Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,170
- 5,528
DIWANI wa Kata ya Langai, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara, Jackson Leskar Sipitieck (Mugabe), amejitolea kumlipa Sh. 100,000 mwalimu wa Shule ya Msingi Langai ambaye anafundisha kwa kujitolea.
Pia diwani huyo maarufu kama Mugabe, ametoa trekta lake na kuwalimia ekari 10 kwenye shamba la shule, ili wanafunzi wa Shule ya Msingi Langai wapate kula chakula cha mchana shuleni.
Sipitieck akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Shule ya Msingi Langai, amesema analipa Sh. 100,000 kwa mwalimu huyo, lengo likiwa kumwezesha mwalimu huyo anayejitolea kufundisha shuleni hapo.
"Baada ya kusikia changamoto ya mwalimu ambaye hajaajiriwa na serikali anayejitolea kufundisha watoto wetu, nikaona niwezeshe hilo ili kumpa motisha ya kufundisha zaidi," amesema Sipitieck.