IkuluKwetu
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 535
- 393
Mustapha Sabodo anaweza kumjibu mleta mada vizuri zaidi.
Tupe sentensi sahihiIf it were me? Mh! Acha nifanye ni typing error.
Jamani si lazima kutumia English! Wewe hujui english specifically pronouns and conditional sentences! Sasa hii If it were me I will ......,jamani hizi Dv 5 za kata shida kweli !
Nimemsikia Rais Dr.John P . Magufuli akitupa "dongo" kuwa kuna hata Vyama vya siasa ambavyo ni mabingwa wa kuitaka Serikali kuhamia Dodoma lakini wao makao yao Makuu yako Dar es Salaam! Wadau ebu mnijuze licha ya ofisi za CHADEMA Makao Makuu pale Kinondoni Makaburini mtaa wa Ufipa kutokuwa na hadhi wanazo hata ndoto za kuhamia Dodoma! ?Mtu mwenye akili nzuri akitaka kujua ni lini CHADEMA wanaweza kukabidhiwa Ikulu ya Magogoni ni kuangalia hadhi ya Ofisi yao na Ikulu ilivyo! Ni Mlima Kilimanjaro na Kichuguu! Mlango wa ofisi yao utadhani ni "frame" ya Butchery pale Shekilango Legho! Msitoe Mapovu,njooni na maelezo ya maana na pia m-justfy ruzuku mnazotafuna na fedha za wafadhili! Pia elezeni ni kwa nini Lowass
a hatumii hizo "frame" zenu badala yake anatumia "godown" zake !?
Watu wa aina yako ndiyo mnaowafanya viongozi wetu wawe mahiri wa kuongea "pumba", mtu mwenye akili timamu hawezi kushabikia kila pumba itikayo vinywani mwa watu wanaojiita " viongozi".Suala la serikali kuhamia Dodoma si suala la kichama,ni takwa la kikatiba,ni katiba inayotamka uwepo wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kutaja makao makuu ya serikali husika.Kumsikiliza kiongizi akihoji wanaoihimiza serikali kuhamia Dodoma huku wao wakibakia Dar-es-salaam,na wasikilizaji wakaitikia kwa mbwembwe na vifijo huku wengine wakiibeba pumba hiyo na kuitupia Jf,ni upumbavu iliovuka vigezo vya mtu kuwa mpumbavu.
Dodoma haikutajwa kuwa makao makuu ya chama,ilitajwa kuwa makao makuu ya serikali,bila kujali ni serikali ya chama gani iliyopo madarakani.Tunapohoji kwa nini serikali haihamii Dodoma,tunaitaja serikali,si chama cha mapinduzi.Kama ccm haifungwi na takwa la serikali kuhamia Dodoma,iweje wewe kiwavi jeshi uihusishe CHADEMA na kuhamia Dodoma?Jaribu kutumia akili yako kufikiri,jukumu la kufikiri ni la kwako,hupaswi kuliacha kwa mtu mwingine.
Tatizo Watanzania tumeacha kufikiri,badala yake tumekabidhi jukumu hilo kwa viongozi,sisi tumebaki kushabikia fikra zao hata kama wanayoyafikiri na kuyasema ni kinyume na misingi iliyoliasisi Taifa letu,tumekuwa watu wa kushangilia vijembe vya kisiasa badala ya kukaa chini na kuutafakali kwa pamoja mustakabali wetu kama Taifa.
Viongozi wetu kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa wanaufahamu udhaifu wetu,ndiyo maana wamekuwa wabunifu wa aina mbalimbali za ulaghai wa kisiasa kwa sababu wanajuwa tunavutiwa sana na ulaghai na uzushi kuliko Ukweli.
Ofisi za chama chochote hapa nchini,kiwe ccm au CHADEMA hazijawahi kuwa kikwazo cha Maendeleo yetu kama Taifa,kuuhusisha uduni wa Taifa letu na ofisi kuu za vyama vyetu ni upuuzi unaopaswa kupuuzwa kwa kiwango kinachostahili.Ni walevi wa itikadi za vyama na wale waliokabidhi jukumu la kufikiri na kutenda kwa watu wengine mithiri ya enzi za "zidumu fikra za mwenyekiti", ndiyo wanaoweza kushangilia pumba hiyo kwa kigezo cha kuwa imetoka kwa mkubwa.Wenye akili timamu hawawezi kuipa uzito wowote hiyo kauli ya kisiasa isiyo na mashiko yoyote,zaidi sana wataishia kuibeza kama wanavyoendelea kuzibeza sarakasi nyingine zinazoendelea nchini.
Akili za kushikiwa ! Hawa ndo utasikia wanasema wanamuunga Magufuli mkono na si CCM. Hujui Chama ndo kinaunda Serikali baada ya kushinda uchaguzi! Watu kama wewe wanadhani CCM wameweka Makao yao Makuu pale Dodoma labda ili wawe karibu na nyama za mnadani Subirini Bunge litaonyeshwa live ili mfurahie mipasho ya akina Msigwa!Huna hoja. Chama na serikali ni vitu tofauti kabisa.
Huna lolote baada ya kupigwa chini hapa Musoma sasa unasaga lami tu! Tanga labda uniambie uko njiani unaelekea Mombasa kutafuta biashara!Njoo Tanga mtoa mada tuuze juice ya miwa mama
Hahahahahah dah umemalizaMbona ofisi yako ipo bar?
Mbona na wewe umeandika kiswanglish.Jamani si lazima kutumia English! Wewe hujui english specifically pronouns and conditional sentences! Sasa hii If it were me I will ......,jamani hizi Dv 5 za kata shida kweli !
Hivi hizo ruzuku mnafanyia nini?Nimeangalia hii post nikajua vijana tumebaki na akili za kusukia ukindu na kuvukia barabara tu, tusahau kabisa kuhusu akili za kutafakari mambo na akili za kuleta maendeleo.Utafananisha vipi ikulu na ofisi za chama cha siasa?Ikulu ilijengwa na inakarabatiwa na kodi za wanachi wote bila kuangalia itikadi ilhali chama cha siasa kinajiendesha kwa ruzuku kidogo kutoka serekalini na vijimichango kidogo kidogo kutoka kwa wanachama wake, Na pia ukiangalia majengo na makao makuu ya CDM na CCM huwezi kuyalinganisha kwani CCM imekuwa chama dola na chama kimoja tangu 1961-1992 wakati huo wananchi wote walikuwa wanajitolea michango kwa ujenzi wa ofisi za chama sasa inakuwaje unawalinganisha na chama chenye umri wa miaka takribani miaka 25.
Hamna lolote,mkiambiwa ukweli ni mapovu ndio huwatoka!Hakika wewe ni mpuuzi
If it were me? Mh! Acha nifanye ni typing error.
Wameshindwa kujenga ofisi za maana basi hata mlango waweke wa maana kwenye hiyo frame yao wanayoita ofisi kuu!Hivi hizo ruzuku mnafanyia nini?
Ofisi hamjengi bali mnaishia kujenga majumba na mahoteli binafsi tu
Ofisi za mikoani hazipati hiyo ruzuku
Fedha za kampeni mnapitisha michango kwa style ya makapu ya sadaka
hata zile bilioni 10 za babu mmeshindwa kujengea ofisi??
Mkipewa nchi mtaweza??
Ukweli gani? CCM ndo INA makao makuu yake dodoma, ni bora andiko lako ukamprlekea mwenyekiti Wa CCM,Hamna lolote,mkiambiwa ukweli ni mapovu ndio huwatoka!
Nenda kaangalie maneno yaliyofuatia baada ya "if it were" ndio ulete hizo comment sio unadandia garimoshi kwa mbele.Usitafute aibu. Jua kwanza matumizi ya "if" - kusema "if it were me or if it were me" ni sahihi!! Usitake kukariri kwa kusema "I au it" lazima vifuatwe na "was". Usichanganye swala hili ni plural ukadhani "were" inawakilisha "wingi" na kumfanya aliyeitumia kama amefanya kosa. Siendelei na sentensi ya mleta mada tungo lakini kwa ulichosema, haukuwa sahihi.