zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,273
- 31,170
Habari za asubuhi wanajukwaa, kumekuwepo na sifa kedekede kwa Mbunge Luhaga Mpina kwa kinachoitwa uzalendo na uchapakazi. Lakini kinyume na wengi humu, sijawahi kukubali aina za siasa za Mpina sababu ni opportunist tu na hana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko.
Hapa chini nimeweka video Mpina akilalamika kuhusu Ufisadi uliopo Wizara ya Nishati na Tanesco lakini cha ajabu lawama zote anamtupia Makamba na Maharage Chande licha ya kwamba kuna waziri mwingine kwa zaidi ya mwaka sasa.
Mfano analalamikia pesa za CSR kutotolewa na huyu mjenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere? Anasema kuna ufisadi, kama waziri ni Biteko kwanini lawama azipeleke kwa January na Chande ilihali hawana mamlaka juu ya hayo tena?
2. Ananalamika hatujalipwa pesa za IPTL zaidi ya Billion 200, ila bado anamlaumu Makamba na chande kwa kutolipwa pesa hizo. Je kwanini asimlaumu Biteko ambaye ni waziri kwa sasa?
3. Analaumu kwa Serikali kutolipwa pesa za ucheleweshaji wa mradi wa Bwawa la Nyerere. Cha ajabu anamlaumu Makamba kwa kutosimamia pesa hizo zilipwe, je ni kwanini asimlaumu Biteko ambaye ndiye waziri mwenye dhamani ya kudai pesa hizo? Is it fair?
Mambo ni mengi anayaolalamikia kwa sasa ila nilichogundua Mpina anaongozwa na chuki tu na ukabila ndio maana anakwepa kumshambulia Biteko ila anaweka lawama zote kwa mtu ambaye alishaachana na hiyo wizara almost mwaka mzima. Rai yangu ni Mpina kama amejitanabaisha kuwa mzalendo basi asione haya kumlaumu Biteko kama amekosea kuliko kufocus kwa January ambaye alishaacha hiyo wizara kwa mwaka sasa.
Huu unafiki haumsaidii kabisa, kama ambavyo analaumu ripoti ya CAG haifanyiwi kazi ilihali kipindi cha JPM ripoti ilikua haifanyiwi kazi bungeni ila alikaa kimya sababu alikua ananufaika na maslahi ya serikali.
Pia soma
- Kuelekea 2025 - Luhaga Mpina kufungua Kesi zote ndani ya masaa 24
View: https://youtu.be/deGwIm86FcY?si=rc6xA8rxPydMpb65