Lowassa kugombea tena Urais Mwaka 2020, asisitiza yupo fiti

Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa mawzo yake kwakuwa ana utashi wake binafsi so naomba nitoa mtizamo wangu na sitatoa maoni ili kumfurahisha mtu humu ndani ya Forum ni maoni yangu na nina haki ya kuwa tofauti au sawa kimawazo na mtu yoyote.EL anaifaa Tanzania kwa sababu zifuatazo:-

Ni Kiongozi huyu shupavu,jasiri na mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama na serikali kwa upande wa serikali hili linadhihirika aliposhika nyazfa mbali mbali kama:-

a.Kusimamia Sekta ya Elimu ambayo ndiyo Uti wa mgongo wa maendeleo ya Taifa lolote hapa Duniani.Alisimamia kwa ukakamavu kutekeleza mpango wa kupanua Elimu ya Sekondari na alihimiza kwa nguvu zake zote ujenzi wa Shule za Kata Nchi nzima ili kuwapa Fursa Mamilioni ya Watanzania wenzetu waishio Vijijini kupata Fursa ya Elimu.

Zoezi hili lilihitaji uwekezaji mkubwa sana na Tukumbuke kwamba Taifa letu ni Maskini sana,changamoto zilizo ikabili Sekta ya Elimu kama Ukosefu wa vifaa vya maabara,Nyumba za Walimu,Madarasa ya Kutosha na upungufu wa Vitabu si kosa la mtu Fulani bali umaskini wa Taifa letu ndio maana WB na IMF hutoa misaada kwa nchi maskini kusaidia maendeleo ya Elimu kwakuwa ni Sekta inayohitaji uwekezaji mkubwa kifedha na Rasilimali zingine.

EL ni mtu anayeamini katika Elimu ndi maana motto wake ni tofauti kidogo na Motto wa Chama chake na anasema '' ELIMU KABLA,KILIMO KWANZA'' Ni kweli kabisa kwamba hakuna linaloweza kufanikiwa bila Elimu,Unaweza kuwaambia watu wasio na Elimu ya kutosha Walime Kilimo cha Kisasa?Me I agree kwamba Elimu KABLA na Kilimo Kwanza.

Mataifa Makubwa yaliondelea leo Duniani yalifanya uwekezaji Mkubwa kwanza katika Elimu,hasa Elimu ya Msingi(Kwa mfano China,Brazil na USA) na Baadaye kufanya Mapinduzi Makubwa ya Kilimo,baadaye Viwanda Vidogo na baadaye Viwanda vikubwa ambavyo vilichochea kukua kwa kasi kwa Sekta za Huduma na kupelekea mfumuko wa nafasi kibao za ajira kwa Vijana!!!

b.Kuwafukuza bila woga hadi kuwasindikiza Airport wawekezaji wababaishaji wa Kampuni ya City Water hadi kuwapandisha ndege uwanja wa
Taifa:

Akiwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo ,EL alitekeleza wajibu wake kwa umahili mkubwa na bila uwoga na moja ya mambo ambayo yatakumbukwa ni kufukuzwa kwa wawekezaji wababaishaji wa Kampuni ya Kitapeli ya City Water ambao walishindwa kutekeleza wajibu wao,aliwatimua na kuwasindikiza hadi Airport!EL ni Kiongozi Shupavu sana na asiyeogopa mtu!

c.Kiongozi Mwajibikaji na asiyeogopa kufanya maamuzi magumu hata kama yatamuuza

Kujiuzulu kwake kutoka katika Wadhfa wake wa Uwaziri Mkuu kufuatia Kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond inachukuliwa na wengi kama kuhusika kwake katika Saga hilo.Napenda kuwakumbusha Watanzania wenzangu kwamba Waziri Mkuu ndiye mtendaii Mkuu wa Shughuli za Serikali na mtekelezaji wa Maagizo ya Baraza la Mawaziri ambacho kimsingi ndicho chombo kikubwa cha Utendaji wa serikali (Govt. Machine) na hivyo kama kuna Kosa linafanyika basi Linatosha kuiangusha Serikali nzima so katika SAGA ile ilibidi Serikali Nzima akiwa ni Pamoja na Rais wajiuzuru lakini EL akubali mwenyewe kwa ajili ya kulinda heshima ya Chama chake na Serikali, huu ni mfano mzuri wa kuigwa kwa Waafrika wote.

Siku zote tatizo letu waafrika ni kukosa kuwajibika pale inapobainika uzembe umefanyika,ukweli umebaki kuwa wazi mpake leo hii NCHI IPO GIZANI migao ya Umeme inaendele kama kawaida na dada wa Richmond ambaye ni Dowans Mitambo yake inawashwa na tumerudi pale pale!! Mimi nasema kwa kosa la Richmond,Serikali nzima ilikuwa imeanguka.

d.Mfuatiliaji na asiyechoka kufuatilia kero za na hakai ofisini kungoja taarifa
Wakati wa janga la Njaa lilisababishwa na ukame kwa msimu wa mwaka 2007/08 ni huyu EL alikuwa akishirikiana na Wakuu wa Wilaya zote zenye njaa na wakati mwingine alishiriki yeye mwenyewe kupita nyumba kwa nyumba kusimamia zoezi la ugawaji wa chakula kwenye Familia zenye njaa ili kuhakikisha kwamba azma ya serikali ya kwamba hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa inatimizwa ni huyu huyu EL.


Mtu hawezi kukosa mapungufu hata siku moja,nakubali ana mapungufu yake lakini EL ni embe dodo lililoiva tayari kuvunwa na Watanzania Mwaka ukifika 2020
 
raisi wa shirikisho la walioshindwa uchaguzi. yeye achukue ramani ya ikulu akajenge monduli na si vinginevyo.
 
....
.....kila Mtanzania angejaa mapesa viraka tupa kulee ...wakulima kama Texas tungefuga farasi wa kukagulia mashamba....
 
hata wewe unafaa kuwa rais, watanzania hawako demanding unachotakiwa kuwadanganyadanganya tu
 
Kwa kipimo chochote kile, safari ya Mh. Edward Lowasa kuelekea ikulu imekua ndefu. Amepitia na kuvuka mabonde na milima. Mito yenye mafuriko kavuka. Sifa kwa matusi zote kapitia. Ilifika mahali hata wale walio mtusi na kumkejeli kuliko pitiliza akawasamehe na kuungana nao ili safari iendelee. Swali, je safari bado inaendelea au imefika mwisho kabla hajafika?
 
Kwa hiyo sasa amekubali kuwa ameshindwa na hakuna tena kupeleka case ICJ?
Kwa kauli hii ya Lowasa sasa nimeamini kuwa mkataba ulio sainiwi kati ya Mbowe na Lowasa na ulio gharimu zaidi ya billion 4 ulikuwa ni wa miaka zaidi ya 10 Lowasa kugombea Urais bila kupingwa au kupendekezwa na mtu yeyote ndani ya chadema!

Ni wazi chadema ni mali ya Lowasa....
Lowassa alipendekezwa na Kamati Kuu ya CHADEMA, Dr Slaa akiwemo, kisha akaja kupitishwa na mkutano mkuu pale Mlimani City, ingawa kulikuwa na kura moja ilimkataa Lowassa lakini haikutosha kimzuia. Kwahiyo hayo uyasemayo ni yakwako mwenyewe!
 
1.2020 unagombea ?
2.Makato kwa wadaiwa wa loan board itakuwa 15%?
3.Malimbikizo na maslahi kwa watumishi apo unasemaje?
4.Ule wimbo wako uliokuwa unasema tatizo la ajira ni Bomu linalosubiri kulipuka umejipangaje kulitegua?
5.Upo tayari kurudi nyumbani?
 
Back
Top Bottom