Maaskofu Pentekoste waiomba Serikali kulifuta Kanisa la Askofu Gwajima

Huyu askofu Hajaisikilza hiyo audio vizuri !
Pili Huyo Gwajima ameyasemea kanisani kwake

TATU :
Alisema anaongea Na waumini wake kama Baba wa Familia .
Kama ambavyo sisi walutheri au Wakatoliki tunavyoweza tunvyosomewa waraka wa Kichungaji au wa Kanisa .
NNE Kwa maoni yangu sijaona alippochoaganisha zaidi ya kueleza anayoamini, !
NajiuliA wsle walokewepa kodi ya mkomtena
Hiyo sentensi ya mwisho ulitaka kusema nini...
 
Hiyo mbona simple wakilifuta kanisa lake anahama nchi watu wengi wanamuhitaji na huko atakoenda ataenda kuendeleza harakati mara mbili zaidi ya hapo na atakapo hakikisha nchi imekombolewa kutoka mikononi mwa ccm ataludi tanzania na atapokelewa kama shujaa.
Huyo Ikongo Mnafiki tu huyo.
Walifute kwa kosa gani?

Hawa viongozi wengine wa dini ni tatizo tu.
Kama shida ni Gwajima kusema aliyoyasema, Mbona naye kaja kuongea mambo ya siasa hapa. Dini na siasa havitenganishwi. Vyote ni mifumo iliyoweka katika maisha yetu. Gwajima hata kama asingekuwa anaongea na watu wake, bado kama mwananchi anahaki kukosoa anachokiona hakiendi sawa.
 
Hawa wachungaji wanajichanganya. Ninachoona wanataka kuanza kuleta uhasama baina ya waumini wa dhehebu la Kipentecoste na lile kanisa la Ufufuo wa Uzima. Wangenyamaza tu,kama hawayakubaliani nayo waache serikali idili naye.

Gwajima atakapotoka huko alipo lazima atawajibu hawa Wachungaji na uhasama utaanzia hapo. Lengo la makanisa yote ni kuwakomboa walio katika dhambi na kuwanyoosha njia inayopasa. Siyo kuwahamaki na kuwashtaki wenzao kwa kuwa wamekiuka misingi. Kama wangekuwa na busara wangesema Gwajima aonywe na wala siyo kanisa lake lifungiwe.

Sisi wote ni ndugu na tunachagulia pale panapotupendeza. Sasa kanisa likifungwa waumini wa Gwajima watasali wapi? Je,watakuwa wamefufahia hilo jambo?

Gwajima hakuchonganisha aliongea kama baba,wa waumini wake. Sijaona mahali popote alipochonganisha.

Hiyo ishu pia imefika polisi,pale ambapo polisi watatoa ripoti yao kwamba kweli Gwajima alichonganisha ndo wakati ambapo labda matamko haya yangetoka. Wasitafute kiki kwa Gwajima
 
Huyo Ikongo Mnafiki tu huyo.
Walifute kwa kosa gani?

Hawa viongozi wengine wa dini ni tatizo tu.
Kama shida ni Gwajima kusema aliyoyasema, Mbona naye kaja kuongea mambo ya siasa hapa. Dini na siasa havitenganishwi. Vyote ni mifumo iliyoweka katika maisha yetu. Gwajima hata kama asingekuwa anaongea na watu wake, bado kama mwananchi anahaki kukosoa anachokiona hakiendi sawa.
Kweli huyo ikongo nimemuona ni mpuuzi.
 
View attachment 357344

Ushirika wa wachungaji wa Kanisa la Kipentekoste Tanzania (PPFT)umeiomba serikali ifute usajili wa Kanisa la Ufufuo wa uzima la Askofu Josephat Gwajima kwa kukiuka maadili ya kanisa kwa kutoa kauli za uchochezi na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa ushirika wa wachungaji hao Askofu Pius Ikongo mwenye makao yake katika Halmashauri ya wilaya ya Mwanga amesema,kauli hizo zinaweza kubadili fikra za wananchi na kuzaa chuki dhidi ya serikali yao na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Askofu Ikongo ametoa tamko hilo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa kitendo kilichofanywa na Askofu Gwajima kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani wote waliopo ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti huyo wa PPFT amesema, kosa kubwa ambalo limewaumiza wachungaji wa Kipentekoste ni kitendo cha Askofu Gwajima kutumia Kanisa kama jukwa la kisiasa kwa kuleta uchonganishi kati ya serikali ya awamu ya nne na iliyopo madarakani.

Askofu huyo aliyejinasibu kuongea kwa niaba ya wenzake wa Pentekoste ameiomba Serikali kupitia Waizara ya Mambo ya ndani,kulifungia Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Gwajima haraka iwezekanavyo ili kuokoa amani ya nchi na wananchi wake
Hilo ni jina la kanisa lake au? Hicho kikao kilikaa lini na wapi? Nani maaskofu walihudhuria? Kama hakuna kikao cha namna hii, huyo Ikongo atakuwa jipu.
 
1.jpg

Ushirika wa wachungaji wa Kanisa la Kipentekoste Tanzania (PPFT)umeiomba serikali ifute usajili wa Kanisa la Ufufuo wa uzima la Askofu Josephat Gwajima kwa kukiuka maadili ya kanisa kwa kutoa kauli za uchochezi na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa ushirika wa wachungaji hao Askofu Pius Ikongo mwenye makao yake katika Halmashauri ya wilaya ya Mwanga amesema,kauli hizo zinaweza kubadili fikra za wananchi na kuzaa chuki dhidi ya serikali yao na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Askofu Ikongo ametoa tamko hilo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa kitendo kilichofanywa na Askofu Gwajima kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani wote waliopo ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti huyo wa ppft amesema, kosa kubwa ambalo limewaumiza wachungaji wa Kipentekoste ni kitendo cha Askofu Gwajima kutumia Kanisa kama jukwaa la kisiasa kwa kuleta uchonganishi kati ya serikali ya awamu ya nne na iliyopo madarakani.
 
Huyu askofu Hajaisikilza hiyo audio vizuri !
Pili Huyo Gwajima ameyasemea kanisani kwake

TATU :
Alisema anaongea Na waumini wake kama Baba wa Familia .
Kama ambavyo sisi walutheri au Wakatoliki tunavyoweza tunvyosomewa waraka wa Kichungaji au wa Kanisa .
NNE Kwa maoni yangu sijaona alippochoaganisha zaidi ya kueleza anayoamini, !
NajiuliA wsle walokewepa kodi ya mkomtena

Mkuu mchango wako unastahili editing usomeke vyema!!!!
 
View attachment 357344

Ushirika wa wachungaji wa Kanisa la Kipentekoste Tanzania (PPFT)umeiomba serikali ifute usajili wa Kanisa la Ufufuo wa uzima la Askofu Josephat Gwajima kwa kukiuka maadili ya kanisa kwa kutoa kauli za uchochezi na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa ushirika wa wachungaji hao Askofu Pius Ikongo mwenye makao yake katika Halmashauri ya wilaya ya Mwanga amesema,kauli hizo zinaweza kubadili fikra za wananchi na kuzaa chuki dhidi ya serikali yao na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Askofu Ikongo ametoa tamko hilo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa kitendo kilichofanywa na Askofu Gwajima kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani wote waliopo ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti huyo wa PPFT amesema, kosa kubwa ambalo limewaumiza wachungaji wa Kipentekoste ni kitendo cha Askofu Gwajima kutumia Kanisa kama jukwa la kisiasa kwa kuleta uchonganishi kati ya serikali ya awamu ya nne na iliyopo madarakani.

Askofu huyo aliyejinasibu kuongea kwa niaba ya wenzake wa Pentekoste ameiomba Serikali kupitia Waizara ya Mambo ya ndani,kulifungia Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Gwajima haraka iwezekanavyo ili kuokoa amani ya nchi na wananchi wake
Huyo askofu anaakili finyu, kwa hiyo Askofu wa romani catholic au shee akisema kitu akiwa kanisani au shee mskitini basi kanisa catholic au uislamu wote ufutwe? kwa nini asichukuliwe sheria yeye kama yeye aliye sema? Sababu hapo ametumia uhuru wake wa kutoa maoni, ila sehemu aliyo tumia si sahihi
 
ninashida moja kwa watumishi fulanifulani(hasa hawa wa kukosoana) siku hizi ni km ujasiriamali umehamia makanisani!! jamani hubirini watu waache wizi,uzinzi,ufisadi, na maovu mengi tu yote ambayo Biblia inakataza watu waende mbinguni. haya mabo ya kushambuliana hadharani... duh!!
 
Gwajima hajawasemea wapentekoste wote

Tena yeye alisisitiza anajisemea yeye mwenyewe na anaamini waumini wa kanisa lake watamwunga mkono
 
Gwajima kubwa lao!, ha ha haaaah!. Yetu macho na masikio tu, vita vyenu huko huko sisi nchini kwetu hatunaga mambo hayo. Hata kama mtu anauwawa mbele ya macho yako bado hatuna hasira za kuvurugana wao kwa wao. Ushindwe kwa Jina la Yesu ewe pepo!
 
Najiuliza kauli za Askofu Gwajima zina nini nyuma yake. mbona haeleweki? ni ndege au ni mnyama?
alimponda Kard. Pengo na kumsema Rais mstaafu JK na akatangaza wazi kumuunga mkono Lowassa na akasema Lowassa ni msafi. alihimiza achaguliwe Lowassa na si Magufuli na CCM yake kwani alidai CCM ni chafu. leo aliyemuona hafai na chama chake yaani JPM anadai yuko vzr, kulikoni? hakumjua JPM kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana? mbona hana msimamo kiasi cha kutoa kauli za hatari tena za kichochezi ndani ya CCM? ni KUJIKOMBA KWA JPM? AU KUTAFUTA UMAARUFU 'KICK'? AU NI UCHUNGU ALIONAO KWA TAIFA?
 
Huyu Ikongo naye kakurupuka.

Anatafuta kiki tu kwa mgongo wa Gwajima.

Si atafute namna ya kujitangaza!!
 
Back
Top Bottom