Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 216
- 991
Mawakili wa Luhaga Mpina wanazungumza na waandishi wa habari muda huu.
Pamoja na nambo mengine, mawakili hao wamesema mojawapo ya kesi zilizofunguliwa ni ile anayomshtaki Spika wa Bunge na Mwanasheria mkuu wa Serikali kwa kunyang'anywa na kunyimwa haki ya kuwakilisha wananchi wa kisesa na watanzania wote kwa vikao 15 Bungeni ambapo msingi wa kesi yake anaamini ameonewa kwa kuondolewa kinyume cha Sheria.
Aidha, Mpina anaamini hatua za kuchukuliwa dhidi yake zilikuwa zimepangwa hata kabla ya yeye kusikilizwa.
Hadi sasa, zaidi ya Mawakili 100 wamejitolea kumsaidia Mpina kwenye kesi hii.
===
Kesi (ya kupitia uhalali wa kisheria kuhusu utolewaji wa vibali vya kuagiza sukari) imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam ambapo mdai ni ndugu Luhaga Mpina, ambao anawashtaki ni Waziri wa Kilimo, Bodi ya Sukari, viwanda vya ITEL, Zenji Industries, Waziri wa Fedha ambaye yeye anashtakiwa kwa kutoa misahama ya kodi ya VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani) ambapo Mpina anadai hata taarifa ya msamaha wa kodi haikuchapishwa katika gazeti la serikali, lakini pia Mpina amemshtaki Kamishina Mkuu wa TRA kwa kutokudai na kukusanya kodi kwa watu waliopewa vibali vya kuagiza sukari lakini wa mwisho kushtakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, shauri hilo liko mahakamani tayari.
Pia soma