Lissu akiondoka Chadema, hakuna Mwana-Chadema ataondoka kwenye chama kumfuata Lissu

Kuna kaukweli, aliyeharibu ni mbowe, mtu miaka 21+ Bado unalazimisha kugombea tu? Alipaswa kukaa pembeni
 
Shida siyo bisu la Mbowe au Lisu et Al kuhama chama, shida itakuwa CHADEMA kitabaki kuwa cha watu wa aina ipi, wataweza kurudisha imani za watu? Wataendesha siasa za aina gani wakati watu wanaamini watu Hawa hawana tena jambo la maana la kuwa Fanya wawe wapinzani
 
Hoja za Machawa utazijuwa Tu ...Hana point hata moja Ni ushabiki Tu.....kwenda zako hukoπŸ‘†πŸ€”πŸ‘†
 
Alipoitisha maandamano baada ya kushindwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 uliandamana!?
Aliitisha maandamano akiwa Belgium.Huyu na Lema ni nusu hapa nusu Ughaibuni.
Lema alipoona muda wa kusema kweli umewadia na inatakiwa milioni 30 ya Mkutano Mkuu huyoo Canada. Mwenzake kapiga kimya tokea 2011 hajachangia Chama hata Mia.Matamko na kuropoka havijengi Chama.
 
Halafu leo eti HAWEZI kuchangia watu wataila. Yaani watakula hela ambayo hajachanga! Ahahahahaha!!!
 
Reactions: Tui
Kwani kabla ya Lissu ilikuwa na Wanachama?
Tena Lisu mwenye alikuwa NCCR Mageuzi.Alibadili nini?Watu wamekumbwa na kufuata mkumbo.Hakuna cha maana Lisu alichofanya Chadema na atashindwa na atatulia kwani hana uwezo wa kuanzisha Chama chake.Marehemu Maalim Seif aliiacha CUF na kuanzisha. ACT Wazalendo.Na wa challenge si mnadai mna wafuasi wengi anzisheni Chama chenu.Kama hamjageuka Chauma nyingine.Kuendesha Chama cha Siasa sio lelemama.Mna kiburi hata milioni 30 ya kuchangia Mkutano Mkuu hamna kila siku Ma Press Conference zisizo na kichwa wala miguu.
 
Hakuna mwenye akili timamu anayeunga mkono umwenyekiti wa Mbowe usio na kikomo. Mbowe amejidhalilisha, amejiabisha na kuonekana ni mtu anayeiongea demokrasia mdomoni, lakini hana uwezo wa kuiishi, ndiyo maana anakosa ujasiri wa kuongoza mapambanao ya kuougania demokrasia.
 
sio kweli
 
Kama wewe Ukifa hakuna mtu atakayelia πŸ˜…πŸ˜ƒπŸ˜…πŸ˜ƒπŸ€ΈπŸ€ΈπŸ€ΈπŸ™πŸ™πŸ™

Kaka unatoa wapi vichekesho hivi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…