Lissu usimjibu Askofu Gwajima

hahahaha Ngwajima si ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema?
 
Ukishakuwa "mungu" na umeshawahakikishia wafuasi wako pepo unaweza fanya shughuli yoyote ile kwenye madhabahu yako, siasa, umbea twende tu. Mbingu yako kwanini upoteze muda kuwafundisha neno?
 
Watunga sera na sheria wetu ndio hawana uzalendo. Wapinzani mwawasingizia. Wawekezaji wanatuibia kupitia sheria zetu wenyewe. Ifuatayo ni mirahaba kwa Botswana(nimeipata google): 1)precious stones 10%, 2)precious metals 5%, 3) other minerals or mining products 3%. Ni kiasi gani walilipwa kuandika 4% wanajua waliohusika.
 
Leo hii mliokua mnamsifia Gwajima mmeanza kumponda tena kwa kigezo cha ninyi kumtetea Tundu Lisu..any way swala la mchanga tunaomba Rais akamatie hapo hapo wala asiachie kenge kutuibia sisi.hvi ulishawahi kumkodishia mtu shamba na mipaka ukampa then baada ya muda ukirudi kutembelea shambani unakuta kalima mpaka nje ya mipaka uliyompa?hivyo ndivyo swala la makontena ya mchanga lilivyo,msibwabwaje kuhusu mikataba.mikataba ilikua baada ya kuchambua dhahabu yote wanaweza peleka huo udongo kuchambua madini mengine,wao wakawa wanachambua dhahabu ktk mchanga kiasi na mwingine hawafanyi chochote wanaubeba kama ulivyo.nje na makubaliano ya mkataba huo mnaousema,Rais na watu wake wamejua hilo.hongera kwa TISS na RAIS wetu.na uongoze nchi hii mpaka miaka kama 30 hivi ili inyooke
 
Lusu hana ubavu wa kupambana na Gwajima ambaye ni mkweli Daima. Lisu siyo mzalendo ni mkimbizi rohoni mwake elimu duni sana. Kama anajeuri athubutu kupambana na Dude.
Apambane na Gwajima! kuhusu nini? Naomba ndg zangu tuwe watulivu ili tuache nafasi akili na maarifa yetu yapambanue mumbo, ipo tofauti kubwa kati ya Gwajima mchungaj/askofu na Tundu lisu Mwanasheria, mwanasheria wa aina ya Lisu kulumbana na Askofu kwa maswala ya elimu ya kiroho ni kichekesho, ndivyo hata kwa Gwajima, hivyo basi Askofu katumia haki yake ya kikatiba kutoa mawazo yake ni jambo jema, lakini Lisu alizungumza kitaaluma, jambo ambalo simwana taaluma tu anaweza kubisha na kusema yasiyo ya kitaaluma ,kwa mfano Askofu angetwambia endapo itafunguliwa kesi ni kwa namna gani tunaweza kushinda, na nchi kuepuka kulipa gharama ambazo mwisho wa siku ni wananchi wa kawaida tutabebeshwa mzigo, mwisho, naomba wataalamu wa sheria walizungumzie hili swala na muelekeo wake bila kuingiza siasa
 
Back
Top Bottom