Lowassa anasafishwa!

Ukweli ni kuwa akipewa baraka na CCM basi tujiandae tu kumkaribisha ikulu. Kwani iwe isiwe atashinda tu. Hivi sisi kama wananchi jukumu letu katika hili ni nini? Hivi ni kweli hakuna tunachoweza kufanya kama tukihisi chama chetu kinataka kutupeleka pabaya? Je mnataka kuniambia kuwa ni kweli wakati CCM inamsimamisha JK hatukuwa tunaufahamu utendaji wake wa kazi? Mbona basi tuliruhusu akasimamishwa?

Nafahamu wengi mtajibu kuwa hamkuona mwingine wa kumpa kura zenu but hey inawezekana tulikuwa na chance kubwa ya kuzuia ushindi wake katika ngazi ya kusimamishwa kama mgombea pekee wa CCM na si katika uchaguzi kwa vile naamini CCM ninayoifahamu mimi ni ile ambayo ikiamua inataka kitu basi hupata na hakuna wa kuzuia.
 
...na agombee tu. Ni haki yake kikatiba, ...na si ajabu akajizolea kura nyingi tu za kumtosha.
 
1.Yeye Kurejea na Kuiongoza Tanzania-'Over my dead body' and i suppose i speak for many Tzns.

Chunga hiyo kauli, lolote laweza tokea Tanzania ukasononeka sana. Mie sikutegemea kabisa na nikaapa piga ua CCM isingetuchagulia mkuu wa kaya 2005 lakini Wadanganyika, ambao ndio wengi, hasa Kanda ya Ziwa, wakaniangusha najiona!!!

Matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona, nchi haina tena uongozi. Hivi mkuu wa kaya yetu wa leo alikua na wasifu gani hata kuwashinda wagombea wenzake wakati ule kama sio ufisadi tu?
 
...na agombee tu. Ni haki yake kikatiba, ...na si ajabu akajizolea kura nyingi tu za kumtosha.


ni haki ya kikatiba lakini hana qualification...atapata kura kwa vile tu sisi ni wavivu wa kufikiri na wa kukubali mabadiliko-nidhamu ya kiuoga.
 
...na agombee tu. Ni haki yake kikatiba, ...na si ajabu akajizolea kura nyingi tu za kumtosha.

We do not need this kind of spirit, the issue isn't about him going for presidency, the issue is, does he possess what it takes to lead us!
 
ni haki ya kikatiba lakini hana qualification...atapata kura kwa vile tu sisi ni wavivu wa kufikiri na wa kukubali mabadiliko-nidhamu ya kiuoga.

Mkuu nadhani anaweza kuwa na qualification, ila legitimacy ndo inaweza kugomba hapo!
 
Join Date: Tue Mar 2009
Posts: 1
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Credits: 6,610




Mkuu karibu JF na hongera kwa nondo moja....Kaazi kweli kweli,



Duh! Mkuu Jmushi1 una macho aisee!
 
ni haki ya kikatiba lakini hana qualification...atapata kura kwa vile tu sisi ni wavivu wa kufikiri na wa kukubali mabadiliko-nidhamu ya kiuoga.

...nyie nani? CCM? ...anazungumziwa Lowassa kama Mgombea wa CCM, na hakuna mgombea atayepitishwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM bila kupitishwa na halmashauri kuu na 'kapu lao'

We do not need this kind of spirit, the issue isn't about him going for presidency, the issue is, does he possess what it takes to lead us!

...again, ('We do not...') nyie kina nani? ...wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM?

Mimi ni Mtanzania, na kama kawaida yangu kura yangu (ya siri) nitampigia yule tu ninayeamini anamuelekeo wa kuleta mabadiliko na maendeleo nchini. CCM wakileta mgombea mahiri, nitampigia kura, ...hivyo hivyo CHADEMA, CUF au wengineo...

Sipigi kura eti tu kwakuwa CCM 'wameamua' iwe hivyo! No way!...
 
Chunga hiyo kauli, lolote laweza tokea Tanzania ukasononeka sana. Mie sikutegemea kabisa na nikaapa piga ua CCM isingetuchagulia mkuu wa kaya 2005 lakini Wadanganyika, ambao ndio wengi, hasa Kanda ya Ziwa, wakaniangusha najiona!!!

Matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona, nchi haina tena uongozi. Hivi mkuu wa kaya yetu wa leo alikua na wasifu gani hata kuwashinda wagombea wenzake wakati ule kama sio ufisadi tu?

Mkuu hiyo ni kweli tupu? yaani si ajabu kabisa mzee wa kasungura kutuna Magogoni in mwakani!
 
Akitaka kura yangu agombee mwakani 2010 na si 2015.Akijitokeza kum challenge Kikwete patakuwa patamu na ndipo tutashuhudia mparaganyiko kama siyo mgawanyiko ndani ya CCM manake Lowasa ni maji marefu.
Lowassa ni mchapakazi,mfuatiliaji mzuri wa mambo na ana vision isipokuwa tu kwenye uadilifu ndipo inawezekana ana tatizo.Lakini hata hivyo kiongozi gani wa CCM ni mwadilifu?Kwangu mimi Lowasa angeweza kuipeleka Tanzania mbele kuliko Kikwete.
Go Lowassa Go..
 
Msijisumbue na tetesi jamaa.........Dk. S.J. Malecela alishasema....na kama mngejua how many in CCM are behind his sentiments.......wala msingejisumbua na hizo tetesi.....hiyo ndio imetoka JK ni nominee wa CCM for 2010 Presidential elections........
 
huyu mtu kweli ni Kin'gan'ganizi kama bado ana-ndoto hiyo, lakini ukweli wenyewe hiyo sio 'pipedream' tu ni kitu ambacho ni possible ingawa ni unimaginable. many of us see 'EL' for what he is (chui kwenye ngozi ya kondoo) and what he represent for Tanzanias (Yudas) asiejali mimi na wewe tunaenda wapi. sasa basi kwa upande wangu na nnavyojua mimi kugombea kiti kupitia CCM lazima, wabunge kadhaa wakukubali na wakupigie kura kama mwakilishi wao au labda kama siku hizi CCM inaweza kutoa wagombea wawili kwa wakati mmoja ntashukuru kufahamishwa kama nimekosea hapo. na iwapo nipo sawa kama huyu mtu atapitishwa na wabunge awe kama msimamizi wa CCM for the first time in my life nntasema sasa nisapoti chama kingine labda nianze kusikiliza sera za CUF, vizuri after all Bwana Lipumba in my opinion was the most qualified person to run Tanzania if only he was under CCM.

lakini bwana fisadi akipita au akipitishwa na wabunge maana yake basi hata wao hawajali maisha yetu sasa kuna sababu gani ya kumlilia mzazi ambae kesha sema we si mwanangu embu tufikirie vitu kwanza kabla atuja jadili, implications zake na vina maana gani. huyu mtu ni wa kufukuzwa CCM na si wa kusimamia chochote zaidi yaa Monduli huko tunajua wengi hawata elewa lakini wapo amboa wange prefer General Sayore awa represent huko kuliko huyu shetani.

embu angalieni shetani muone shetani na si kitu kingine chochote

Mungu Ibariki Tanznania
 
Last edited by a moderator:
Any disqualifications he has for not dare inter into the race?
 
Last edited:
JK na EL ni marafiki wa muda mrefu na hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kwamba urafiki umekufa ama umetetereka tangu siku EL alipojiuzulu. Kama wawili hawa bado wanaelewana na kama ni kweli EL ana nia ya kutaka kuwa Rais 2015 JK hatasita kumsaidia.

Kama ni kweli EL anajiandaa kwa 2010 haitashangaza tukisikia kwamba amepata baraka za JK. Who knows, huenda JK kutokana na afya yake kutetereka anaweza kuamua kuachia ngazi kwa hiari yake ampishe mshirika wake aendelee na kipindi kijacho. Tuliwahi kuambiwa kwamba kulikuwa na dili kati yao kwamba yeyote atakayepata urais basi mwenziwe awe PM? Nani zaidi wa kuweza kuachiwa nafasi hiyo? Katika utatu ulle, RA si rahisi kuachiwa kwa sababu si CCM wala wananchi walio wengi watakaoweza kukubali kumpa kura. Bado Watanzania wazawa hawajafikia hatua ya kukubali kutoa uongozi kwa 'mtu yeyote' tu.

Nchi hii kwa hali ilivyo, chochote kinawezekana. Tuombe Mungu hapo EL atakapopata urais amgeukie Mungu, akimshukuru kwa utajiri wote alionao na kwa kuupata urais aliokuwa akiutamani kwa muda mrefu. Aridhike, amtumikie Mungu kwa kuwatendea Watanzania haki iliyopotea. Atumie ujasiri wake kwa kutomuonea haya yeyote, awaondolee Watanzania janga linalowaumiza na linaloimaliza nchi yetu - UFISADI.
 
Back
Top Bottom