Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,805
- 13,574
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika Septemba 23 katika jiji kuu la kibiashara, Dar es Salaam. Marufuku hiyo imetolewa kwa lengo la kudumisha amani na usalama wa wananchi.
Misime aliongeza kwamba hatua hii imechukuliwa kwa sababu baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakipanga mikakati ya kuchochea vurugu nchini, hali ambayo inaleta hatari kwa amani ya nchi. Alisema kuwa mara kadhaa serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini walipo wanachama waliodaiwa kupotea, lakini baadhi ya watu wanaendelea kutoa mipango inayolenga kuharibu amani.
Pia Soma:
~ Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea
~ Kuelekea 2025 - Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'
"Kwanini wanataka kututoa kwenye reli hatua za kiupelelezi zinazoendelea baada ya Rais Samia Suluhu kuagiza kufanyika kwa uchunguzi, mara kadhaa viongozi na wafuasi wamekuwa wakipanga na kuratibu mikakati mbalimbali na kutoa mipango yenye lengo la leta vurugu nchini ili kuharibu amani ya nchi yetu kwasababu zao wenyewe, kutokana na taarifa hiyo jeshi la polisi nchini limepiga marufuku kuacha kuendelea kuhamasisha kujihusisha katika uhalifu huo"