Lowassa, Sumaye wametumwa, Mbowe ni adui wa mabadiliko

Unaweza ukawa sio mwanachama kwa maana ya kwamba hujakata kadi ya uanachama, kwa jinsi ulivyoelezea mada yako inaonesha dhahiri kuwa wewe ni shabiki wa CHADEMA and so obviously ni mkereketwa na mfuasi wa hiki chama hasa ulipomalizia na kibwagizo cha "tuanze upya..."
Mi naona kiujumla wake bila kumung'unya maneno, mwenyekiti wa chama na baadhi ya wazee founders wa hiki chama wana ajenda ya siri dhidi ya mkakati madhubuti wa kushika hatamu za uongozi wa hii Nchi.
Kiukweli kabisa chama kinaendeshwa kwa matukio na uanaharakati. Uongozi hauna vision ya kukijenga chama from grassroots licha ya kwamba chama kimeenea na kutambulika nchi nzima na kimesheheni wafuasi wengi wenye ari ya mabadiliko, uzalendo na utayari wa kutumika kwa masrahi ya chama lakini utastaajabu mpaka leo hii kuna miji imeshikiliwa na CDM huko wilayani lakini chama hakina ofisi maalum.
Kero kuu za uchaguzi mathalani TUME HURU YA UCHAGUZI bado hadi leo haijaoneshwa ni namna gani chama kitashughurikia... N.K N.K
#TRUTHMUSTBESPOKEN
 
ila dah....ujue kwa kipindi cha miaka ya Kikwete Chadema imekuwa kubwa kweli na hali ingeendelea kama kwenye kipindi cha Kikwete nadhani CHADEMA wangekuwa wanafanya aina ya siasa aliyoitaka Lowassa hapa



ila kwa huyu aliyeingia madarakani sasa hivi naona yeye ndio analazimisha CHADEMA wawe wana harakati kwa kuturudish tena nyuma kama jenerali ulimwengu alivyosema
Maandamano kwa siasa za Afrika bana ni muhimu, hasa kwa serikali na vyama tawala ambavyo havisikilizi upinzani kama Kenya walikuwa wanataka tume mpya lakini serikali ikabana jamaa wakaingia mtaani, serikali ikaja kwenye majadiliano
 
Huwezi amini kumsikia mh Mbowe wa sasa na mbowe enzi ya Dr. slaa. Believe Mbowe ni mfanyabiashara.

Msikilize Lowasa
1) huwezi zuia wafanyabiashara
2) chama hatutaki hara


kati na maandamano tena.

msikilize mbowe
hakuna tena harakati wala maandamano, haki IPO mahakamani.

swali je hajui huko mahakamani majaji huteuliwa na mwenyekiti wa ccm yani raisi, haoni tatizo .
amesahau hukumu ya mita 200, amesahau ya wenje,amesahau ya kafulila. hio ni tahadhari.

Harakati za bavicha zimrsaidia jeshi la polisi kuruhusu mikutano ya ndani mbn mbowe unakuwa kipofu?

mbowe unamtumikia Lowasa au chadema?

Bavicha kunahaja ya kujitafakari km kuna haja ya kumsikiliza Lowasa na strategy za kiccm.

mh mbowe isije ikawa 2015 u gained something!!
Hii ndiyo shida ya kunywa mataputapu asubuhi,mtu mzima unalewa asubuhi hii wewe hujitambui kabisa.
 
Una hoja lakini kuna baadhi ya nyaya za hasi na chanya zimegusana kichwa zinatoa cheche za unafiki. Ulitoka ighaibuni kuja kumpigia Lowassa kura bado unasema huna chama. Unashauri "tuanze upya" wewe na nani kama huna chama? Futa huo Uzi ujipange upya uurudishe ukisha U edit.
Alimpigia Lowasa huyo
 
mtoa maada nakubariana na wewe 100%.yani kitendo cha Dr slaa kuhama chama na kupokelewa Lowassa ilikuwa ni raha kwetu wapenzi Wa CCM!!Mimi kabla ya mkutano Mkuu Wa ccm July 2015 nilikuwa najiuliza haya
1.CCM itamweka nani Wa kubambana na Dr slaa?Dr slaa alikuwa anauzika sana ile mbaya hata Mimi nampenda!!

2.CCM walicheza mziki mzuri sana aisee!maana kama wangemweka lowassa wangeanguka vibaya sana!!kuwa hiyo namshukuru sana Mungu lowassa kuhamia chadema

3.chadema walinishangaza sana!!how can you compare Dr slaa versus Lowassa?good comparison was Dr slaa versus Dr Magufuli!!

4.bado chadema wananishangaza sana!eti lowassa amewasaidia chadema kupata kura nyingi ,majiji etc
this is very wrong!! kwanza walipoteza vitu vingi mpaka sasa!!
 
Watu wameshapiga tuzo za amani utawaambia nini...???
Kwi kwi kwi...
Kwa wengine CDM ni kila kitu kwa hiyo mleta mada atapingwa sababu kuukubali huu ukweli ni sawa na kujipiga risasi mguuni....

Tunasubiri chama kipya....
hakuna upinzani Tanzania...

Hakuna anayependa mifujo ambayo inaangamiza wasio nacho...ila kwa ujio wa huyo Mzee huko CDM naona wameishiwa pozi zote...hata cha kuongea majukwaani hawana.....wamebaki kulazimisha bifu na serikali au hata speaker...

Huwezi amini kumsikia mh Mbowe wa sasa na mbowe enzi ya Dr. slaa. Believe Mbowe ni mfanyabiashara.

Msikilize Lowasa
1) huwezi zuia wafanyabiashara
2) chama hatutaki hara


kati na maandamano tena.

msikilize mbowe
hakuna tena harakati wala maandamano, haki IPO mahakamani.

swali je hajui huko mahakamani majaji huteuliwa na mwenyekiti wa ccm yani raisi, haoni tatizo .
amesahau hukumu ya mita 200, amesahau ya wenje,amesahau ya kafulila. hio ni tahadhari.

Harakati za bavicha zimrsaidia jeshi la polisi kuruhusu mikutano ya ndani mbn mbowe unakuwa kipofu?

mbowe unamtumikia Lowasa au chadema?

Bavicha kunahaja ya kujitafakari km kuna haja ya kumsikiliza Lowasa na strategy za kiccm.

mh mbowe isije ikawa 2015 u gained something!!
 
Mi sio mwanachama wa chama chochote lakini kwa elimu yangu ndogo niliyo nayo nimeanza kuwa na mashaka na uepo wa Lowassa CHADEMA

Baada ya kufatilia kauli zake nyingi nimegundua anaibadilisha taratibu CHADEMA kuwa kama CCM.

CHADEMA ni chama chenye wafuasi wenye nembo ya uaminifu,utiifu,ukweli na uwazi not double standard.

Kwa kauli hizi

1:Nauchukia umasikini;

Hivi kweli ninani achukii umasikini awe Magufuli, Kikwete, Mkapa, Mbowe wote wanauchukia umasikini hata mimi nauchukia umasikini kwahiyo kauli ile nilikuwa ni kauli dhaifu kabisa kuwashawishi watu wakupigie kura ingawa labda nyuma yake ulikuwa na lengo zuri.

2:C HADEMA ni chama cha uanarakati:

Kitendo cha kusema CHADEMA ni chama cha uanaharakati ni kuwakatisha tamaa wanachama karibu robo tatu na wafuasi wao waliokuwa wanapigania mabadiliko ya kweli watu kama Lema,Sugu,Mnyika,Lissu unafikiri hii kauli wanaichukuliaje?

3:Uwezi pambana na wafanya biashara;

Unaeza sema kwa maana nzuri lakini ukajikuta unaaribu maudhui na maana halisi ya unachokimaanisha hapa mi najua hakuna taasisi,watu mtu aliye juu ya sheria kila kitu inabidi kizibitiwe!!

4:pPigeni kura mimi nitazilinda;

Mimi nilisafiri kutoka masomoni nje na kuja nyumbani kumupigia kura kwakujua atazilinda kinyume chake akaja na sababu ya kuibiwa kura najua aliwakatisha tamaa mamilioni ya watanzania.

Ukweli mchungu najua kuna watu watakuja kunishambulia lakini nina uhakika kama CHADEMA wasingempokea Lowassa wangepata vitu zaidi vya ubunge na kingeimarika zaidi.

Kujiondoa kwa Dr slaa:

Dr slaa alitakiwa abaki CHADEMA kwa gharama yeyote kuliko kuondoka
Ni aibu kama Dr slaa asiye na chembe ya ufisadi kuondoka ndani ya chama alafu watu wakaja hapa na kusema hakuna athari?

Nimekaa nikajifikiria hivi tulikuwa serious tunataka mabadiliko au tunatania?

Lowassa huyu aloyekataa katiba ya Warioba??
Lowassa huyu huyu tajiri Mwenye kilakitu duniani?

Lowassa huyu huyu ambaye wamekuwa na tuhuma kibao kama walivyo magamba wenzie waliobaki CCM?

Lazima kama taifa tufike sehemu tukubali ukweli tuanze upya kwani kwanza upya kuna gharama gani?

Sio lazima Lowassa aondoke CHADEMA la hasha ila asipewe nafasi ya kuwa na nguvu kama wanavyotaka kufanya sasa kama anakifadhiri chama afanye kama mwanachama wa kawaida naamini CHADEMA bado ni chama cha upinzani chenye watu wengi na lakini ila ili kiendelee kuaminika lazima watu wenye makandokando kama Lowassa,Sumaye, na wengine wasipewe nguvu ndani ya chama.

NB;
Mtu ambaye CHADEMA ilimchukua kwa umakini ni Ester Bulaya tu.

Kiukweli tuanze upya tumeshindwa kupata mabadiliko tunayoyataka nina uhakika tukijipanga 2025 tunaweza kuwaangusha magamba lakini sio kwa kuwatumia Lowassa,Sumaye, masha, etc

Angalizo ndani ya UKAWA pia wamulikeni Sumaye, Mbatia, Lipumba kama akirudi na Zitto kama akirudi.

Nawasilisha!

Declare tu interest,muongo huwa hajifichi!Angalia kwenye bold ukinzani unavyotokea
 
Lowassa alipiga NO kupitisha rasimu ya ya Mzee Warioba!
CHADEMA sasa mtapigania katiba mpya ipi wakati mgombea wenu 2015 na likely 2020 alipiga kura ya hapana rasimu ya Warioba?

CHADEMA imepoteza dira!
 
Anaweza asiwe cdm lkn anapenda mabadiliko. Anayosema yupo sahihi uyu lowasa alikamata wenyeviti wote ccm. Cdm kaanza na mameya nyie mnamchekea tu.


kwani kukamata wenyeviti wa huko ccm nini aliambulia? Au akikamata mameya ndo kuikamta chadema? Ile taasis sio mtu mmoja anaetoa maamuz kama yanatija yatafuatwa kama hayana yatapgwa chini hizo ramli chonganish achaneni nazo.
 
Tatizo
Sasa kama huna chama si utulie kama katumwa au hajatumwa wewe inakuhusu nini? Fanya yako kama siku zote endelea kuvipa kisogo vyama vya siasa maanguko yao hayatakuathiri kwa kuwa haufungamani na upande wowote.[/QUOtatizo sisi watanzania huwa hatupendi kushauliwa wala kukosolewa,mimi naamini karata ya lowasa itakuja kuigharimu sana chadema kuliko faida tuliyoipata,naungana na mleta madaa
 
Naipenda CHADEMA.....Lakini umakini wa Viongozi wangu unanitia mashaka sana.....
 
Hfd dh
y [Iguj vvgh
MG] [/IMG]/IMG]
ibhj. gbugh v
vvgv[gvIMG]h[/IMG]
[/IMG][/IMGg
jvg hu h
[/IMG][/IMG]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom