Linux (Ubuntu, kubuntu, Debian, fedora, linux mint, kali linux, android etc) special thread

Badala ya ku-install vpn katika ubuntu yako, unatakiwa uwe na configuration files zilizo na extension ya *.ovpn
Hayo mafile unaweza kuyapata kwa website ambazo zinatoa huduma za bure kabisa kwa huduma ya vpn, mfano vpnbook ambayo mafile yake yanayokuunganisha na seva waweza pata hapa.
Free VPN Accounts • 100% Free PPTP and OpenVPN Service
Download mafile yaliyo upande wa openvpn, kwa chini kuna username na password utakazojaza ili kukuunganisha na openvpn server.
Extract mafile yako na kisha weka moja ya hayo mafile popote hata kwenye Desktop,
Ukishaweka kwenye Desktop, ili kuunganisha na server kuficha IP yako andika code zifuatazo

Code:
openvpn --config jina_la_file_ulioweka_desktop

Kumbuka kama utakuwa na maujanja openvpn inaweza ikatumika hata kupata free internet kama ukiwa na VPS.
 
mi natumia Ubuntu.....mwaka wa 5 sasa.......sijawahi waza kutumia windows....... nipo na Gmac OS baada ya kutomia sana pear Linux .
Nilianza kutumia Ubuntu mwaka 2010 na mwaka 2014 nikaachana nayo nikaanza kutumia Kali Linux mpaka sasa nimeshaisahau windows kabisa ingawa pc yangu ina dual booting
 
JE WAJUA UNAWEZA KUTENGENEZA SHORTCUT ICON KWENYE UBUNTU KAMA ILIVYO WINDOWS OS?
kufanikisha hili kompyuta yako inatakiwa uinstall software ya launcher au kuuandika lines kwenye terminal.
kwanza install software kwa command japokuwa huwa inakuwepo moja kwa moja ila unapaswa tu aunadike code zifuatazo.
Code:
sudo apt-get install --no-install gnome-panel
halafu andika code zifuatazo
Code:
gnome --desktop-item-edit --create-new ~/Desktop
itatokea dialog ikikuuliza jina la software unayotaka kutengeneza desktop icon, na command ambayo hiyo soft inafunguliwa kwenye terminal, kwa mfano ukiwa unataka shortcut ya blender, jina la application ni blender na command yake ya kufungua application ni blender.
kumbuka kufungua terminal unaweza bonyeza ctrl+alt+T
 
ENGLISH DICTIONARY.
zipo dictionary nyingi zingine zikiwa kwenye mtindo wa GUI nyingine ni za command lines kupitia Terminal.
Moja ya English Dictionary nzuri ni ile ya artha ambayo ni GUI na nyepesi kutumia
andika code ifuatayo kwenye terminal.
Code:
sudo apt-get update
sudo apt-get install artha
 
natumia linux mint 18 - 64bit nina wine ila kuna aplicación za window nimeshindwa ku install
 
Mbali na kuweka software kwa kutumia terminal, lakini pia unaweza ukainstall software kwa njia ya kawaida vile kama android ambapo kuna google play basi kwenye ubuntu kuna Ubuntu Software Center na ni njia rafiki kabisa.

Lakini njia ya terminal ndio nzuri kwa sababu unaweza kuta software zingine zipo outdated hivyo inahitaji manual way kuiweka, lakini pia kuna third party softwares ambazo repositories zake hazipo ubuntu, hivyo itakupata ku-add kwanza mafolder yake kwa njia ya terminal. Ndo maana njia ya terminal inakuwa ni bora zaidi.

Pia kama ww ni developer, unahitaji source codes za baadhi ya software za ubuntu uzitumie basi njia nzuri ya kupata hizo source code ni kwa njia ya Terminal ambayo utaipata kwa kubonyeza ctrl+alt+T.
 
Linux mint ni sister os ya ubuntu, huwa inapotoka ubuntu tu na linux mint pia hutoka.

Linix mint uzuri wake inakua preloaded na codecs kwa ajili multimedia files kama sauti na video, ambapo kwenye ubuntu ukishasanikisha inabidi ufanye hivyo manually.

Ubuntu huwa inatoka mwezi wa 4 {April} na mwezi wa 10 {October} kila mwaka, hivyo kwa sasa iliyoko ni 16.10 na linux mint pia ni hivyo, mwezi wa 4 zitatoka, kwa ubuntu huwa na herufi LTS kwa maana ya long-term support kwa kawaida ni 2 years ikizidi hiyo hutapata support kama ilivyo kwa xp kwa sasa hivi, hivyo unashauriwa uwe una upgrade kila toleo jipya likitoka.....

Hongera kwa mleta uzi, tuendee kushirikishana kila inapobidi

Cheers
 
Back
Top Bottom