Lissu alaani agizo la Magufuli kwa Wakuu wa Mikoa

Kwa kifupi hakuandaliwa kuwa mtawala.
Ushauri wa bure Mh.Magu hata Roma haikujengwa kwa siku moja.
Pia elewa kuwa askari wetu hata hao wastaafu IQ zao hazipo sawa na maoni yako.Maelekezo unayowapa utaiingiza nchi kwenye
machafuko....HATUHITAJI KUFIKA HUKO.
 
Kamateni wale walioidhinisha vimemo vya kutoa makontena bandarini,mkimaliza rudisheni zile nyumba zetu za serikali mlizouziana kishkaji kwa bei ya kutupa,halafu tena muende mkauze yale mashangingi mnayotembelea,nitajua kweli hii ni serikali sikivu.
 
Kwani wewe huna Ndugu anayependa upinzani, unaweza kukuta mke wako yuko upinzani au mwanao

Hakuna kwa maana wote ni wale wale Majizi ya mali za umma na wauaji wa Tembao hapo sijawaweka wauza unga sasa saa ngapi atakuwa upinzani??
 
Kuna miners [wafanyakazi wa migodini] na walinzi wa usikuwanaotinga kazini usiku na asubuhi ndio muda wao wa kupumzika,je nao wasicheze pool au wasinywe bia mchana?kwani mchana wa wengine ndio usiku kwao na usiku wa wengine ndio mchana kwao.
kwa hoja yako hii unawezaje kutofautisha mfanyakazi wa mgodi na wengine ili kuwaruhusu waingie baa saa 2 asubuhi na kucheza pool
 
Kuna miners [wafanyakazi wa migodini] na walinzi wa usikuwanaotinga kazini usiku na asubuhi ndio muda wao wa kupumzika,je nao wasicheze pool au wasinywe bia mchana?kwani mchana wa wengine ndio usiku kwao na usiku wa wengine ndio mchana kwao.
Umewasahau wavuvi
 
Suala ni kupoteza muda kwa kucheza pool wakati wa kazi! Kama amekesha overnight kazini basi apumzike home si ktk pool table! Hata hivyo wakishakamatwa watahojiwa na kupelekwa ktk kambi maalum wakapige kazi kwa sasabu asofanya kazi na asile!
 
  • Thanks
Reactions: nao
Tundu Lissu anatafuta kick. Tulizoeshwa kuona wakuu wa mikoa wakiwa ni wapambe wa viongozi wa juu. JPM anataka waende wakaifanyie kazi mishahara yao, na wasiishie kuwa wapambe na watu wa majungu. Uzembe unaolisababishia umasikini taifa hili una mwisho wake. Zile akili za awamu ya nne wakati watu walizoea kumuona rais akitabasamu kwa kila mtu, lazima zibadilike. Tuwe serious kwa faida ya kulikomboa taifa hili, ule muda wa kuchekeana hovyo umeshakwisha, Tundu Lissu na wenzake wanapaswa kuufahamu ukweli huo.
Kwa hiyo unakiri hawamu ya nne ilikua futuhi na hii ni maigizo?
 
Suala ni kupoteza muda kwa kucheza pool wakati wa kazi! Kama amekesha overnight kazini basi apumzike home si ktk pool table! Hata hivyo wakishakamatwa watahojiwa na kupelekwa ktk kambi maalum wakapige kazi kwa sasabu asofanya kazi na asile!
Unawapangia watu jinsi ya kupumzika?
 
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu, ametoa maoni yake kuhusu kauli ya Rais Magufuli ya kuwaagiza wakuu wa mikoa kawakamata vijana wanaocheza pool muda wa kazi.

Mwanasiasa huyo maarufu, alisema ni wazi kuwa agizo la Rais Magufuli linataka kuchochea matumizi mabaya ya madaraka kwa wakuu wa mikoa na wilaya nchini.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ambayo ndio inasimamia agizo hilo, inawapa mamlaka ya kipolisi wakuu wa mikoa na wilaya kukamata watu wanaovunja sheria pale ambako hakuna polisi.

Alisema sheria hiyo pia inaeleza kuwa mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 na aliyemkamata anapaswa kuandika maelezo ya sababu za kumkamata.

“Sifahamu kama maelekezo hayo wamepatiwa au wameelekezwa tu wakamate wanaovunja sheria? Lakini pia wafahamu sheria hii inaruhusu kiongozi huyu kumkamata mtu kama hakuna polisi na kama wapo, sheria hii haimruhusu kufanya hivyo.

"Siku hizi kila tukio mkuu wa wilaya anaongozana na OCD (mkuu wa polisi wa wilaya), je ni wakati gani atakamata watu kama si kutaka kuvunja sharia?” alihoji.

Lissu alieleza agizo hilo ni wazi litasababisha wakuu hao wa mikoa na wilaya kukamata hata wasio na hatia.

“Wameelezwa tu kuwa wakamate watu wawaweke polisi, lakini hawajapewa maelezo ya sheria hii inayowasimamia, hivyo ni hatari kwa jamii, matokeo yake ni muendelezo wa matukio kama kukamatwa kwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Paul Makonda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Konondoni,” alisema.

Chanzo:Nipashe


Hakuna cha matumizi mabaya ya madaraka, vijana warudi vijijini wakalime. Hii nchi itajengwa na vijana kwa kujihusisha na shughuli za kilimo siyo kushinda kwenye pool table wakati huo wakifanya kazi za deal za kuchora mishemishe za wizi

Lakini siwashangai sana CDM na kauli mbiu yao ya kutetea maovu maana kwa sasa ndiyo agenda yenu kuu
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom