Mateso
JF-Expert Member
- Aug 6, 2008
- 259
- 19
Waungwana juhudi zinazofanyanywa na serikali yetu ni za kuungwana mkono. Ila ningependa kumshauri Mh. Lukuvi asiwe anachukua maamuzi ya pupa ya kunyang'anya watu ardhi tuakaja kusumbuana mahakamani kwa muda mrefu. Pili hakuna mtu aliyeko juu ya sharia. Kama kuna mtu aliagizwa na kiongozi wake wa ngazi za juu kufanya kazi ambayo alijua ni kinyume cha sharia na yeye akaifanya akijua kuwa ni kosa atakuwa mpumbavu na atastahili kubeba mzigo wake mwenyewe. Wewe kama ni msaidizi na mshauri wa kiongozi akakuambia ufanye jambo haramu na wewe ukaacha kumshauri ajue na kukubali kuwa hilo jambo ni haramu basi wewe utakuwa haramu na hustahili kuwepo kwenye jamii.Hapo umenena kinachostahili. Kwa walio hai wakamatwe na wapelekwe mbele ya sheria na wakishindwa kesi mali walizochuma kifisadi zitaifishwe. Kwa waliofariki mali zao zinaeleweka zikamatwe na kutaifishwa. Suala la kusema tuliambiwa na fulani halina uzito wamwite mahakamani kama atawatetea sawa ila ni jambo ninaloelewa ni ngumu.Raisi magufuli endeleza kasi yako wala usitishwe na yeyote walio nyuma yako ni wengi zaidi.