Nyagei
JF-Expert Member
- Jul 7, 2015
- 13,201
- 44,601
AminiaNiaje wana ?
Jiji la Dar es salaam ndio jiji la ukweli na lenye mbwembwe kwa hapa Tanzania .....Pamoja na sifa zote lakini lina vijimambo vyake bwana !!!
1/ Uchafu ndio mwake!!
Dsm ndio jiji chafu zaidi nchini Tanzania..kuanzia sehemu za Uswahilibi hadi katikati ya jiji ni mwendo wa uchafu tu..Mtuache na uchafu wetu bhana!!!!
2/Vijana wa mission town.
Vijana wengi hawana kazi za kueleweka..wanaamka saa 2 asubuhi wanapiga mswaki kisha wanapanga dili zao za kimagumashi..usishangae mtu hana kazi mjini lakini anamiliki mkoko!!!
3/Chai hunyweka kuanzia saa 4 asubuhi
Pamoja na joto Kali la bongo idadi kubwa ya watu has a uswaz hunywa chai mida ya saa 4,5&6 ....Usishangae tunaita kutafuta faulo!!!
4/Foleni kila sehemu
Kila mahali watu kibao..barabarani watu/magari kibao,msikitini/kanisani watu kibwena,benki nako watu kibao..Kila sehemu watu kibao kasoro vituo vya kupima HIV/AIDS tu!!
5/wali ndondo kama fasheni vile!!
Hawa ndio wana DSM bwana..usiku idadi kubwa ya watu wali maharage utafikiri wamesaini nayo mkataba!!! Na butchery ni vinara wa kununua 1/4 kilo....
6/ Madadapoa wa kumwaga !!
Dsm kumejaa madadapoa kila sehemu kuanzia uswahilini kama vile Buguruni, Mwananyamala, Temwke, Manzese uwanja wa fisi na sehemu za kiahua kwa mfanoCorner bar sinza na Ohio street Posta..Ni chaguo lako tu mwana!!;
7/ Hela inapatikana kiurahisi...
Waliosema mjini akili, nguvu kijijini hawakukosea!!! Mjini kupata pesa sio ishu, ishu ni jinsi ya kuitumia...kila kitu kinauzwa hadi mbilimbi !!! Hata yaje mafuriko haturudi kijijini.....
8/Kila mtaa kibanda cha chipsi
Joto City chipsi mayai zinashobokewa na kila MTU......usiniulize kwa nini Makonda anawasaka mashoga !!
9/Usiku mbu, mchana nzi, sisimizi wapambe!!
Kutokana na hali ya hewa ya joto kali pamoja na tabia ya uchafu jiji la Dsm usiku ni full mbu, mchana nzi ndio bosi & sisimizi ndio wapambe !!!
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Rais wa Masela
The Bitoz