mgogoone
JF-Expert Member
- Dec 28, 2015
- 2,900
- 2,097
Punguza jazba anti maana naliona povu limekujaa.Nafikiri kabla ya kutoa hukumu,ungetusaidia kutambua katiba ya Zanzibar inasemaje kuhusu viongozi wakuu wa nchi.Hata kama humpendi,Maalim Seif ni Kiongozi aliyemaliza muda wake na kwa wadhifa wake ana haki ya kuhudumiwa na serikali bila kujali ni serikali gani iliyopo madarakani.
Kwa katiba yetu huku bara,hata shetani aje aitawale 'danganyika'bado shetani huyo na serikali yake atalazimika kuwahudumia viongozi wakuu wastaafu wote.Au hujuwi kuwa hata kama UKAWA ingeingia madarakani bado ingeendelea kuwahudumia viongozi wote wastaafu wa serikali ya Chama Cha Majipu (CCM)?
Maalim Seif kuhudumiwa na serikali ya kibaguzi ya Zanzibar si suala la hiari,ni takwa la kikatiba.