Maadhimisho ya miaka 60 ya muungano na idadi ndogo ya mahudhurio uwanjani, nini tatizo?

Huyaa Dr

JF-Expert Member
Jan 12, 2023
312
874
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano,idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe,je ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini? Maoni yenu wakuu.
na ukizingatia mwaka huu wamelifanyia sana ma-promotion na maombi ya kuzuga kila mahali eti kuliombea taifa na raisi,waache watu wameshachoka na huo muungano wa upande moja kuonewa
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano,idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe,je ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini? Maoni yenu wakuu.
Soon watatangaza posho watajaa
 
Hali halisi leo tarehe 26 April 2024 kutoka uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Tanzania katika Maadhimisho ya miaka 60 ya toka Muungano wa kidugu kuasisiwa kisheria baina ya nchi mbili za kiafrika za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu Wa Zanzibar

1714120761688.png


Tukumbuke kuwa mahusiano ya mataifa haya mawili yalianza kabla ya mwaka 1964 ambapo kwa miongo mingi raia wa pande hizo mbili walishirikiana kiuchumi, kielimu kidini na burudani bila vikwazo vyovyote.

Watu kutoka Tanganyika walikwenda soma katika skuli za elimu ya juu enzi hizo zinapatikana Zanzibar tu, kutoka sehemu mbalimbali za Tanganyika mfano mkoa wa Tanga uliokuwa na shule kongwe za mwanzo lakini hazikuwa na madarasa ya juu hivyo baadhi yao kulazimika kuvuka na kwenda Zanzibar kumalizia elimu zao za sekondari.

Upande wa biashara, Zanzibar ilikuwa kitovu cha majahazi kuleta mali kutoka bara Arabuni na India pamoja na ulaya hivyo wafanyabiashara wa kutoka Tanganyika walimiminika kutafuta bidhaa hizo Zanzibar.

Zao la karafuu na mbata (nazi)wakati wa msimu wa mavuno mashambani Pemba na Zanzibar yalihitaji mikono mingi ya wavunaji, wakwezi na wafua nazi na kulazimu kupata mikono hiyo kutoka Tanganyika ya usukumani na unyamwezi hivyo waTanganyika hao kupata ajira za muda za ujira wa kukimu maisha yao na familia.

Mahusiano mengi kama Zanzibar kuwa daraja la kupeleka imani ngeni za kuja kwa majahazi na merikebu, kwanza zilitupa nanga Zanzibar kuongea na wajuvi wa safari za ndani ndani Tanganyika watafikaje. Ndipo ndugu zetu wa Zanzibar wakaaaongoza maalimu na baadaye wamisionari kueneza imani za dini.

Mambo ni mengi na miaka mingi baadaye wanasiasa wakaona muingiliano huu wa kiuchumi, kielimu na kijamii tayari umeweka kila kitu sawa hivyo ni heri kufanya mambo kisheria na hivyo kusiliba muungano huu usio rasmi unaotambulika kwa kuutia ndani ya karatasi ya mkataba kuwa Muungano rasmi mwaka 1964.

Hivyo Julius Nyerere na mwenzie Mzee Abeid Karume wakaona wafanye mambo kiusasa na Muungano wa wananchi hawa wa karne kibao kuwekwa katika utambulisho wa Muungano kikatiba kuhitimisha walichoanzisha wananchi wenyewe kwa miaka mingi.

 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano,idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe,je ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini? Maoni yenu wakuu.
Kuna mambo mawili;
Mvua
Hisia za watu juu ya Muungano

Mvua: Watu hawana uhakika wa kula yao ya leo sababu ya hizo mvua zenu, bado unawataka wahudhurie maadhimisho hayo? Wapite kwenye barabara gani wakati miundombinu imeharibika, mitaa imejaa maji, ajali zimeongezeka, nyumba zinaelea kwenye maji na mvua zinaendelea kunyesha?
Nani aende uwankani kunyeshewa na mvua mwanzo mwisho. Timu za mpira zenyewe pia zina struggle kujaza viwanja sasa hivi.
Lile fungu ambalo CCM hupewa ili kukusanya watu na kuwasafirisha kwenda kwenye matukio kama hayo, safari hii limeliwa

Hisia za watu
Linaweza likawa ni jibu la watu juu ya Muungano. Wameamua kuukataa na kutoutambua kwa vitendo. Muungano hauna tija kwa wananchi zaidi ya kuwasababishia waishi na wenzao kwa kusimangwa kwa kila kitu utadhani labda wao ni wakinbizi au wakoloni tu.
 
Nature imekataa watu wasiende,licha ya ugeni mzito wa marais toka nje na promo njingi katika media ,all in all tuimbee nchi yetu na kuipenda.
 
Mwenzio anaenda kuadhimisha akiwa amekaa ndani ya v-8 mafuta kalipiwa chai ya ofisi n.k

Wewe ujinyenyue kutoka ulipo kwa nauli yako mgukoni and you call that uzalendo?

Nononono!!
Halafu wewe unapanda mwendokasi, unashushwa njiani kutokana na barabara kujaa maji, unaogelea kituo kimoja hadi kingine ili ukakae unyeshewe kuangalia wanaosherehekea wakitokea kwenye magari ya kifahari.
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano,idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe,je ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini? Maoni yenu wakuu.
Mvua ina nyesha mji mzima barabara zinazo elekea uko na mjini zime fungwa una tegemea watu wakajazane uwanjani wakati local channel zote ziko MBASHARA
 
Mleta uzi sometimes punguza kuwa na akili finyu ina maana huoni mvua tena zimenyesha mfululizo siku ya 4 hii?

Sio uwanjani tu hata makanisani sikuhizi watu ni wachache sababu ya mvua.
 
Back
Top Bottom