Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo,ametoa ripoti na kusema Jairo anarudishwa kazini kuanzia kesho.
===========
UPDATES:
Luhanjo anasema tuhuma zilikuwa za uwongo
Anasema taasisi za Wizara hazizidi 7 na si zaidi ya 20 kama ilivyodaiwa
Taasisi nne tu ndizo zilizochangia na zilichanga karibu TZS 500mil na si zaidi ya 1bil kama ilivyodaiwa
Pesa zilichangwa ili kuwawezesha watendaji watakaoenda kwenye bunge la bajeti
REA walichangia 50mil
TANESCO walichangia 40mil
EWURA waliombwa 40mil lkn hawakutoa, walichangia gharama za chakula na malazi kwa watendaji wa Wizara
Idara ya Uhasibu ya Wizara ilitoa 150mil
Idara ya mipango ya Wizara ilitoa 278mil
More updates to follow
Hapo kwenye msimbazi, hebu atuambie walilipia kwa kutumia nini? Tunataka tujue gharama za chakula na malazi ni kiasi gani? Hawa wakisafiri huwa wanapewa Imperest, sasa wanalipwa vipi tena na EWURA.