Maandamano ya vyama vya upinzani ndio mafanikio ya kipekee kabisa ya Awamu ya 6 ya Rais Samia

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
9,805
20,689
Sikumbuki ni utawala wa awamu ya ngapi hasa tuliona polisi wakiyalinda maandamano ya vyama vya upinzani,hata nchi jirani ya Kenya maandamano Yao yamejaa vurugu mauaji na damu kumwagika,hata awamu ya nne ilioulea upinzani tunaouona hadi Leo haikuruhusu maandamano ya amani,Bado nakumbuka mauaji ya Arusha kipindi kile cha vurugu za chadema na vijana was ccm.

Ni dhahiri kwamba jambo pekee nitakalolikumbuka na kuwasimulia wajukuu katika uzee wangu ni kuona vyama vya upinzani vikiandamana bila uoga vikilindwa na polisi hata ikafikia hatua askari magereza wakabeba bango la kulaumu kikotoo!

Kwa Hilo pekee ndilo linalomtofautisha Raise samiah na Marais wengine wa awamu iliyopita,hata mikutano ya nchi nzima ya upinzani imeonyesha ni namna Gani Kuna ukomavu was kiuongozi wa huyu mama!!

Dalili hizi zinaonyesha uelekeo mpya was Tanzania mpya ijayo,kwamba upinzani sio uadui Bali ni sehem ya taasisi na kusukuma agenda za maendeleo katika nchi yetu!

Nitumie jukwaa hili kuwaasa vyama vya upinzani viendeleze siasa za kindugu kistaarabu bila kuleta chuki na migogoro kwenye jamii yetu,wasipofanya hivyo hawatotofautiana na CCM ya awamu zilizopita!!

Niiombe kamati kuu ya chama changu ccm kufanyia kazi changamoto za kikatiba na kichaguzi zinazo liliwa na wapinzani katika maandamano yao!!


Nimatumaini yangu kwamba kuelekea uchaguzi mkuu changamoto za sintofahamu za uchaguzi.zitakua zimeisha Ili tufanye siasa safi Kwa mstakabali wa Tanzania ijayo!!



Mungu ibariki Tanzania,Mungu vibariki vyama vya siasa vidumishe undugu!!

Tuendelee kukemea wizi,rushwa na ubadhirifu unaoripotiwa Kila Kona nchini na hatua za kisheria zifuatwe Kwa wahusika!
 
Mimi ni Tomaso mpaka tuone haki na huru kwenye chaguzi hapo nitasema apewe award ya Ibrahim
 
Back
Top Bottom