M23 yaanzisha mapigano tena huko Walikale

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Jan 31, 2025
398
671
Baada ya serikali ya Doha, kuanzisha njia ya upatanishi kati ya kundi la AFC/M23 na serikali ya DRC, serikali ya Qatar na USA waliiomba M23 kurudi nyuma na kuachia eneo la Walikale, ambalo lina Mgodi mkubwa wa Serikali ya Canada.

M23 ilitii agizo hilo, na baada ya kuondoa wanajeshi wake, serikali ya Congo iliwarudisha majeshi yake, na wanaowasaidia,wakiwemo FDLR na Wazalendo.

Huko Doha, M23, iliiomba serikali ya DRC kwanza kuachia watu wake wapatao 700 waliofungwa na serikali.

Raisi wa DRC, ametupilia mbali ombi hilo, na kusababisha pande zote kurudi nchini bila muafaka.

Baada ya kuombwa kuondoa wanajeshi wake Walikale, M23 ikatii, Mgodi wa AlfaMining uliendelea na shughuli zake, baada ya M23 kuondoka.

Leo hii, baada ya makubaliano kutofikiwa, M23 imeanzisha tena vita kuiondoa tena serikali ya DRC katika eneo hilo la Walikale.

Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya matajiri na viongozi, wameanza kujiunga rasimi na M23.

Siku za nyuma, rais Tshisekedi amekuwa akiwatuhumu badhi ya watumishi wa serikali kuwa ni wasaliti, kutokana na kuwa kila serikali ilichokuwa ikipanga, M23 ilikuwa ikipata taarifa mapema, na kuzitangaza kabla ya serikali kufanya ilichokipanga.
 
Safari hii wanangu wa m23 twenden mpk uvira kabisa hakuna kuweka bunduki chini
Uvira ni njia ya kuwaondoa warundi tu kwanza. Mpango ni Kisangani, Maniema na katanga. Kwanza zile sehemu zenye kipato kikubwa kwa serikali. Baada ya hapo kuna maeneo mengine serikali itakuwa inajiondoa yenyewe, na njia ni mpaka Kinshasa.
 
Hao jamaa inaonyesha ina askari imara na vifaa vya kutosha,haina mabishoo katika jeshi lao....maana safari hii wamejipanga sana,nchi zote wameshindwa kuwadhibiti,nasikia Kabila pia anawapa sapoti.
 
Tshekedi hawamtaki anagombana hata na Watangulizi wake anagombana na watu wa Serikali mwisho yatamkuta ya Kuku wa Zabanga
 
Sasa itakuwaje ikiwa inasemekana kabila kaenda Goma kinyemela pia aliona na Elon Mask? Hii circle ya hii vita ilivokaa na inavoendelea kuna watu wakija kushtuka watapata heart attack. Tshekedi nimeona bank ya Swiss wanadai kahifadhi $8 billion wame freeze account.
 
Siasa hainaga rafiki, siasa ina faida. Hapa M23 ina maeneo safi na salama, waliokuwa wakimbemenda Thsisekedi, washaweka dau kwa M23.
 
Baada ya serikali ya Doha, kuanzisha njia ya upatanishi kati ya kundi la AFC/M23 na serikali ya DRC, serikali ya Qatar na USA waliiomba M23 kurudi nyuma na kuachia eneo la Walikale, ambalo lina Mgodi mkubwa wa Serikali ya Canada.

M23 ilitii agizo hilo, na baada ya kuondoa wanajeshi wake, serikali ya Congo iliwarudisha majeshi yake, na wanaowasaidia,wakiwemo FDLR na Wazalendo.

Huko Doha, M23, iliiomba serikali ya DRC kwanza kuachia watu wake wapatao 700 waliofungwa na serikali.

Raisi wa DRC, ametupilia mbali ombi hilo, na kusababisha pande zote kurudi nchini bila muafaka.

Baada ya kuombwa kuondoa wanajeshi wake Walikale, M23 ikatii, Mgodi wa AlfaMining uliendelea na shughuli zake, baada ya M23 kuondoka.

Leo hii, baada ya makubaliano kutofikiwa, M23 imeanzisha tena vita kuiondoa tena serikali ya DRC katika eneo hilo la Walikale.

Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya matajiri na viongozi, wameanza kujiunga rasimi na M23.

Siku za nyuma, rais Tshisekedi amekuwa akiwatuhumu badhi ya watumishi wa serikali kuwa ni wasaliti, kutokana na kuwa kila serikali ilichokuwa ikipanga, M23 ilikuwa ikipata taarifa mapema, na kuzitangaza kabla ya serikali kufanya ilichokipanga.
Kagame anaiona Drc mashariki kama himaya yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom