Gazeti la Tanzania Daima limetuhabarisha leo ya kuwa Mheshimiwa Mbunge wa Monduli ametofautiana na JK kuwa yeye anaamini nchi itangulize elimu kwanza badala ya kilimo kwanza.....
Lowassa amkosoa Kikwete
Asema elimu kwanza, kilimo baadaye
na Salehe Mohamed, Dodoma
ALIYEKUWA Waziri Mkuu, Edward Lowassa, amesema serikali inapaswa kutanguliza Elimu Kwanza badala ya Kilimo Kwanza, ili kuwawezesha wakulima na wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu shughuli wanazofanya.
Lowassa alitoa kauli hiyo jana katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chamwino, mjini hapa baada ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na kuongeza kama elimu itapewa kipaumbele zaidi kuna kila dalili Tanzana ikapiga hatua katika nyanja za kilimo, uvuvi, ufugaji na nyinginezo.
Alisema mkulima mwenye elimu ya kutosha hataweza kulima kilimo cha kisasa pamoja na kuwasiliana na wanunuzi wa mazao yake.
Mimi naona tungetoa nafasi kwa Elimu Kwanza halafu ndiyo ije hiyo ya Kilimo Kwanza; kuna nchi zimeendelea zaidi kwa sababu walianza kuwekeza kwenye elimu, naiomba serikali kuliangalia suala hili kwa umakini zaidi, alisema Lowassa.
Aliongeza kuwa serikali ya sasa inapaswa itafute mbinu madhubuti ya kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana ambalo linawafanya vijana wengi kukimbilia mjini kwa lengo la kutafuta kazi.
Alisema tatizo hilo linaweza kutatuliwa iwapo huduma muhimu za kijamii, pamoja na shughuli mbalimbali za kiuchumi zitapelekwa vijijini.
Wakati akizindia mpango wa Kilimo Kwanza, Rais Jakaya Kikwete alizitaka sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kutekeleza na kufanikisha mpango huo akisema awali ushiriki wa sekta hiyo ulikuwa dhaifu hali iliyopelekea kudhoofika kwa mipango mbalimbali ya kilimo iliyowahi kutangazwa.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, ambaye alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Pinda, alisema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana lisipoandaliwa mikakati madhubuti litakuja kuiyumbisha nchi na kuleta mvurugano.
Alisema nguvu kazi kubwa ya sasa ni vijana na hawana kazi hivyo ni vema serikali ikajenga mazingira bora ya kuwawezesha kiuchumi pamoja na kujenga viwanda vitakavyosaidia kutoa ajira.
Ukosefu wa ajira ni bomu la muda, tusipokuwa makini likija kulipuka nchi haitoweza kukalika, tuandae mazingira mazuri yatakayosaidia kuwepo kwa viwanda au kuwawezesha kiuchumi, alisema Lipumba.
Alibainisha kuwa Waziri Mkuu ana wajibu mkubwa kuhakikisha kunaundwa Tume huru ya Uchaguzi ili kuepusha mizengwe inayotokea mara kwa mara kwenye chaguzi.
Naye Mwenyekiti wa TLP, Agustine Mrema, alisema Pinda ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi hivyo ni vema akautumia kurekebisha masuala mbalimbali ambayo ni kero kwa wananchi ikiwemo umaskini.
Sherehe za kuapishwa kwa Pinda, zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dk. Alli Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad na viongozi mbalimbali.
Wakati huo huo, wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamesusia kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikiwa ni msimamo wao wa kutomtambua Rais Jakaya Kikwete, ambaye wanadai alipata ushindi kwa sababu ya kuchakachua (kuiba) kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Mheshimiwa Lowassa amesema bila ya raia kuwa na uelewa wa kutosha hata hicho kilimo kwanza utekelezaji wake utakuwa mgumu..............
Maono yangu yananiongoza kuamini ya kuwa JK hana mpango wa kumweka Lowassa kwenye baraza la mawaziri kwa sababu siyo za uadilifu au uchapaji kazi - JK hajali sifa hizo katika uteuzi zake na huzitaja tu ili kumwaga changa kwa wapigakura tu- lakini JK anamwona Lowassa atavuruga hesabu zake za kumrithisha Uraisi mzanzibari ambaye JK atamwandaa hivi sasa kwa madai ya kuimarisha muungano huku anaendeleza ajenda ya siri ya kuhakikisha maamuzi ya uanzishwaji wa mahakama za kadhi na nchi hii kujiunga na OIC hayatahojiwa na serikali inayoongozwa na mkristu...........bila ya kujali chama anachotoka................
Ninauhakika ya kuwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo nchi hii itakuwa imejiunga na OIC na mahakama za kadhi kuanzishwa .......................mbali ya JK jana kudai ya kuwa kuna nyufa za udini na serikali yake itafanya juu chini kuzishughulikia.................lakini ukweli ni kuwa kazi kubwa atakayoifanya kwa miaka mitano ijayo ni kuzikuza nyufa hizo kwa kutoa upendeleo kwa dini yake...............
Lowassa haya yote amekwisha kuyaelewa na ndiyo maana anaonyesha ghadhabu zake kwa kutofautiana na JK hadharani.................