Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Ingekuwa si uhuni wa Mtatiro na Maalim Seif hakika Lipumba angerudi katika kiti chake na maisha ya CUF yangeenda bila zengwe!
Lakini sasa chombo kishagonga mwamba, na Lipumba kajeruhiwa, na kwakuwa jambo lilofanywa ni uhuni kwavyovyote vile Lipumba atarudi katika kiti chake, ni suala la muda tu.
Jeraha alilopata Lipumba, namshauri akirudi katika kiti, Maalim Seif, Mtatiro na genge lao wavuliwe uanachama na wafukuzwe CUF.
Kwakuwa mamlaka ya nidhamu ya katibu mkuu ni mkutano mkuu(kama sikosei) na kwakuwa mkutano mkuu wameumizwa na uhuni wa Seif, na kwakuwa kuna sahihi zaidi ya 400 za wajumbe wa mkutano mkuu walio umizwa na uhuni huo, nina hakika Maalim Seif hana chaguo, aidha ajiunge CHADEMA au aunde chama chake.
CHADEMA hawana nguvu Zanzibar, wanachochea kuni na wanampa kichwa Maalim Seif ili atimuliwe CUF ajiunge na chama chao ili CHADEMA ipete Zanzibar kwa nyota ya Maalim Seif. Ndio maana binafsi sishangai kwa makada wa CHADEMA kujaza masusu juu ya kadhia hii huku wakiegemea upande wa Wazanzibari(Maalim)
Nimelala, naota tu, jogoo akiweka mnistue kama sitamsikia.
Njano5
0622845394.