yule mwanasiasa machachari wa mageuzi mpiganaji mabere nyaucho marando, amechukua form ya kugombea uspika wa bunge la jamuhuri ya muungano kupitia chadema.
Pamoja na yeye kuna vijana wengine kama watatu waliojitokeza kupitia chadema. (source: Itv news bulletin)
kama muujiza ukitokea na marando akawa spika wa bunge, basi katiba mpya iko mbioni kupatikana kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Pia itakuwa ni pigo kubwa kwa mafisadi wote.
marando hafai kabisa kuwa spika ni mtu wa majungu na ndie aliechangia kwa kiasi kikubwa kusambaratika kwa upinzani miaka ile ya 90 wakati alipokuwa na mgogoro wa kugombea madaraka yeye na lyatonga mrema!
Pili ni msaliti mkubwa kwa upinzani wakati wapinzani walikuwa na chaguo lao la mbunge wa afrika mashariki cha kushangaza huyu marando alipigiwa debe na ccm na kuibuka mshindi!!!
Sasa kama yeye ni miganaji mbona alisambaratisha nccr na baadae kukimbilia chadema tena karibia na uchaguzi?
Kama alikuwa na hamu yauspika kwanini hakugombea ubunge ktk jimbo la uchaguzi ili apate ridhaa ya wananchi na ndipo aje kugombea uspika lakini anangojea kapu maalum!!!
It is possible bunge lina viti kama 323 hivi hadi sasa wapinzani wana kura(viti) kama 100 bado kama 50, mavuvuzela yakijichanganya kama yalivyoanza kuzomeana kwenye vyombo vya habari yanagawa kura zao kwa chuki wakitahamaki tayari kumekucha.
ni marando kupitia Chadema, ana jazba, hasira na hamaki. hawezi kuwa spika wa bunge letu hili.
atanaweza kupitisha misaada ya hasira na kutuingiza taifa ktk mitafaruku hasa kwa majirani zetu
nadhani apatikane spika makini
Piga picha ifuatayo ya safu ya hoja Nzitto kwa maslahi ya taifa:
1. Spika - Marando - (Muunda Kamati)
2. Tindu Lissu - Hoja binafsi ya Katiba
3. Mwakyembe - Mwenyekiti wa Tume Maalumu ya Kuunda Katiba Mpya
4. Zitto Kabwe - Mjumbe wa Kamati
5. Halima Mdee - Mjumbe wa Kamati na Katibu wa Kamati
6. Anne Kilango - Mjumbe wa Kamati
7. Freeman Mbowe - Mjumbe wa Kamati
8. Hamadi Rashidi - Makamu Mwenyekiti wa Kamati
.
.
.
Hebu nimalizieni kamati hii ya watu 10 itakayoleta Tanzania Mpya . . . . Mmmh! Au naota tu?
cuf hawana uzalendo kihivyo na baraMkuu Superman,
Ninakubaliana na analysis ya kwako, hapa cha kuomba ni kimoja mipasuko iendelee ndani ya chama ili kuiweka CC kwenye wakati mgumu zaidi. Tatizo la wabunge wengi wa CCM ni wepesi kurubuniwa na mafisadi. Tone ya wabunge siku Lowassa anaachia ngazi ilikuwa kali sana, after few days wengi walishaanza kubadilisha misimamo yao. Lakini kwa misukosuko waliyoipata majimboni hawana uhakika kama 2015 watabahatika tena kurudi mjengoni nina imani watakuwa makini kwenye upigaji kura wao na salaam za wapiga kura za mwaka huu zitawafanya watumie akili kupiga kura.
Marando ana maswahiba wengi CCM na hata kwenye Bunge la Afrika Mashariki walimpa kura nyingi tu, lakini hicho hakiwezi kuwa kigezo, maana wakati huo alikuwa akigombea na watu wengine wa kambi ya upinzani. Kama anagombea na m-CCM mwenzao, ili wampe kura lazima wawe na uhakika kwamba huyo m-CCM ni mchafu au akichaguliwa kuwa Spika atawaharibia mbio zao za kurudi mjengoni ifikapo mwaka 2015.
Nilisikia pia Mh. Hamad Rashid nae alikuwa anafikiria kugombea, nadhani hapo ndipo panaweza kuwa na tatizo. Sina tatizo na wote wawili, lakini wangekaa na kukubaliana ili mmoja kati yao aungwe mkono na Kambi yote upinzani [minus Mrema wa TLP].