Lowassa amkosoa Kikwete

Unapochangia kwa nia ya kuelimisha wengingine usiwe mbinafsi wa kuruhusu fikra zako zionekane za msingi zaidi kuliko uhalisia wa kile unacholenga kuelimisha. Lowasa anamaono yake na dira yake.Labda ameshaambiwa yeye kuwa waziri tena ni ngumu ndio maana yeye anamwaga ugali ikiwa Jk kamwaga mboga. Unanipa tafakuri kubwa sana juu dhana ya UDINI. Kwa maana yako mwizi wa umma kama Lowasa kumbe kafanya sawa kwa misingi dini ya kikikristo? Au unamaanisha Lowasa akija CHADEMA ATAKUWA msafi mbele ya watanazia? Kwa hiyo CHADEMA NI CHAMA CHA DINI YA KIKIKRISTO sio!!! MWALIMU MZURI NI YULE MWENYE UWEZO KUMFUNDISHA MWANAFUNDISHA AKAELEWA ( Capable to deliver knowledge) na sio CHETI CHA UALIMU. Wewe sio muelishaji bali mfinyu wa fikra
Hujanielewa hata kidogo............Lowassa hana ajenda yoyote ya udini na wala hajali hayo.......yeye anachojali ni kupora mali za umma..............lakini kama akibanwa sana aweza naye kurukia udini kama muasisi wa udini Jk ili kuwavuruga wananchi na kujichumia kile ambacho hajapanda...........................................kama JK anavyovuna Uraisi kwa jasho la Dr. Slaa........................Unaposhindwa kuelewa usisingizie wengine jaribu kutafakari zaidi itakusaidia............
 
Naomba kuungana na JK na Mzee wangu Kayanza, mtu akishiba ni rahisi kufanya maendeleo mengine, uwezi kukaa darasani na njaa asilani. NI lazima tuwe na uhakika kuwa kesho tutakula nini!! hivyo ni rahisi kukaa darasani na masomo fomula, definitions, calculas, yoote yaho yaka gota kichwani kwa makini. NJAA HAINA ADABU, watu washibe kwanza ndio akili itafanyakazi. So what I conclude, JK na Kayanza keep it up!! KILMO KWANZA MAZEEE!!

Napingana na mawazo yako katika hii mada, kilimo tulicho nacho kwa sasa hakijamsaidia Mtanzania kutokana na kukosa elimu ya kujikita zaidi katika kilimo kama cha wenzetu katika nchi ambazo zimefanikiwa katika kilimo. ni kweli huwezi kukaa darasani huku ukiwa na njaa, kilimo chetu kinatuwezesha kupata mlo lakini siyo maendeleo. hivyo ni vyema elimu kwanza itakayo kusaidia kuwa na kilimo chenye kukuletea maendeleo.
 
Gazeti la Tanzania Daima limetuhabarisha leo ya kuwa Mheshimiwa Mbunge wa Monduli ametofautiana na JK kuwa yeye anaamini nchi itangulize elimu kwanza badala ya kilimo kwanza.....

Lowassa amkosoa Kikwete

• Asema elimu kwanza, kilimo baadaye

na Salehe Mohamed, Dodoma

ALIYEKUWA Waziri Mkuu, Edward Lowassa, amesema serikali inapaswa kutanguliza Elimu Kwanza badala ya Kilimo Kwanza, ili kuwawezesha wakulima na wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu shughuli wanazofanya.

Lowassa alitoa kauli hiyo jana katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chamwino, mjini hapa baada ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na kuongeza kama elimu itapewa kipaumbele zaidi kuna kila dalili Tanzana ikapiga hatua katika nyanja za kilimo, uvuvi, ufugaji na nyinginezo.

Alisema mkulima mwenye elimu ya kutosha hataweza kulima kilimo cha kisasa pamoja na kuwasiliana na wanunuzi wa mazao yake.

“Mimi naona tungetoa nafasi kwa Elimu Kwanza halafu ndiyo ije hiyo ya Kilimo Kwanza; kuna nchi zimeendelea zaidi kwa sababu walianza kuwekeza kwenye elimu, naiomba serikali kuliangalia suala hili kwa umakini zaidi,” alisema Lowassa.

Aliongeza kuwa serikali ya sasa inapaswa itafute mbinu madhubuti ya kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana ambalo linawafanya vijana wengi kukimbilia mjini kwa lengo la kutafuta kazi.

Alisema tatizo hilo linaweza kutatuliwa iwapo huduma muhimu za kijamii, pamoja na shughuli mbalimbali za kiuchumi zitapelekwa vijijini.

Wakati akizindia mpango wa Kilimo Kwanza, Rais Jakaya Kikwete alizitaka sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kutekeleza na kufanikisha mpango huo akisema awali ushiriki wa sekta hiyo ulikuwa dhaifu hali iliyopelekea kudhoofika kwa mipango mbalimbali ya kilimo iliyowahi kutangazwa.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, ambaye alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Pinda, alisema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana lisipoandaliwa mikakati madhubuti litakuja kuiyumbisha nchi na kuleta mvurugano.

Alisema nguvu kazi kubwa ya sasa ni vijana na hawana kazi hivyo ni vema serikali ikajenga mazingira bora ya kuwawezesha kiuchumi pamoja na kujenga viwanda vitakavyosaidia kutoa ajira.

“Ukosefu wa ajira ni bomu la muda, tusipokuwa makini likija kulipuka nchi haitoweza kukalika, tuandae mazingira mazuri yatakayosaidia kuwepo kwa viwanda au kuwawezesha kiuchumi,” alisema Lipumba.

Alibainisha kuwa Waziri Mkuu ana wajibu mkubwa kuhakikisha kunaundwa Tume huru ya Uchaguzi ili kuepusha mizengwe inayotokea mara kwa mara kwenye chaguzi.

Naye Mwenyekiti wa TLP, Agustine Mrema, alisema Pinda ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi hivyo ni vema akautumia kurekebisha masuala mbalimbali ambayo ni kero kwa wananchi ikiwemo umaskini.

Sherehe za kuapishwa kwa Pinda, zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dk. Alli Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad na viongozi mbalimbali.

Wakati huo huo, wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamesusia kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikiwa ni msimamo wao wa kutomtambua Rais Jakaya Kikwete, ambaye wanadai alipata ushindi kwa sababu ya kuchakachua (kuiba) kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu.


Mheshimiwa Lowassa amesema bila ya raia kuwa na uelewa wa kutosha hata hicho kilimo kwanza utekelezaji wake utakuwa mgumu..............

Maono yangu yananiongoza kuamini ya kuwa JK hana mpango wa kumweka Lowassa kwenye baraza la mawaziri kwa sababu siyo za uadilifu au uchapaji kazi - JK hajali sifa hizo katika uteuzi zake na huzitaja tu ili kumwaga changa kwa wapigakura tu- lakini JK anamwona Lowassa atavuruga hesabu zake za kumrithisha Uraisi mzanzibari ambaye JK atamwandaa hivi sasa kwa madai ya kuimarisha muungano huku anaendeleza ajenda ya siri ya kuhakikisha maamuzi ya uanzishwaji wa mahakama za kadhi na nchi hii kujiunga na OIC hayatahojiwa na serikali inayoongozwa na mkristu...........bila ya kujali chama anachotoka................

Ninauhakika ya kuwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo nchi hii itakuwa imejiunga na OIC na mahakama za kadhi kuanzishwa .......................mbali ya JK jana kudai ya kuwa kuna nyufa za udini na serikali yake itafanya juu chini kuzishughulikia.................lakini ukweli ni kuwa kazi kubwa atakayoifanya kwa miaka mitano ijayo ni kuzikuza nyufa hizo kwa kutoa upendeleo kwa dini yake...............

Lowassa haya yote amekwisha kuyaelewa na ndiyo maana anaonyesha ghadhabu zake kwa kutofautiana na JK hadharani.................




Wakipata elimu wengi kutakua hamna wa kumburuta, bora wapige siasa za kilimo kwanza ambazo hawajui hata zinatekelezekaje na waendelee kuendesha nchi watakavyo ila lowasaa ana point kwa hili!
 
kila penye kutofautiana kuna ukweli ndani yake.
Elimu kwanza ndo mpango,
kilimo kwanza inabidi mtu uwe risk taker kutokana na hali ya hewa kwa miaka hii ilivyobadilika.
Je bila elimu tutaweza kuwa risk taker.

Japo watu wameelimika mpaka leo tz ss ni waoga wa kujaribu mambo.

elimu haileti maendeleo. Kinacholeta maendeleo ni elimu bora, nidhamu ya mali ya uma, na utashi wa dhati wa kisiasa, utokanao na wazalendo wa kweli.
 
Naomba kuungana na JK na Mzee wangu Kayanza, mtu akishiba ni rahisi kufanya maendeleo mengine, uwezi kukaa darasani na njaa asilani. NI lazima tuwe na uhakika kuwa kesho tutakula nini!! hivyo ni rahisi kukaa darasani na masomo fomula, definitions, calculas, yoote yaho yaka gota kichwani kwa makini. NJAA HAINA ADABU, watu washibe kwanza ndio akili itafanyakazi. So what I conclude, JK na Kayanza keep it up!! KILMO KWANZA MAZEEE!!

Sera inaposema kilimo kwanza haimaanishi ni kilimo hiki kidogo cha chakula (Ni vuzuri ukatumia akili kwa mambo madogo kama haya).
 
who ? lowasa arghhhhhhh!!!! please

Unachosikitika nini? Lowassa ana mabaya yake na mazuri yake, kama unamuona mtu mbaya haimaanishi kwamba hawezi kuongea point. Hii serikali ya awamu ya nne lowasa maamuzi kama mkuu wa serikali amefanya 2.5yrs, ila huyu mkwere amefanya 5yrs na ana more 5yrs
 
ni ukweli..we unafikiri wakulima watalima bila kuwa na ujuzi hata wa crop rotation....
 
Lowasa is 100% Right.......


Sure Lowasa is 100% Right. Huwezi kuendelea kwa kuwa na wananchi wajinga.

Ingekuwa kilimo kwanza basi watoto wao wangewapeleka huko vijijini kulima, lakini wana wapeleka nje ya nchi ili wapate elimu iliyo bora.
 
jk na lowasa wanajuana.wote ni marais wa nchi hii,nashangaa jk anamwogopa sana lowasa sijui kuna nini nhapo katikati,na tusipoangalia anaweza kumapa wizara
 
Wakipata elimu wengi kutakua hamna wa kumburuta, bora wapige siasa za kilimo kwanza ambazo hawajui hata zinatekelezekaje na waendelee kuendesha nchi watakavyo ila lowasaa ana point kwa hili!

Wakishiba hawatadumaa miili na akili zao wata reason out kama yule mtoto kwenye tangazo la haki elimu anaemuuliza mwalimu wake "mzee chilo" kwanini TZ ina rasilimali nyingi lakini watu wake masikini?

Unaweza kupewa elimu lakini kama umeathirika na udumazi akili yako ikadumaa utakuwa unasoma ili ufaulu mitihani na sio kujiuliza kwanini sindano inazama na meli haizami? matokeo yake tunakuja kuwa na maprof na dr wasio kuwa na tija kwa taifa. Mie naona chakula ni muhimu zaidi na kwangu kilimo ni jambo linalokuja kwanza then mengine. Huwezi kuwa na amani ukiwa na njaa kilimo kwanza itekelezwe kwa vitendo sio kwa semina!
 
Sure Lowasa is 100% Right. Huwezi kuendelea kwa kuwa na wananchi wajinga.

Ingekuwa kilimo kwanza basi watoto wao wangewapeleka huko vijijini kulima, lakini wana wapeleka nje ya nchi ili wapate elimu iliyo bora.

Lazima awe 100% na najua waTZ mnamkubali get ready for 2015 sitakai tena mje mumkatae maana hapa JF huwa wanachungulia kupima upepo kwa jinsi mlivyomsifia its a step forward kwenye mission yake ya Urais 2015.
 
Waungwana hutoa sifa panapositahili na kutoa sifa pasipositahili. Kwa habari hii mimi naungana na Lowassa.

Ila kwa kuwa serikali ni ya CCM na yeye ni kiongozi ndani ya CCM kwani nini asitumie vikao vya CCM kueleza hii maada ambao mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana nayo.

Mhe Lowassa nakushauri peleka hoja hii kwenye vikao ile sera za chama chenu ziende na zile za chama mbadala. CCM isione aibu kuchukua hii sera na kuitekeleza kwa vitendo. Kwani nia na madhuni ni kuendeleza taifa. Nadhani kwenye uchaguzi kuna chama kilichokuwa kinasema sera yake ingekuwa na pamoja elimu tena ya bure.

Bila elimu ufahamu wa binadamu katika kutenda kazi zikiwemo za kilimo ni hafifu.

JK alishasema pale Karimjee wakati anatangazwa mshindi kwamba atatumia zile sera nzuri za vyama pinzani katika kuboresha maendeleo.Tatizo tu ni kwamba JK anaposema maendeleo wengi wetu tunashindwa kuelewa anasema nini kwani mwishowe hutayaona anayoyasema.
 
Sure Lowasa is 100% Right. Huwezi kuendelea kwa kuwa na wananchi wajinga.

Ingekuwa kilimo kwanza basi watoto wao wangewapeleka huko vijijini kulima, lakini wana wapeleka nje ya nchi ili wapate elimu iliyo bora.

Nimpongeze Lowasa kwa kuliona la elimu,kwani hata siye Chadema kama sio ujinga uliokithiri TZ tungekuwa Ikulu.Sasa basi namwomba atusaidie hilo la elimu kumsafishia njia DR wa ukweli 2015.Tutamshukuru tu ila hatutampa nafasi kwenye serekali yetu.
 
Kwa kauli hiyo ni dhahiri el anaunga mkono sera ya cdm ya elimu bure.
Lkn kama kasema kinafiki ili ajisafishe ajue bado tunakumbuka manyanga yake na hulka yake ya kiherehere.
 
Back
Top Bottom