Maalim amewasaliti wana mapinduzi

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,981
45,903
Kitendo chake cha kukaa hotelini na kutumia mamilioni kimetosha kabisa kufisha morale ya wapiganaji.

Kanuni ya kwanza ya mwanamapinduzi yoyote ni unyenyekevu na utu.

Kuishi kwa starehe ni kinyume cha imani za wanamapinduzi wote ulimwenguni.

Hakuna popote katika historia ya dunia mwanamapinduzi kufuja rasilimali.

Wote kuanzia Fidel Castro, Che Guevara, na wengineo walijitenga na anasa.

Sidhani kama ilikua sahihi kwake kuishi hotelini.

Je. hakuna nyumba za serikali?

Hakuona umuhimu wa kusave fedha ili ziboreshe huduma kwa wapiga kura wake.

Amenifisha moyo sana...

Ametoa somo baya kwa wanasiasa wa vizazi vijavyo...

Kwamba ni sawa tu kutumia fedha za serikali hovyo maana hazina mwenyewe.

Maalim you owe us an explanation and an apology.
 
nakuunga mkono kamanda. ulipo tupooo. na sio hilo tu. tunawataka pia mafisadi waliohamia ukawa waondoke haraka. na wale wote waliouza uhuru wao kwa kitu pesa basi wajipime waone kama wanafaa kuendelea kuwepo kwwnye vyama hivi
 
Aaaaaah we kijana Maalim sio mwanamapinduzi ni mwanasiasa,mwanamapinduzi ni Shein aliyepindua Katiba na matokeo ya October 25,wakishirikiana na John na jakayaa kiguu na njia
 
Umenena vyema Comred
Na wapo wengi wanaojiita wanamapinduzi wa aina ya Maalim na hasa cream ya UKAWA ni hivyo hivyo tu....
 
Maalim Kakaa Hotelini huku pesa ikilipwa na serikali, kwa nini hakukaa kwake hapa Dar es salaam, Kwa nini akubali kulipiwa pesa na serikali ile ile anayosema imemdhulumu ushindi?

MAALIM ALISHACOMPROMISE
 
Kabla hujamlaumu kwa kukaa hotelin mlaumu yule aliyeuza nyumba za uma koz xabab kubwa n yy kutopewa nyumba huku bara kama sheria inavotaka
 
Maalim ni mnafiki na fisadi tu kama wanafiki na mafisadi wengine wa UKAWA..angekuwa anaipenda Zanzibar na wazanzibar angeenda kuugulia huko huko kwao unguja, Si Maalim huyu huyu anaepigaga vita muungano???MNAFIKI TU huyu.
 
HIYO NI SHIDA BADALA YA KUFIKIRIA MIAKA KARIBU AROBAINI YA MUUNGANO HAKUNA NYUMBA YA VIONGOZI SMZ MNAMJADILI MAALIM ULIZA" WAPI NYUMBA YA KUFIKIA VONGOZI WA SMZ"?UJUWE HUO MFUMO WA CHAMA CHETU TWAWALA
 
N
Ni makosa kumlinganisha maalim seif na wanamapinduzi kama kina che guevara na fidel castro. Maalim seif sio mpigania uhuru au demokrasia. Yeye ni mpigania madaraka.
 
Ukiwa unafiki usiwe msahaulifu.Mgombea madaraka ni Shein aliyefuta uchaguzi halali na kutumia mabilioni ya shilingi kufanya uchaguzi huu fake ili mradi awe Mtawala.
 
Maalim kawaingiza mikenge wazanzibar ila kwa vile hawaoni na hawasikii waache wakae huko huko mikengeni..Shein piga kazi mweee!! ngenge nini?
 
Maalim kawaingiza mikenge wazanzibar ila kwa vile hawaoni na hawasikii waache wakae huko huko mikengeni..Shein piga kazi mweee!! ngenge nini?
umenena sawa mkuu; haya ni maneno kwa ajili ya waelewa wachache na sio kila mtu.
 
Alikua anakula za mwisho mwisho, alisha jua hana chake tena akaona bora ale bata tu.
 
nakuunga mkono kamanda. ulipo tupooo. na sio hilo tu. tunawataka pia mafisadi waliohamia ukawa waondoke haraka. na wale wote waliouza uhuru wao kwa kitu pesa basi wajipime waone kama wanafaa kuendelea kuwepo kwwnye vyama hivi
Lini na wapi Seif amejiita mwanamapinduzi? Huwajui wanaojiita Chama cha mapinduzi ? Wanaotoa kauli za mapinduzi daima? Wanaosema serikali haitolewi kwa vikaratasi. Umejiuliza nafasi yake katika serikali ya umoja wa kitaifa?
Kuna mawaziri mmojawapo amekaa hotel ya New African hotel kwa muda wa miaka saba hamjawaona?
Nyumba za serikali zimeuzwa tena zikishikiwa kidedea na huyu huyu mtumbua majipu leo mmemuuliza kwa nini aligawa nyumba za serikali kwa jamaa zake hadi mahakama?
Ukiwa CCM lazima uwe mpotoshaji pia
 
Ma-ccm yana shida kweli kweli, mwenye akili zake timamu hawezi kuwa sisiiem hata iweje!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…