Mabalozi wa Tanzania wanaweza kuwashawishi Diaspora kuvaa mavazi yatakayoitangaza vema nchi kila ifikapo tarehe 9 au 26 ya kila mwezi

Hiki unachosema ni kweli, ila hiki si kitu unatakiwa uwaambie wafanye, ni kitu kinatokea naturally, sasa jiulize kwann hakifanyiki?

Uzalendo kwa sasa ni shida kidogo, kwa huu ukandamizi na uonevu usitarajie moyo wa kizalendo...
Sidhani kma ukandamizaji na kuitangaza nchi yetu vinahusiana!!
kwani wee ukiwa mtu wa dini flani kisha kiongozi wako wa dini akawa mchafu asie na maadili je utaikana dini yako sababu yake??!!huo ni mfano tuu.
Nchi lazma tuipe haki yake ni matter what
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi Infantry Soldier na classmate wangu Beautiful Nkosazana tupo wazima sana.

Hivi Tunao watanzania wangapi wanaoishi nje ya nchi kwa uhalali? Ni kwa namna gani na kwa mbinu ipi mabalozi/serikali inawatumia katika kuitangaza vema nchi yetu? Mimi maoni yangu ni haya;

Mabalozi wa Tanzania wanaweza kuwashawishi Diasporas kwa uungwana/diplomatically kuvaa t-shirts/mavazi yatakayoitangaza vema nchi yetu kila ifikapo tarehe 9 ama 26 ya kila mwezi. Public Relations Advice.
View attachment 967330View attachment 967332
Kwanini ni tarehe 9 ama 26 ya kila mwisho wa mwezi? Jibu ni rahisi sana. Nimechagua tarehe 9 ama 26 kwa maana tarehe 9 ndio siku ambayo Tanganika ilipata uhuru na kuwa Jamuhuri kamili na tarehe 26 ndio Tanzania iliundwa.

Mavazi/T-shirts zinakuwa na ujumbe mmoja kwa lugha tofauti kulingana na lugha mama ya nchi husika.

(1) Marekani na Uingereza >>> Welcome to Tanzania the home of mount Kilimanjaro and Serengeti.

(2) Ujeremani >>> Willkommen in Tansania, der Heimat des Kilimanjaro und der Serengeti.

(3) Russia >>> Добро пожаловать в Танзанию, дом горы Килиманджаро и Серенгети

(4) Italy >>> Benvenuti in Tanzania, la patria del monte Kilimanjaro e del Serengeti

(5) France >>> Bienvenue en Tanzanie, la maison du mont Kilimandjaro et du Serengeti.

(6) China >>> 欢迎来到坦桑尼亚乞力马扎罗山和塞伦盖蒂的家

Inakuwa hivyo kila taifa tunaweka ujumbe mmoja kwa lugha yake mama.

Jenga picha tu ikifika tarehe 9 watanzania wote wa Ufaransa, Italia, Ujeremani ama Urusi wakafanya hivyo, matokeo chanya yake yapoje?

KIJANA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. TOA MAONI NA USHAURI UTAKAOIJENGA NCHI YAKO ISONGE MBELE.
View attachment 967341

Soma pia>>> Shilingi mia tano ya sarafu ya sasa ilipaswa kufanana na shilingi ishirini ya zamani ili kuitofautisha na shilingi mia mbili ya sasa - JamiiForums
Utukome
 
Uzalendo haushurutishwi wala haushauriwi ,
uzalendo upo au haupo naturally.
Uzalendo haufundishwi darasani.
 
Hakuna kulazimishana kwenye uzalendo. Hakuna mtanzania hata mmoja ambaye amechagua kuzaliwa Tanzania. Na hata nyie mnaojifanya wazalendo sana, laiti kama mngekuwa na nafasi ya kuchagua mzaliwe nchi gani, inawezekana hakuna hata mmoja kati yenu ambaye angechagua kuzaliwa Tanzania. Hivyo basi, acheni kulazimisha uzalendo wenu feki.

Kama wewe unaona Tanzania inakutendea haki, inakutunza, na inakujali, basi kuwa mzalendo. Lakini kama unaona Tanzania inakufanyia dhulma na kukukwaza kwa namna mbalimbali, huna ulazima wa kuwa mzalendo.

Kuna nchi duniani hapa ukifika, unakaa Hotelini, pale hotelini wanaizuia pasipoti yako ya Tanzania, wanasema utapewa pasipoti yako utakapo check out. Hapo ndipo utakapojua kama tanzania si chochote si lolote nje ya Tanzania.

Utaipenda nchi yako pale nchi yako itakapoonyesha utashi wa kutumia dipomasia au nguvu kukutetea mwananchi wake unapopatwa na matatizo nje ya nchi yako. Ukionewa nchi yako inatakiwa iwe tayari kukutetea kwa kutumia hata nguvu. Ukikamatwa na makosa, nchi yako inatakiwa iwe tayari kukutetea kwa kutumia diplomasia.
Leo hii mtanzania ukipata tatizo nje ya tanzania, serikali inasema na anyongwe, kwani ametumwa na serikali.
Acheni kulazimisha uzalendo wenu feki.
 
Kuitangaza vyema nchi kwa mavazi ndio kuitangazaje?! Hata ningekuwa ni miongoni mwa diaspora nisinge fanya ujinga huo.
Hao diaspora wakiomba vitambulisho vya taifa hamuwapi. Waliomba uraia pacha mkakataa, halafu upumbavu wenu waufanye, watakuwa mazombi kweli.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi Infantry Soldier na classmate wangu Beautiful Nkosazana tupo wazima sana.

Hivi Tunao watanzania wangapi wanaoishi nje ya nchi kwa uhalali? Ni kwa namna gani na kwa mbinu ipi mabalozi/serikali inawatumia katika kuitangaza vema nchi yetu? Mimi maoni yangu ni haya;

Mabalozi wa Tanzania wanaweza kuwashawishi Diasporas kwa uungwana/diplomatically kuvaa t-shirts/mavazi yatakayoitangaza vema nchi yetu kila ifikapo tarehe 9 ama 26 ya kila mwezi. Public Relations Advice.
View attachment 967330View attachment 967332
Kwanini ni tarehe 9 ama 26 ya kila mwisho wa mwezi? Jibu ni rahisi sana. Nimechagua tarehe 9 ama 26 kwa maana tarehe 9 ndio siku ambayo Tanganika ilipata uhuru na kuwa Jamuhuri kamili na tarehe 26 ndio Tanzania iliundwa.

Mavazi/T-shirts zinakuwa na ujumbe mmoja kwa lugha tofauti kulingana na lugha mama ya nchi husika.

(1) Marekani na Uingereza >>> Welcome to Tanzania the home of mount Kilimanjaro and Serengeti.

(2) Ujeremani >>> Willkommen in Tansania, der Heimat des Kilimanjaro und der Serengeti.

(3) Russia >>> Добро пожаловать в Танзанию, дом горы Килиманджаро и Серенгети

(4) Italy >>> Benvenuti in Tanzania, la patria del monte Kilimanjaro e del Serengeti

(5) France >>> Bienvenue en Tanzanie, la maison du mont Kilimandjaro et du Serengeti.

(6) China >>> 欢迎来到坦桑尼亚乞力马扎罗山和塞伦盖蒂的家

Inakuwa hivyo kila taifa tunaweka ujumbe mmoja kwa lugha yake mama.

Jenga picha tu ikifika tarehe 9 watanzania wote wa Ufaransa, Italia, Ujeremani ama Urusi wakafanya hivyo, matokeo chanya yake yapoje?

KIJANA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. TOA MAONI NA USHAURI UTAKAOIJENGA NCHI YAKO ISONGE MBELE.
View attachment 967341

Soma pia>>> Shilingi mia tano ya sarafu ya sasa ilipaswa kufanana na shilingi ishirini ya zamani ili kuitofautisha na shilingi mia mbili ya sasa - JamiiForums
Mkuu, hilo ni wazo zuri. Hata hivyo, tayari limeishafanyiwa kazi ingawa tarehe husika sio hizo ni mwezi Septemba wa kila mwaka. Wizara ya Maliasili na Utalii imeaanzisha Tamasha linaoitwa ....Urithi Festival, Celebrating Our Heritage.......kuanzia mwaka 2018 na kuendelea mwezi wa tisa wote kutakuwa kunafanyika Matamasha nchi nzima, Watanzania wote popote walipo watahamasishwa kuvaa nguo za utamaduni wa Tanzania au zinazoitangaza Tanzania, kupika na kula vyakula vya Kitanzania n.k. Kwama ya kwanza limefanyika mwaka huu na lilizinduliwa Dodoma na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Baada ya hapo lilifanyika Zanzibar, Dar es Salaam, Arusha na Karatu. Kuanzia mwaka 2019 kila mkoa na Balozi zetu zitaadhimisha Tamasha hilo. Aidha, Utambulisho wa Tanzania/Branding Tanzania umebadilika sio.... the home of mount Kilimanjaro and Serengeti.... bali ni ......UNFORGETTABLE TANZANIA
 
Ok thanks for the info mkuu
 
*TUWAPIGIE KURA WASANII WETU MVP MUSIC AWARDS.* Hizi ni tuzo kubwa huko Nigeria. Turudishe heshima ya Tanzania.

Kwa kuwa wasanii wetu wengine wako wawili kwenye kipengele kimoja tupange tumpigie nani kura kila kipengele ili tusigawanye kura na tukashindwa kuchukua tuzo.

Vipengele:
*BEST MALE*
Hapa yupo Harmonize na Diamond. Tumpigie HARMONIZE kwa kuwa Diamond yupo kwenye vipengele vingine vingi.

*BEST FEMALE*
Tumpigie Maua Sama. Yupo peke yake toka Tz na East Africa

*BEST HIP HOP*
Hapa hakuna mbongo. Tumpe Khaligraph Jones mkali jirani yetu toka Kenya.

*BEST POP*
Tumpigie *Diamond Platnumz* yupo peke yake toka Tz na East Africa

*BEST COLLABORATION*
Hapa kuna JIBEBE na KATIKA. Tuipigie kura KATIKA YA NAVY KENZO kwa kuwa Diamond bado yupo kwenye vipengele vingine vingi. Isitoshe na kwenye KATIKA yumo

*DIGITAL ARTIST OF THE YEAR*
*Tumpigie Diamond Platnumz.* Hapa yupo peke yake kutoka Tanzania & East Africa

*BEST GROUP OF THE YEAR*

Tuwapigie Navy Kenzo

*SONG OF THE YEAR*
Hapa kuna *African Beauty ya Diamond*, na kuna *KWANGWARU* ya Harmonize na Diamond. Tuipigie *KWANGWARU* maana itapata kura nyingi zaidi toka nchi nyjngine za Africa kwa kuwa mpaka sasa ndo most viewed African music video kwa 2018. Na pia Diamond yumo

*BEST NEW ARTIST*
Tumpigie MBOSSO. Yupo peke yake kutoka Tz & East Africa

*LISTENERS' CHOICE*
Hapa ipo KATIKA ya Navy Kenzo na KWANGWARU ya Navy Kenzo. Tuipigie KATIKA ya Navy Kenzo maana KWANGWARU tushaipigia hapo juu

*AFRICAN PRODUCER OF THE YEAR*
Tumpigie NAHREEL yupo peke yake kutoka Tz & East Africa

*AFRICAN ARTIST OF THE YEAR*
Tumpigie *Diamond Platnumz* yupo peke yake kutoka Tz & East Africa

*JINSI YA KUPIGA KURA*
Click hii link
Soundcity MVP Awards Festival – Nominees are… Vote Now

Utakutana na vipengele vya tuzo zenyewe na majina ya wasanii husika (Nominees) gusa msanii unayempigia kura. Kura nu mara 1.

Tuache team zisizokuwa na maana. Tulete tuzo nyumbani.

*SAMBAZA KWA GROUPS ZAKO ZOTE*
 
Iwe tarehe 9 ama 26 yoyote ile inafaa ili mradi tu tunawatumia diasporas wetu kuitangaza vema Tanzania
Kwan hao diaspora wote walipelekwa huko na serikali au wengine walienda wenyewe kwa juhudi na gharama zao?

Kumbuka kuna wengine waliondoka TZ baada ya mambo kuwa magumu tena unakuta mtu alifanyiwa figisu figisu, sasa mtu kama huyu atapata wapi hamu ya kuvaa TShirt ya kuitangaza TZ!

Somo;
Wananchi wote tuishi kwa uzalendo kutoka moyoni.

Siyo wengine wanakula keki ya taifa, wakati wengine wanakula msoto, halafu mwisho wa siku tunahubiriana uzalendo!

Uzalendo siyo maneno, uzalendo ni vitendo vya haki na usawa kwa raia wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaotangaza huo Uzalendo na wezi.Mimi nimevunjika moyo na hii CAG shit.Uzalendo kwisha,yaani mimi nitangaze nchi na wengine wapige pesa zote.
 
Back
Top Bottom