MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 398
- 670
Baada ya serikali ya Doha, kuanzisha njia ya upatanishi kati ya kundi la AFC/M23 na serikali ya DRC, serikali ya Qatar na USA waliiomba M23 kurudi nyuma na kuachia eneo la Walikale, ambalo lina Mgodi mkubwa wa Serikali ya Canada.
M23 ilitii agizo hilo, na baada ya kuondoa wanajeshi wake, serikali ya Congo iliwarudisha majeshi yake, na wanaowasaidia,wakiwemo FDLR na Wazalendo.
Huko Doha, M23, iliiomba serikali ya DRC kwanza kuachia watu wake wapatao 700 waliofungwa na serikali.
Raisi wa DRC, ametupilia mbali ombi hilo, na kusababisha pande zote kurudi nchini bila muafaka.
Baada ya kuombwa kuondoa wanajeshi wake Walikale, M23 ikatii, Mgodi wa AlfaMining uliendelea na shughuli zake, baada ya M23 kuondoka.
Leo hii, baada ya makubaliano kutofikiwa, M23 imeanzisha tena vita kuiondoa tena serikali ya DRC katika eneo hilo la Walikale.
Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya matajiri na viongozi, wameanza kujiunga rasimi na M23.
Siku za nyuma, rais Tshisekedi amekuwa akiwatuhumu badhi ya watumishi wa serikali kuwa ni wasaliti, kutokana na kuwa kila serikali ilichokuwa ikipanga, M23 ilikuwa ikipata taarifa mapema, na kuzitangaza kabla ya serikali kufanya ilichokipanga.