhuri dhidi ya Boniface Jacob na Godlisten Malisa ilisikilizwa juzi, Jumanne, Aprili 12, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Ifuatayo ni sehemu ya cross examination kati ya Wakili Msomi Peter Kibatala na Shahidi wa Jamhuri.
KIBATALA: Shahidi, ikumbushe Mahakamaa unaitwa nani?
SHAHIDI: Staff Sergeant Lugano (anataja Force number yake).
KIBATALA: Kazi yako?
SHAHIDI: Askari polisi.
KIBATALA: Kituo chako cha kazi?
SHAHIDI: ofisi ya ZCO kanda maalumu Dar.
KIBATALA: Majukumu yako?
SHAHIDI: Mimi ni Mpelelzi lakini pia nafanya kazi kama dereva.
KIBATALA: Shahidi, hivi kuna tija yoyote kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?
SHAHIDI: Sijatoa ushahidi wa kutunga.
KIBATALA: Sijasema umetunga, nimekuuliza: hivi kuna tija yoyote mtu kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?
SHAHIDI: Nimekula kiapo, na kwenye kiapo hakuna kutunga.
KIBATALA: Sijakuuliza kama kwenye kiapo kuna kutunga au hakuna. Nimekuuliza: kuna tija yoyote mtu kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani? Jibu ndiyo au hapana.
SHAHIDI: Mimi sijatunga ushahidi.
HAKIMU: Shahidi, nakuonya. Jibu maswali kama unavyoulizwa.
KIBATALA: Shahidi, nakuuliza mara ya mwisho. Kuna tija yoyote kutoa ushahidi wa kutunga mahakamani?
SHAHIDI: Hakuna tija.
KIBATALA: Unajua ushahidi utakaoutoa utatumika kupima uwezo wako wa akili, hekima na uadilifu wako?
SHAHIDI: Nina akili timamu.
KIBATALA: Sijasema huna akili timamu. Nimesema: unajua kwamba ushahidi utakaoutoa utatumika kupima akili yako, hekima yako na uadilifu wako?
SHAHIDI: Nimekuja kutoa ushahidi nikiwa na akili timamu.
KIBATALA: Shahidi, acha kujitungia maswali. Jibu kama ninavyokuuliza.
SHAHIDI: Unanipimaje akili wakati nina akili timamu?
KIBATALA: Usiniulize maswali. Mimi ndiye natakiwa nikuulize wewe. Kazi yako ni kujibu.
HAKIMU: Shahidi, upo chini ya kiapo. Tafadhali Jibu kama unavyoulizwa.
SHAHIDI: Mheshimiwa, ananiuliza maswali kwa malengo yake.
KIBATALA: Ndiyo, ni kwa malengo yangu kama wakili. Kwa hiyo tuliza kichwa ujibu.
KIBATALA: Unajua kwamba ushahidi utakaoutoa utatumika kupima uwezo wako wa akili, hekima na uadilifu wako? Ndiyo ama hapana?
SHAHIDI: Ndiyo.
KIBATALA: Umesema wewe ni dereva wa polisi?
SHAHIDI: Ndiyo.
KIBATALA: Umeonesha leseni ili kuthibitisha kama kweli wewe ni dereva?
SHAHIDI: Sijaulizwa.
KIBATALA: Jibu swali, leseni umeonesha au hujaonesha?
SHAHIDI: Sijaulizwa.
KIBATALA: Shahidi, usijitungie maswali ambayo hujaulizwa, unaipotezea mahakama muda. Leseni umeonesha au hujaonesha?
SHAHIDI: Sijaulizwa.
KIBATALA: Unajifanya mjanja eeh? Tutakaa hadi saa 9 hapa.
SHAHIDI: Hata tukikaa hadi saa 10 hakuna shida. Ninao muda.
HAKIMU: Shahidi, nakuonya, jibu maswali kama unavyoulizwa.
KIBATALA: Leseni umeonesha au hujaonesha?
SHAHIDI: Sijaonesha.
KIBATALA: Umemwambia Mheshimiwa Hakimu kama ulishuhudia Boniface Jacob akipewa haki zake wakati anahojiwa?
SHAHIDI: Sio kazi yangu. Ni kazi ya mpelelezi.
KIBATALA: Hapa nakuhoji wewe sio mpelelezi.
SHAHIDI: Jukumu la kuhakikisha mtuhumiwa anapewa haki zake ni la mpelelezi.
KIBATALA: Shahidi, elewa swali. Umemwambia Hakimu kama ulishuhudia Boniface akipewa haki zake wakati anahojiwa?
SHAHIDI: Mimi nilikuta tayari ameshahojiwa.
HAKIMU: Shahidi, jibu swali kama unavyoulizwa.
SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, Wakili hanipi nafasi ya kutoa ufafanuzi.
HAKIMU: Wewe jibu kama anavyokuuliza, akitaka ufafanuzi atakuambia.
KIBATALA: Shahidi, ulimwambia Hakimu kama ulishuhudia mshtakiwa Boniface Jacob akipewa haki zake kwa mujibu wa sheria? Umemwambia au hujamwambia?
SHAHIDI: Sijamwambia.
KIBATALA: Sasa mbona ulikuwa unapoteza muda wa mahakama bure?
KIBATALA: Shahidi, una elimu gani?
SHAHIDI: Elimu yangu haikuhusu.
KIBATALA: Inanihusu.
SHAHIDI: Haikuhusu.
KIBATALA: Unataka nikuoneshe kama inanihusu? (Anafungua nyaraka na kusoma vifungu, kabla hajamaliza Hakimu anaingilia kati).
HAKIMU: Shahidi, una wajibu kisheria wa kutaja elimu yako ikiwa Wakili atahitaji kufahamu.
SHAHIDI: Elimu yangu ni Form Four.
KIBATALA: Kumbe ndiyo maana ulikuwa unakataa kutaja? Sikuulizi ulipata division ngapi usije ukashindwa kuendelea na ushahidi.
MAHAKAMA: (Kicheko)
KIBATALA: Sheria inataka mtuhumiwa kabla hajapekuliwa, yeye awapekue kwanza askari. Je, ulimwambia Hakimu kama Boniface alipata nafasi ya kuwapekua askari?

KIBATALA: Shahidi, hapa umeletwa wewe au mpelelezi?
SHAHIDI: Mpelelezi atakuja utamuuliza.
KIBATALA: Kwa sasa mahakamani mpelelezi yupo?
SHAHIDI: Atakuja.
KIBATALA: Nakuuliza wewe, umemwambia Hakimu kama ulishuhudia Boniface akiwapekua askari kabla? Umemwambia, hujamwambia?
SHAHIDI: Sijamwambia.
KIBATALA: Sasa kwa nini unapoteza muda wa mahakama?
SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, samahani, naomba kumuelimisha kidogo Wakili.
KIBATALA: Huwezi kunielimisha chochote. Hapa umekuja kujibu maswali, sio kuelimisha. Kama unataka kunielimisha subiri nikija kituo cha polisi, lakini hapa upo kwenye himaya yangu, na utajibu maswali kama navyokuuliza.
SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, naomba kumuelimisha Wakili kuhusu taratibu za utendaji kazi za polisi.
HAKIMU: Jibu maswali kama anavyokuuliza. Akitaka kujua taratibu za kazi atakuuliza.
SHAHIDI: Sawa Mheshimiwa.
KIBATALA: Pole sana Shahidi, unajisikia vibaya?
SHAHIDI: Hapana.
MAHAKAMA: (Kicheko).
KIBATALA: Umesema wakati wa upekuzi nyumbani kwa Boniface kuna jirani aliitwa kushuhudia.
SHAHIDI: Ndiyo.
KIBATALA: Anaitwa nani?
SHAHIDI: George Steven.
KIBATALA: Unajua kwamba hakuna jirani yeyote wa Boniface mwenye jina hilo?
SHAHIDI: Anaitwa George Steven.
KIBATALA: Unajua kwamba kati ya majirani wanaomzunguka Boniface ni mmoja tu mwenye jina Frank Steven. Na hata huyo si yeye aliyekuja kushuhudia upekuzi.
SHAHIDI: Mi sikumbuki.
KIBATALA: Jina la jirani aliyeshuhudia upekuzi lipo kwenye nyaraka zenu au halipo?
SHAHIDI: Lipo.
KIBATALA: Na nyaraka hizo umezipitia lini mara ya mwisho?
SHAHIDI: Mheshimiwa Hakimu, Wakili ananiuliza maswali bila kunipa nafasi ya ufafanuzi.
HAKIMU: Amekuambia anataka ufafanuzi?
SHAHIDI: (Kimya).
HAKIMU: We jibu kama anavyokuuliza, akitaka ufafanuzi atakuambia. Pia baadae una nafasi ya kutoa ufafanuzi kadri utakavyoongozwa na Wakili wa Jamhuri.
SHAHIDI: Sawa, Mheshimiwa.
KIBATALA: Unafahamu kuwa Bonny ni kiongozi wa kisiasa mwenye wafuasi wengi na anayefahamika ndani na nje ya nchi?
SHAHIDI: Labda anafahamika na familia yake.
KIBATALA: Familia yake haihusiki hapa. Nimekuuliza wewe.
SHAHIDI: Sijui.
KIBATALA: Unajua Bonny amewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo?
SHAHIDI: Sijui.
KIBATALA: Unajua Bonny ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani na alishinda akiwa gerezani?
SHAHIDI: Sijui.
KIBATALA: Unajifanya mjanja eeh? Sasa hao waliokutuma leo utaenda kuwaambia ulichokutana nacho mahakamani.
KIBATALA: Umemwambia Hakimu mlipoenda kumpekua Bonny mlichukua simu aina gani yenye IMEI number gani?
SHAHIDI: Sijamwambia.
KIBATALA: Umemwambia Hakimu kama Bonny alisaini hati ya upekuzi?
SHAHIDI: Sijamwambia.
KIBATALA: Ukiwa dereva wa gari la polisi lililoenda nyumbani kwa Bonny, ulimwambia Hakimu nani alifungua geti?
SHAHIDI: Sijamwambia.
KIBATALA: Ulipokuja hapa umeoneshwa hati ya upekuzi ili uitambue?
SHAHIDI: Hiyo ataoneshwa mpelelezi.
KIBATALA: Jibu swali, usijitungie maswali yako.
SHAHIDI: Utaratibu wa kazi haupo hivyo.
KIBATALA: Sijakuuliza utaratibu wa kazi zenu. Nimekuuliza umeoneshwa hati ya upekuzi au hujaoneshwa?
SHAHIDI: Sio kazi yangu.
HAKIMU: Shahidi nakuonya upo chini ya kiapo, jibu maswali kama unavyoulizwa.
SHAHIDI: Sijaoneshwa Mheshimiwa.
KIBATALA: Sasa kwa nini unatupotezea muda?
KIBATALA: Umemwambia Hakimu mlipotoka kwa Bonny mlielekea wapi?
SHAHIDI: Tulirudi ofisi ya ZCO.
KIBATALA: Elewa swali. Umemwambia Hakimu au hujamwambia?
SHAHIDI: Sijamwambia.
KIBATALA: Umemwambia Hakimu mliporudi kituoni mliripoti kwa nani?
SHAHIDI: Sijamwambia.
KIBATALA: Ni hayo tu Mheshimiwa.
HAKIMU: Jamhuri kuna re-examination?
JAMHURI: Hapana Mheshimiwa.
HAKIMU: Shahidi, tumemaliza unaweza kuondoka.
HAKIMU: Upande wa Jamhuri mmebakiza mashahidi wangapi?
JAMHURI: 10 Mheshimiwa.
HAKIMU: Kama mashahidi wenyewe ni kama huyu, nashauri mulete watatu watatu.
MAHAKAMA: (Kicheko).
HAKIMU: Namaanisha kama watatoa ushahidi mfupi kama huyu basi waje watatu watatu ili tumalize haraka.
JAMHURI: Sawa Mheshimiwa.
Credit age ya malisa fb
HAKIMU: Kesi imeahirishwa itasikilizwa mfululizo tarehe 05, 06 na 07 Mei 2025.

Credit