Kuelekea 2025 Luhaga Mpina amshtaki Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuondolewa Bungeni kinyume na Sheria

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mawakili wa Luhaga Mpina wanazungumza na waandishi wa habari muda huu.

Pamoja na nambo mengine, mawakili hao wamesema mojawapo ya kesi zilizofunguliwa ni ile anayomshtaki Spika wa Bunge na Mwanasheria mkuu wa Serikali kwa kunyang'anywa na kunyimwa haki ya kuwakilisha wananchi wa kisesa na watanzania wote kwa vikao 15 Bungeni ambapo msingi wa kesi yake anaamini ameonewa kwa kuondolewa kinyume cha Sheria.

Aidha, Mpina anaamini hatua za kuchukuliwa dhidi yake zilikuwa zimepangwa hata kabla ya yeye kusikilizwa.

Hadi sasa, zaidi ya Mawakili 100 wamejitolea kumsaidia Mpina kwenye kesi hii.

Pia soma

Anajisumbua bure tu.

Mwambieni Luhaga Mpina kwamba ajiunge na wa-Tanzania wengine wenye mapenzi mema na nchi hii ambao wanapigania Haki, Demokrasia pamoja na upatikanaji wa Katiba Mpya iliyo nzuri yenye kubeba Maoni, mawazo na fikra za Wananchi walio wengi zaidi kwenye nchi hii.
Suala la upatikanaji wa Katiba Mpya iliyo Bora nchini Tanzania siyo Jambo linalowahusu CHADEMA au Wanasiasa peke yao.
 
Mahakama ni chombo cha kutoa haki. Mpina anatakiwa kutendewa haki
Mahakama inafuata sheria. Usifanye kosa la kuchanganya sheria na haki.

Mahakama zishawahi kutupa kesi za mashauri ya bunge kwa msingi wa kutenganisha nguvu za Bunge na Mahakama.

Nimeuliza swali hujanijibu, sijui kama hata umelielewa.

Mahakama haiingilii Bunge. Hii ni mihimili tofauti na yote inajitegemea. Sijui watu hawaelewi hii kanuni au vipi?

Hii kesi ya Spika na masuala ya Bunge linavyoendeshwa itasikilizwaje na Mahakama bila Mahakama kuingilia uhuru wa Bunge?

Huoni kwamba Mpina alitakiwa kwenda Bungeni na kuweka motion ya kumpigia Spika kura ya kukosa imani, Spika awe impeached? Wabunge wamalize mambo yao Bungeni bila ya kuingia kwenye mtego wa kupeleka kesi Mahakamani halafu Mahakama ikatae kusikikiza kesi kwa sababu ni jambo la uendeshwaji wa Bunge, na Mahakama haiwezi kuingilia mambo ya uendeshwaji wa Bunge?
 
Mahakama inaweza kutoa hukumu kuhusu uendeshwaji wa mhimili unaojitegemea wa Bunge na Spika?

Hukumu hiyo haitaharibu uhuru wa Bunge kama mhimili unaojitegemea?
Hiyo kesi imeshaisha, inasubiri hukumu tu. Nawashangaa hao Mawakili wake kwa kushindwa kumshauri mtrja wao.
Kitu pekee cha bunge ambacho Mahakama ina mamlaka ya kusikiliza kama kitapelekwa kwenda kuwa challenged Mahakamani ni sheria zilizotungwa na bunge, lakini maamuzi ya bunge. Bunge hata lingeamua kumnyonga Mpina, hakina chombo ambacho kina legal power ya kuhoji maamuzi yake.
 
Hao wanasheria wengine hata kama wanajua hapa hakuna kesi, wanaweza kumjaza ujinga Mpina ili wale pesa zake tu.

Ila kiukweli hapa Mahakama itaitupilia mbali hii kesi kabla hata ya kuisikikiza kwa kina.

Kwa sababu ya "separation of powers".

How do people not see something that is so obvious?
 
Yes, ni kweli, Kesi hii haina mashiko kisheria.

Mchawi mkubwa zaidi kwa Kesi hii kukosa mashiko ni kwa sababu ya kuwepo kwa Katiba mbovu na mbaya.
 
Kwa hiyo Spika wa Tanzania yupo juu ya sheria? Anaweza kufanya lolote analotaka kwenye himaya yake na asichukuliwe hatua?
 
Yes, ni kweli, Kesi hii haina mashiko kisheria.

Mchawi mkubwa zaidi kwa Kesi hii kukosa mashiko ni kwa sababu ya kuwepo kwa Katiba mbovu na mbaya.
Katiba ni mbaya, lakini mara nyingi tunailaumu katiba wakati tatizo ni sisi wenyewe.

Hata kwa katiba hii mbaya, Mpina ana uwezo wa kwenda bungeni na kuanzisha process ya kumu impeach Spika, Waziri Mkuu na Rais.

Lakini watu walio Bungeni hawawezi ku support lolote kati ya hayo.
 
Back
Top Bottom