“Kuweni watulivu na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.
****************************
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema njia ni nyeupe kwa Chadema kuingia Ikulu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.
“Kuweni watulivu na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.
Akizungumza nyumbani kwa kada wa Chadema, James Lembeli katika kijiji cha Mseki, Kahama, Lowassa (pichani) alisema ameshindwa kuzungumza na kufanya mkutano na wananchi wa kijiji hicho akihofia kukamatwa na polisi kama alivyokamatwa Geita na kuwataka wawe wavumilivu hadi uchaguzi wa mwaka 2020.
Kadhalika, Lowassa aliwataka vijana wasikubali kuibiwa kura kwa madai uchaguzi uliopita hawakutendewa haki na ndio maana walikosa ushindi.
*By Shija Felician, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz*
MY TAKE: Hivi kwanini Lowasa usisubiri mchakato ufike? Kwanini unajimilikisha ugombea urais? Utakatwa na huko CHADEMA.
Alisha nunua chamaIla siasa za bongo pasua kichwa yaan mtu anajitangaza kugombea uraia kabla hata muda kufika? Sifahamu katiba ya chadema inasemaje kuhusu mchakato wa kumpata mgombea urais ila kwa style hii kwa sisi wapenda democracy inatutia mashaka
Hakuna michakatoHapo inatakiwa kama chama chadema watolee ufafanuzi kwa kua kumpata mgombea kuna michakato yake
Na sasahivi anamamluki kibaoLowasa ndiye mwenye chama ameweka zaidi ya billion 5 hapo na zitakwisha 2030 hivyo wakimkata patachimbika kabisa..............
HahahaHakuna michakato
Ukisha malizana na Mbowe
Basi wewe ni mgombea