Live coverage on JamiiForums

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
572
2,169
1/7/2024

1719847600224.png

Vifo vinavyotokana na maandamano ya kushinikiza Rais Ruto aachie ngazi vyafikia 26, baada ya watu wawili zaidi kutokana na majeraha

Kevin Madanga (22) ambaye alipigwa risasi 3 wiki iliyopita amefia Nakuru na Daniel Kakai (17) mwanafunzi kutoka Bungoma aliyepigwa risasi Alhamisi iliyopita naye amefariki akiwa anaendelea na matibu. Siku ya tukio Daniel alikuwa maeenda saluni kukata nywele maandamano yakiendalea na alipigwa risasi wakati akijaribu kukwepa maandamano hayo

Kituo cha Habari cha CNN imeachia video ya tukio walilolinasa wakati wa maandamano ambapo polisi alirusha risasi na kuua si chini ya waandamanaji watatu ambao hawakuwa na silaha siku ya Jumanne 25/6/2024. Moja ya waandamanaji aliyepigwa risasi na kunusurika amapoteza uwezo wake wa kutembea, hivyo hatatembea tena katika maisha yake yote.


Tar 30/6/2024
Alipokuwa akihojiwa jana tarehe 30/6 na waandishi wa habari, Rais Ruto alisema japo amekubali kuondoa na kutokusaini Finance bill hiyo lakini anasikitika sana kwani bill hiyo ilikuwa na manufaa makubwa wa wakenya wote na ililenga kuikomboa kuingia kwenye madeni makubwa.

Alisema kuwa Wakenya wengi walioandamana kupinga mswaada huo hawajui kilichomo ndani ya bill hiyo bali wanafuata mkumbo.

Tar 25/6/2024

Waandamanaji kadhaa wafariki dunia kwa kupigwa risasi
Waandamaji zaidi ya Watano wameuwawa kwa risasi wakati Polisi wakipambana na Waandamanaji wanaopinga Muswada wa Fedha 2024

Chama cha Madaktari cha Kenya kimeripoti kusambaa kwa miili kadhaa ya Watu nje ya eneo la Bunge ambapo waandamanaji walivamia jengo hilo Jijini Nairobi

Wakati huohuo, Hospitali ya Taifa ya Kenyatta imeendelea kupokea idadi kubwa ya majeruhi asilimia kubwa wakiwa ni vijana

==============

Kama Gen Z walivyoahidi kulizingira bunge na kuizima Kenya nzima kwa maandano, ikiwa ni pamoja na kwenda Bungeni wamefanya hivyo, ambapo mpaka sasa wandamanaji wawili wanaripotiwa kupoteza maisha baada ya kupigwa risasi na polisi wanaotuliza ghasia.


Inasemeka zaidi ya wabunge 150 wamekwama bungeni baada ya waandamanaji kuvamia bungeni hapo. Baadhi waliweza kuchomoka kwa miguu huku wengine chini ya uangalizi mkali wa polisi.

Screenshot 2024-06-25 160926.png

Baadhi ya waandamanaji wakijichana katika moja ya vyumba vya bunge ambako ni maalum kwaajili ya kupata chakula.

Screenshot 2024-06-25 160849.png

Tarehe 23/6/2024

Ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la ACK Dayosisi ya Nyahuhuru nchini Kenya, ambapo Rais Ruto alisali, ilibidi hadi Wachunguji wapekuliwe kuhakikisha hakuna hali inakuwa shwari wakari wote ambao Rais atakuwa kanisani hapo.



=====

1719128286886.png

Mbunge Slyvanus Osoro, moja ya wabunge waliopokea maelfu ya jumbe kutoka kwa waandamanaji
Wabunge walazimika kuzima simu kukwepa maelfu ya jumbe za waandamanaji

Haya yanatiokea baada ya namba zao za simu kuchapishwa hadharani katika mitandao ya kijamii kwenye kampeni ya kuwashinikiza wakatae kupitisha mswada huo tata.

Wale waliopiga kura kuunga usomwe kwa mara ya pili Alhamisi ndio wanaopata tabu zaidi kwa kupokea jumbe nyingi kutoka kwa waandamanaji wakiwaambia wasahau kuchaguliwa tena kutokana na kuunga kwao mkono muswada huo.

“Simu zilikuwa nyingi, betri ya simu ilichukua dakika 15 kuisha moto. Tatizo kuu lilikuwa ukosefu wa maudhui hata kama mtu angeamua kuzungumza nao,” alisema kiongozi wa wengi bungeni Silvanus Osoro.

“Ukipitisha mswada huu, sahau kuchaguliwa tena,” ulisema ujumbe uliotumiwa mbunge mmoja.

Nambari nyingi za simu za wabunge zinazojulikana hadharani zimezimwa. Katika jitihada za kuthibitisha uhalisi wa namba zilizosambazwa kwa waandamanaji, Wabunge walitumiwa pesa nyingi kupitia Mpesa, ambapo jina la mtu husika huonekana na hivyo kutoa uthibitisho kuwa mwenye namba hii ni fulani kweli.

“Watu wengi walikuwa wakinitumia kiasi kidogo cha pesa, wakati mwingine kidogo kama shilingi mmoja, uwezekano wa kuthibitisha kama nambari ni yangu. Wengine waliomba niwatumie pesa,” Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa aliambia Taifa Leo.

“Nilipokea karibu Sh125,000, ambazo zilinifanya kutambua kuwa nina mashabiki huko nje. Baadhi ya watu waliuliza kwa nini nilipiga kura ya ‘ndiyo’ na walionyesha kusikitishwa, lakini nilipowauliza waeleze mswada huo hawakuuelewa.”

Vitisho hivi vimezidisha wasiwasi miongoni mwa wabunge hao, huku wengine wakionyesha hofu kuhusu usalama wao na wa familia zao.

Katika bunge, Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah alitoa malalamiko bungeni kuhusu kunyanyaswa na baadhi ya waandamaji hao.

Tarehe 21/6/2024

Reject.png

Gen Z watangaza siku 7 za maandamano baada ya wenzao wawili kuuliwa kwenye maandamano hayo. Waweka maazimio ya kutekeleza kwenye siku hizo 7;

Tar 21: Kushiriki mazishi ya Juma, kijana aliyeuliwa kwenye maandamano

Tar 22: Kusimamisha mziki mara kwa mara kwenye baa na klabu zote ambazo Gen Z huenda kujirusha na kusikiliza vibwagizo vyao vya: (Rito must go / Reject Finance Bill (Ruto lazima atoke, na Kataa Mswada wa Fedha)

Tar 23: Kuwazuia wanasiasa wote waliounga mkono muswada wa fedha kuhutubia kanisani

Tar 24: Kwenda bungeni na kwa dhumuni la kuwaona wabunge waliounga mkono muswada wa fedha na kuwaambia, "Endelea hivyo hivyo! Susia biashara za wasiliti hawa na kuwatenga kwa kuwasaliti wakenya milioni 54, na kukuanza kukusanya sahihi za kutosha kuwaondoa madarakani

Tar 25: Kulizingira bunge na kuizima Kenya nzima: Mgomo wa kitaifa kufanyika. Gen Z wawapa Wakenya wote wanaofanya kazi kwa bidii siku ya mapumziko. Wazazi waaswa kuwaweka watoto wao salama nyumbani kama juhudi za kuunga mkono kwa yanayoendelea mtaani. Hashtag ya #OccuppyParliament itatatumika vilivyo katika siku hii

Tar 26: Kutafuta Haki kwa Rex, kijana aliuliwa na kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandanano. Kutembelea Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) pamoja na kutembelea ukurasa na Instagram wa Polisi kudai haki ya Rex kwa hashtag ya #JusticeForRex

Tar 27: Kuzuia barabara kuu zote zinazoelekea katika jiji la Nairobi na kwenda Ikulu kushuhudia Rais Ruto akitia saini 'kutoa maisha ya Wakenya kwenye Utumwa' huku hashtag ya #OCCupyStateHouse ikitembea

Block main roads leading to Nairobi and #Occupy State House to witness Ruto sign our lives to slavery

=====

Kijana Rex Masai (24) afariki dunia kwenye maandamano baada ya polisi kupiga risasi kwenye maandamano jana usiku CBD Nairobi kwa waandamani waliokuwa mtaani bado zaidi ya saa mbili usiku.

Jambo hili limeongeza hasira zaidi kwa waandamanaji wakitoa maoni mtandaoni wakisema kifo cha Rex hakitaenda bure, wataendelea na maandamano mpaka wapate mabadiliko wanayoyataka

1718950504609.png

1718946780365.png

Maandamno yapamba moto, waandamanaji wasonga kuelekea Ikulu!



====

Wabunge 204 wamepiga kura kuunga mkono Mswada wa Fedha wa 2024, dhidi ya 115, ambao walipiga kura kuupinga. Mswada huo sasa unaelekea kwenye Kamati ya Bunge zima.

1718898588965.png

Baadhi ya wabunge wakitoa maoni baada ya wabunge 204 kuunga mkono Muswada wa Sheria ya Fedha 2024.

Polisi warusha bomu la machozi kwenye matatu! Abiria watoka mbio kwa taharuki kujiokoa wasiathirike na moshi huo.


Waandamanaji wamsaidia polisi aliyeumia kupanda kwenye bodaboda ili awahishwe hospitali.



Waandamanaji wakisaidiana maji ili kuosha macho yalioathiriwa na mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwatawanja.




Waandamanaji wakimwagiwa maji ili kusambaratisha mkusanyiko wa watu



Wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini humo wameingia Mitaani kupitia Maandamano ya kupinga Muswada wa Sheria ya Fedha unaolamilikiwa wakidai una vifungu vyenye Kodi kandamizi

Maandamano hayo yanaingia Siku ya 5 leo tar 20/6/2024 huku yakiwa na mafanikio ya kushawishi Bunge kuondoa baadhi ya Vifungu ikiwemo ongezeko la 16% ya Kodi kwenye Mikate na Kodi ya Kutuma Fedha kwa Simu.


====

Screenshot 2024-06-19 111348.png

Jana tarehe 19/6/204 Mbunge kutoka Mberee Kaskazini, bwana Geoffrey Ruku aliwasilisha Bungeni, muswada utakaowezesha Wakenya kufungwa kwa mwaka mmoja, faini ya Tsh. 2,000,000 (Ksh. 100,00) au vyote kwa pamoja kw awakenya watakaoandamana bila ya kuwa na vibali stahiki.

Kwa habari kamili soma: Mbunge awasilisha Mswada wa Kuwafunga Wakenya wanaoandamana bila vibali


====

nguvu.png

Jumanne tar 18/6/2024 ikiwa ni siku ya 3 toka maandamano hayo yaanze, Bunge lililazimika kubadilisha baadhi ya vifungu kwenye Mswada wa Sheria ya Fedha kutokana na shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi kutokana na maandamano hayo.

Zaidi soma: Nguvu ya Umma: Bunge lalazimika kubadilisha Muswada wa Sheria ya Fedha baada ya maandamano ya Wananchi

=====
Maandamano yapata sura mpya kwa Gen Z kuwa mtsari wa mbele kupinga Muswada huo

The #OccupyParliament protests in Nairobi CBD on Tuesday, digitally planned, physically execut...jpg
The #OccupyParliament protests in Nairobi CBD on Tuesday, digitally planned, physically execut...jpg
Maandamano ya #OccupyParliament huko Nairobi CBD siku ya Jumanne, yaliyopangwa kidijitali, na kufanyika mtaani yakiongozwa na kizazi kipya maarufu kama GenZ yavutia wengi, yamefanya mabadiliko makubwa katika historia ya waandamanaji nchini Kenya. 'Wapiganaji wa kibodi (keyboard warriors) na waandamanaji mtandaoni' waliwashangaza wengi walipokuwa wakiendesha kampeni mtandaoni mpaka kwenye kushiriki kwao kwenye maandamano hayo kwenye mitaa mbalimbali Kenya.

The #OccupyParliament protests in Nairobi CBD on Tuesday, digitally planned, physically execut...jpg

Waandamanaji hao wenye sura nzuri, waliovalia mavazi ya kifahari na vifaa vya maridadi, walionekana kutokuwa na madhara huku wakiwa na mabango yao yaliyobeba jumbe mbalimbali. Walikusanyika kwa amani katika CBD ili kuandamana hadi Bungeni, lakini wakavurugwa na polisi wa kupinga ghasia jambo ambalo linataja kuwa sababu kuu ya kufanya maandamano kuchukua sura nyingine na kuwa makali zaidi.

The #OccupyParliament protests in Nairobi CBD on Tuesday, digitally planned, physically execut...jpg


Watu mashuhuri, wasanii na wenye ushawishi waliunga mkono, na kuongeza safu ya kuonekana na uhalali wa maandamano. Hata kama zaidi ya 250 walikamatwa, waandamanaji waliofungwa pingu walionekana wakiimba nyimbo za kuipinga serikali, bila kuvunjwa moyo na vitendo vya polisi. Moyo wao uliendelea kuwa juu, huku wengi wakiendelea kuimba hata wakiwa wamezuiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, wakidumisha msimamo wao wa kukaidi.

The #OccupyParliament protests in Nairobi CBD on Tuesday, digitally planned, physically execut...jpg

Upangaji mkakati wa mtandaoni wa maandamano hayo, kurekodi kila hatua, na kushiriki kwa haraka matukio kwenye mitandao ya kijamii uliwaacha polisi bila chaguo ila kuwashughulikia waandamanaji kwa tahadhari, na kwa mara ya kwanza, hapakuwa na ripoti yoyote juu ya uporaji, uharibifu, au vifo vya raia, isipokuwa kwa polisi ambao walifanya vurugu kali kwa waandishi wa habari wanaoripoti maandamano hayo na polisi mmoja aliyejeruhiwa kwa mikono yake kukatika baada ya bomu la machozi kumlipukia.

The #OccupyParliament protests in Nairobi CBD on Tuesday, digitally planned, physically execut...jpg
waaswa
 

Attachments

  • 1719047562327.png
    1719047562327.png
    312 bytes · Views: 8
  • 1719047821585.png
    1719047821585.png
    312 bytes · Views: 10
Kundi la vijana limeandamana mjini Nairobi, Kenya leo Juni 20, 2024 kuishinikiza serikali kufuta mapendekezo ya muswada wa sheria ya kodi, ambao wanadai hauna tija kwa wananchi.

Vijana hao wamedai muswada huo haukushirikisha wadau wengi wakiwemo wanasiasa, ili uweze kujadiliwa kwa maslahi ya taifa jambo ambalo haliwezi kukubalika kwa mujibu wa sheria.

“Muswada huu fedha una utata na haujapangwa wala kujadiliwa na wanasiasa na huu ni uasi, “ wamedai vijana hao.

20240620_145647.jpg
 

Attachments

  • TMIL8zx5vhCI_65O.mp4
    9.9 MB
1719002583235.png

Kenya's Generation Z are yet again set to express their undying determination in opposing the Finance Bill 2024 with a new set of demonstrations planned to run for the next week.

From #OccupyParliament hashtags to #OccupyStateHouse and #JusticeForRex, the youth have continued to be dynamic in their online presence with this time coining yet another hashtag, #totalshutdown.

A poster widely shared on social platforms revealed that the youth will be undertaking a seven-day protest which they say is meant to show solidarity for their slain colleague and also push the government to heed the plight of Kenyans by rejecting the Bill which has since sailed through the second reading.
Dubbed '7 days of rage', the demonstrations will also serve as a warning to Members of Parliament who voted in support of the Bill on Thursday against the will of their respective constituents and will also coerse multi-agency bodies to probe incidences of police brutality meted out by protesters.

"We reject the Finance Bill in its entirety. And despite our peaceful protests, police have responded with bullets, killing two of our own, maiming many others and one person is in critical condition. We refuse to be silenced, so we're marching on," read a section of the poster.

On Friday, June 21, the youth are set to visit the City Mortuary, attend Juma prayers at Jamia Mosque, and give water to those leaving after the prayers.

On the second day, Saturday, June 22, the youth have extended a unity call to bars and clubs that Gen Z frequent, where music will stop at midnight and everybody will listen to a national crescendo of, 'Ruto must go, and Reject Finance Bill'.

Sunday, June 23 will see a number of activities including holding into account the 204 MPs who voted in support of the Bill in churches. The Gen Zs plan to rally churches to deny the said MPs platforms to address congregants.
Monday will see a courtesy call stating, "Endelea hivyo hivyo!' made to the MPs' who supported the bill at their respective constituency offices and their constituents would be urged to boycott any businesses affiliated with them. The youth also plan to mount support by collecting signatures in order to recall them.

The notice says that Tuesday will mark the second #OccupyParliament protest where GEN Zs warn of a 'Total Shutdown' of the country through a nationwide strike.

" Gen Zs are granting all hard-working Kenyans a day off. Parents keep your children at home in solidarity," stated the notice.

Gen Zs on Wednesday will be leading a call to action demanding justice for the death of Rex who was killed during Thursday's protests in Nairobi. They are expected to visit IPOA offices and also the Inspector General of Police Japhet Koome.

Next week Thursday will mark the climax of the protests where Gen Zs have warned that they will block main roads leading to Nairobi and march to State House under the slogan #OccupyStateHouse. Being the day President William Ruto is expected to sign the Finance Bill into law, Gen Zs say they will be going to 'witness Ruto sign our lives into slavery'.
1719002537940.png
 
Back
Top Bottom